STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, April 2, 2014

Real Madrid yaifumua Dortmund, Chelsea yafa kwa PSG

Gareth Bale scores for Real
Bale akifunga bao lake

Ezequiel Lavezzi
Lavezzi akishangilia bao la kwanza alililoifungia PSG wakati wakiiangamiza Chelsea mjini Paris
REAL Madrid imejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya muda mfupi uliopita kuifumua Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa mabao 3-0, huku Chelsea ya England ikikong'otwa ugenini kwa m,abao 3-1 na PSG ya Ufaransa katika mchezo mwingine wa robo fainali.
Madrid inayosaka taji la 10 la Ulaya na baada ya kupita zaidi ya miaka 12 bila kulitwaa tzngu ilipofanya hivyo mwakaq 2002, iliutumia vyema uwanja wa nyumbani kwa kuwashtukiza wageni kwa bao la mapema.
Bao hilo liliwekwa kimiani na Gareth Bale katika dakika ya tatu tu ya mchezo akimalizia kazi ya Daniel Carvajal kabla ya ya Isco kuongeza la pili dakika ya 27 na kudumu hadi wakati wa mapumziko.
Mwanasoka Bora wa Dunia wa FIFA, Cristiano Ronaldo alihitimisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la tatu dakika ya 57 akimalizia kazi ya Luca Modric na kuiweka Real katika nafasi nzuri kabla ya mechi ya marudiano wiki ijayo.
Katika mechi nyingine iliyochezwa mjini Paris Ufaransa,wenyeji PSG waliifanyia kitu mbaya Chelsea kwa kuizabua mabao 3-1 na kujiweka pazuri kufuzu nusu fainali kama itakomaa mechi yao ijayo mjini London.
Ezequiel Lavezzi aliifungia wenyeji bao la mapema la dakika 4 kabla ya Chelsea kuchomoa kwa mkwaju wa penati kupitia Eden Hazard katika dakika ya 27 na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa nguvu sawa kwa kufungana bao 1-1.
Kipindi cha pili kilikuwa kiama kwa Chelsea baada ya David Luiz kujifunga bao kdakika ya 61 kabla ya javier Pastore kumalizia udhia kwa kufunga bao la tatu katika dakika xa nyongeza na kuiweka PSG katika nafasi nzuri ya kusonga mbele, ingawa Chelsea siyo ya kubezwa kutokana na kuambulia bao hilo la ugenini linaloweza kuwabeba kama wakishinda Stanford Bridge kwa mabao 2-0

As Roma yaiua Parma na kupunguza pengo la pointi kwa Juve

Francesco Totti celebrates his goal against Parma
Totti akishangilia bao lake aliloifungia As Roma wakati wakiiua Parma
KLABU ya AS Roma imezidi kupunguza pengo la pointi na vinara wa Ligi ya Italia, Juventus baada ya usiku huu kuicharaza Parma mabao 4-2 katika mfululizo wa ligi hiyo maarufu kam Seria A.
Gervinho alianza kuiandikia wenyeji Roma bao katika dakika ya 12 kabla ya wageni kulirejesha katika dakika tatu baadaye kupitia kwa Acquah na Francisco Totti akiiongezea Roma bao la pili dakika ya 16.
Mabao hayo yalidumu hadi mapumziko na katika kipindi cha pili, Roma walianza kwa kufunga bao la tatu kupitia kwa Pjanić katika dakika ya 49 kabla ya Taddei kuongeza la nne dakika nane kabla ya pambano hilo kumalizika.
Hata hivyo wageni walijipatia bao lao la pili la kufutia machozi katika dakika ya 90 lililofungwa na Biabiany.
Ushindi huo umeifanya Roma kufikisha pointi 73, nane pungufu na za vinara wa ligi hiyo Juve yenye pointi 81.

Timu ya watoto wa Mitaani waendelea kutamba Brazili


TIMU ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania kutoka Kituo cha Mwanza inaendelea vizuri katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa Watoto wa Mitaani yanayoendelea Rio de Janeiro nchini Brazil ambapo katika mchezo wake wa kwanza ilitoka sare ya mabao 2-2 na Burundi.
Juzi (Machi 31 mwaka huu), timu hiyo inayoongozwa na mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutoka Mkoa wa Mwanza, John Kadutu ilicheza mechi mbili. Katika mechi ya kwanza iliifunga Argentina mabao 3-0 na baadaye ikailaza Nicaragua mabao 2-0.
Michuano hiyo ya siku kumi inashirikisha timu kumi. Mbali ya Tanzania, nyingine ni

Argentina, Burundi, India, Kenya, Liberia, Marekani, Mauritius, Misri na Pakistan. Kwa wasichana ni Afrika Kusini, Brazil, El Salvador, Indonesia, Msumbiji, Nicaragua, Philippines, Uingereza na Zimbabwe.

Kipusa cha Kaole Sanaa chatambulishwa kwa wadau

Sehemu ya igizo hilo kama lilivyokuwa likionekana kwenye screen
Wadau wakipata uhondo wa Kipusa
Iizo likiendelea kwenye runinga
Wadau na wasanii walioshiriki igizo hilo wakifuatilia kwa makini
Joti aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda wa kujadili igizo hilo akizuingumza na wadau waliohudhuria onyesho hilo
We kichwa bana na mkikomaa mtafika mbali na kuleta mapinduzi katika tasnia yetu: Ni kama Raia wa TAFF Simon Mwakifamba akimwambia Katibu wa New Kaole Sanaa, Issa Kipemba
Rais wa TAFF, Simon Mwakifanya (kulia) akitoa nasaha zake huku Joti akimsikiliza kwa makini
Simon Mwakifamba Rais wa TAFF akiwa na Mwenyekiti wa New Kaole, Ndimbangwe Misayo 'Thea'.
Mabrekaaaa! Swebe Santana (kulia) Bi Staa na Bi Terry nao walikuwapo na Muongozaji wa filamu hiyo, Christant Mhengga akionekana kwa nyuma yao (shati jeusi)

Yaani ilikuwa ni fursa ya kuwaona wasanii wakali waliosahaulika kitambo
Nyie wenyewe mmeiona ni bab' kubwa---Joti akizungumza leo
Wadau wakiwa makini kufuatilia igizo kwenye runinga
Ilikuwa ni full burudani toka kwa wakali hao waliokumbusha enzi zao kupitia KIPUSA
Watu walikuwa makini kufuatilia
Chifu Husseni Msopa, Sheikh Sadik Godegode na Sheikh Kassim wakiwa makini kufuatilia igizo hilo
Abdallah Mkumbira 'Muhogo Mchungu' Makamu Mwenyekiti wa New Kaole na mmoja walioling'arisha igizo hilo la Kipusa naye alikuwapo kujishuhudia.
Oyaa umeona pale da! Kama wanaambizana Chifu Msopa na Sheikh Godegode
Watu walikuwa makini kupita maelezo
Viongozi wa Kaole, waigizaji wa Kipusa na wageni mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla hiyo
 

Hakuna aliyetaka kupitwa na uhondo
Sehemu ya waliohudhuria wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii walioshiriki igizo la Kipusa
Muongozaji mahiri wa tamthilia na filamu nchini, Christant Mhengga akitoa nasaha zake
Mwenyekiti wa Kaole Sanaa, Ndimbangwe Misayo 'Thea' akizungumza yake kushukuru wadau waliohudhuria
Kusudio letu ni hili....Thea akizungumza
Kama Mwinjilisti! Thea akiendesha dua maalum ya kufungia hafla mbele ya wadau

'Tunakuomba kwa Jina la Bwana Yesu Kristo Ameen" Wadau wakiwa makini wakati dua maalum iliyoendeshwa na Thea
KUNDI la Kaole Sanaa ambalo kwa karibu miaka 10 lilikuwa kimya, leo limeitambulisha kwa wadau wao tamthilia yao mpya iitwayo 'Kipusa' inayowarejesha rasmi katika ulimwengu wa sanaa nchini.

Utambulisho wa tamthilia hiyo inayorejesha kumbukumbu ya enzi za kundi hilo lilipokuwa likitisika anga la sanaa, ulifanyika kwenye ukumbi wa Dar Modern, uliopo Magomeni Mikumi, jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kuwaonjesha kidogo uhondo mzima wa tamthilia hiyo, lakini wadau waliohudhuria waliburudika vya kutosha na kuwasifia wasanii walioanzisha wazo hilo la kurejesha kundi hilo.
Baadhi ya wadau waliopata nafasi ya kutoa maoni yao baada ya kushuhudia sehemu mbili kati ya 25 za tamthilia hiyo walikiri Kaole ni Baba wa Sanaa na kuwataka wasanii hao kutorudi nyuma.
Miongoni mwa waliohudhuria ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifamba, viongozi wa Taasisi ya Amani Tanzania, Sheikh Sadik Godegode na Mwenyekiti wa Baraza la Habari la Kiislam (BAHAKITA), Chifu Hussen Msopa.
Katika nasaha zake ndogo Rais wa TAFF aliwasifia viongozi na wasanii wa Kaole kwa kutoa wazo la kulirejesha kundi hilo na kudai kuwa wao ndiyo wasanii wa ukweli na wanaojua wanachokifanya.
Mwakifamba pia aliwasisitizia kundi hilo kulenga soko la kimataifa ili angalau Tanzania iweze kutamba na kunyakua tuzo kama ambavyo wasanii wa mataifa ya Nigeria, Kenya na nchi nyingine.
Mwenyekiti wa kundi hilo, Ndimbangwe Misayo 'Thea' aliwashukuru waliohudhuria na kuwataka waendelee kuwaunga mkono katika safari yao ambayo ndiyo kwanza wameianza.
Naye Muongozaji na mmoja wa waasisi wa kundi hilo, Christant Mhenga, alisema anachukua maoni, ushauri na hata ukosoaji uliotolewa na baadhi ya wadau kama changamoto za kuboresha kazi yao.
Msanii wa muziki, Vitalis Maembe 'Mzee wa Sumu ya Teja' aliahidi kuwapiga tafu Kaole ili kuendeleza mipango yao ya kurejesha heshima ya sanaa ya maigizo nchini.

Ni Real Madrid au Dortmund kucheka Ulaya, Chelsea waifuata PSG


REAL Madrid leo watakuwa nyumbani kuwakabilia wanafainali wa mwaka jana wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Borussia Dortmund katika mchezo wa roibo fainali ya michuano ya mwaka huu, huku Chelsea watakuwa ugenini kuwakabili PSG katika mchezo miwngine mkali.
Reala Madrid iliyozinduka hivi karfibuni baada ya kubamizwa mechi mbili mfululizo katika ligi ya nchini mwao na kujikuta wakiporomoka toka kileleni mwa msimamo hadi nafasi ya tatu watakuwa na kazi kubwa ya kuwazuia Wajerumani wasiwaletee madhara kwenye uwanja wao wa Santiago Bernabeu.
Hata hivyo kocha mkuu wa timu hiyo, Carlo Ancelotti ametamba kwamba anajivunia kuwa na timu kabambe alizowahi kuzinoa na kuamini kwamba wataifumua  Dortmund leo.
MUitalia huyo alisema kuwa anajivunia kuwa na wachezaji nyota ambao wameifanya timu hiyo kuwa katika nafasi znuri ya kunyakua mataji matatu kwa msimu huu.
“Mbali na mabingwa kama Cristiano Ronaldo, ninao wachezaji wengi wazuri makinda pamoja na wazoefu. Ninataka kuonyesha ukweli kuwa msimu huu si [Gareth] Bale tu aliyetua hapa, lakini pia wachezaji watano kutoka kikosi cha makinda.”
Madrid bado ipo katika nafasi ya kutwaa makombe matatu msimu huu, kwani vijana wa Ancelotti kwa sasa wanashika nafasi ya tatu kwenye La Liga, wakati wakiwa na mchezo wa fainali wa Kombe la Mfalme (Copa del Rey) dhidi ya Barcelona wakiwa pia kwenye kinyang'anyiro cha Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya  Dortmund.
Hata hivyo kocha huyo wa 'Blancos' amesisitiza kuwa lengo kubwa la klabu hiyo msimu huu ni kutwaa ubingwa wa Ulaya kwa mara ya 10.
“Ndoto za Real Madrid kwa sasa ni kutwa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya,” Ancelotti alisema.
Katika mechi nyingine ya robo fainali, wenyeji PSG kupitia kocha wao,  Laurent Blanc wamedai wanaihofia Chelsea kwa uimara wa ukuta wao..
Mabingwa hao wa Ligue 1, wameshinda mechi zote nane za michuano hiyo lakini beki wa kati wa zamani wa Ufaransa, Blanc anajua vema kuwa Chelsea,  chini ya Jose Mourinho, ina uzoefu na safu ya ulinzi imara ya kuweza kukabiliana na wapinzani wowote.
"Tutapaswa kuwa makini zaidi," alisema Blanc. "Tutakuwa na nafasi chache na tutakazozipata itabidi kuzitumia. Tunajua tunapaswa kuwa katika daraja lingine.
PSG ilisonga mbele bila kupoteza katika kundi lililozozijumuisha Anderlecht, Porto na Olympiakos Piraeus kabla ya hatua ya mtoano ya 16 bora kuitupa nje Bayer Leverkusen.
Tegemeo kubwa katika mechi hiyo kwa Blanc litakuwa ni mshambuliaji wake anayeona nyavu zaidi, Zlatan Ibrahimovic ambaye msimu huu wa Ligue 1 ameshatupia mabao 25, yakiwa ni 11 zaidi ya wanaomfuatia, mchezaji mwenza  Edinson Cavani na Alexandre Lacazette wa Olympique Lyon.
Ibrahimovic pia ameshafunga mabao 10 msimu huu kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwa mara ya mwisho Chelsea kucheza Uwanja wa Parc des Princes ilikuwa 2004-05 kwenye hatua ya makundi, ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa Mourinho kuiongoza klabu hiyo ya London katika michuano ya Ulaya ambapo waliichapa PSG 3-0.
Mourinho leo atashusha kikosi chake uwanjani akiwa na kumbukumbu mbaya ya kipigo cha bao 1-0 alichokipata Jumamosi kwenye Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace.