- MFADHILI ALIYEWALETA AWATELEKEZA
- YADAIWA WALIKUJA KUFANYA BIASHARA HARAMU
- BAADA YA MIANYA KUZIBWA - MFANYABIASHARA ALIYEWALETA AWATEMA
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii - mtu ambaye amekuwa akihusishwa na kuileta timu hiyo nchini kwa ajili ya mechi za kujipima nguvu - ni kwamba 3 Pillars waliletwa nchini na mfanyabiashara mmoja mwenye asili ya kiarabu kwa madhumuni ya kufanya biashara haramu na ndio maana timu hiyo ilikuwa haichukui hata shilingi katika mechi mbili za kirafiki ilizocheza hapa nchini na Klabu ya Yanga pamoja na Coastal Union kwa kuwa walikuwa wanapewa kila kitu na mfanyabiashara aliyewaleta nchini.
Lakini kutokana na hali ya ulinzi kuimarika nchini kutokana na mfululizo wa watanzania kukamatwa na wakiwa wamebeba baishara haramu - kazi ambayo 3 Pillars walitumwa kuja kuifanya Tanzania na mfadhili wao ikawa imeingia mdudu, hivyo mfanyabaishara huyo ameitelekeza timu hiyo ya Nigeria katika hoteli ya Itumbi iliyopo Magomeni Mwembechai ambapo mpaka kufikia siku wanarudi kucheza mechi dhidi ya Yanga tayari walikuwa na deni la millioni 12. Mpaka hivi sasa timu hiyo inadaiwa zaidi ya millioni 17 wakiwa hawajui namna ya kulipa deni hilo.
Mtandao huu uliwasiliana na meneja ya hoteli ya Itumbi na alithibitisha ni kweli klabu hiyo ya 3 Pillars inadaiwa deni hilo: "Ni kweli kabisa hawa jamaa tunawadai kiasi cha millioni 17, mpaka kufikia jana walikuwa hawajatupa muelekeo wa namna watakavyolipa deni hili. Mmiliki wa Hoteli jana alikuwa na kikao na viongozi wao wametoa ahadi kwamba wanaongea na ubalozi wao ili kuweza kupata msaada wa kulipa deni hilo waweze kuondoka nchini na kurudi kwao. Kwa sasa imebidi tusiwape huduma ya chakula ili kutokuongeza deni, hivyo haifahamiki wanakula au vipi," alisema meneja wa hoteli hiyo.
Wakati huo huo imefahamika kwamba ulifanyika mchezo mchafu katika kuzuia 3 Pillars isicheze michezo ya kujipima nguvu Tanzania na baadhi ya viongozi wa TFF kwa maslahi yao binafsi - yanayohusiana na uchaguzi mkuu wa TFF -
...........................itaendelea
SHAFII DAUDA