STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 15, 2013

CHADEMA KUFUTWA? TENDWA ALIPUKA




Msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa.
MSAJILI wa Vyama vya Siasa Tanzania, John Tendwa ameibuka na kusema sasa anaandaa kalamu yake kukifuta Chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA.
Katika Taarifa yake kwa vyombo vya habari muda mfupi uliopita Tendwa amesema CHADEMA wanataka kuanzisha kikundi cha mgambo ambacho ni kinyume na sheria, katiba ya nchi na sheria za usajili wa vyama.
Msajili huyo amesema kwamba kama madai ya CHADEMA ni kuanzisha kikundi cha kujilinda dhidi ya Green Guard wa CCM madai hayo hayana msingi wowote kwani kama CHADEMA wana taarifa kwamba Green Guard wanahatarisha amani basi wanapaswa kuripoti suala hilo polisi ili lifanyiwe kazi kwa mujibu wa sheria.
Tendwa amezidi kuonya kwamba uamuzi wake ni wa mwisho na atakapoifuta CHADEMA maamuzi yake hayapingwi popote kisheria.
Source: JF

Manchester United sasa yamgeukia Fabregas

Cesc Fabregas
 BAADA ya kumkosa kiungo Thiago Alcantara aliyetimkia kwa Mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich, klabu ya Manchester United imeelekeza shabaha yake kwa kiungo wa zamani wa Arsenal anayeichezea Barcelona, Cesc Fabregas.
Mashetani Wekundu hao, wameamua kuweka mezani kitita cha pauni 26 ili kumnasa nyota huyo wa Hispania ili atue Old Trafford.
United imepania kumnasa mkali huyo ikichuana na Arsenal ambao pia wameonyesha nia ya kumrejesha kiungo huyo Emirates baada ya kumuuza miaka miwili iliyopita kwa dau la pauni milioni 31.
Ofa iliyotangazwa na United kwa Fabregas ni pungufu ya kiasi cha Pauni Milioni 5 kufika dau la Pauni Mil 30.75 inayoendelea kushikilia rekodi ya mchezaji wa bei ghali kusajiliwa OT ilipomnunua mshambuliaji wa Tottenham, Dimitar Berbatov mwaka 2008. 
Duru za soka zimekuwa zikisema kuwa kuna uwwezekano mkubwa kwa Cesc kurejea Arsenal licha yha kwamba mwenyewe alishanukuliwa kwamba angependa kuendelea kuichezea Barcelona kwa vile anafurahia kuwepo hapo ili kupigania nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu.
Kama atatua kwa United, kutamfanya nahodha huyo wa zamani wa Arsenal kuungana tena na mchezaji wenzake wa zamani wa Emirates Robin van Persie ambaye alihama klabu hiyo na Arsena msimu uliopita na kufanikiwa kutwaa nao taji la ubingwa wa EPL.

Rais Kikwete ateta na uongozi wa Benki ya TIB

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Maendeleo ya TIB, Bw Peter Noni, Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 13, 2013. Bw. Noni na ujumbe wake walifika Ikulu kumwelezea Rais Kikwete mipango na mikakati kabambe ya kuijenga upya benki hiyo iliyokuwa ikijulikana kama Tanzania Investment Bank (Benki ya Rasilimali Tanzania) ikiwa ni pamoja na miundo mbinu na upanuzi wa wigo wa biashara. PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Maendeleo ya TIB, Bw Peter Noni, Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 13, 2013. Bw. Noni na ujumbe wake walifika Ikulu kumwelezea Rais Kikwete mipango na mikakati kabambe ya kuijenga upya benki hiyo iliyokuwa ikijulikana kama Tanzania Investment Bank (Benki ya Rasilimali Tanzania) ikiwa ni pamoja na miundo mbinu na upanuzi wa wigo wa biashara.

'Mesut Ozil aondoki Santiago Bernabeu'

Mesut Ozil

BABA wa kiungo wa Real Madrid, Mesut Ozil, amesema mwanae hana mpango wa kuondoka Santiago Bernabeu.
Ozil amekuwa akitajwa kutaka kwenda kucheza Ligi Kuu ya England, lakini baba wa mchezaji huyo,  Mustafa amefichua kuwa mwanae hana mpoango huo badala yake anahitaji mkataba mpya wa kuendelea kuitumia timu yake.
Ozil mkubwa alisema mwanae mwenye umri wa miaka 24 ndiyo kwanza amefungua meza ya mazungumzo ya kusalia klabu hapo tofauti na hisia kwamba angependa kumtikia Engaland.
Ozil, nyota wa Kijerumani anatajwa thamani yake ni Pauni Mili 30 na alikuwa akiwindwa na klabu kubwa za Engand, lakini baba yake alisisitiza kuwa; "Mesut anafuraha kubwa ndani ya Madrid," alisema Mustafa na kuongeza imani yao dili mpya kati ya mwanae na klabu yake itambakisha mkali huyo mpaka 2019.

Arsenal bado yamng'ang'ania Suarez sasa yaongeza dau la kumng'oa Liverpool

Luis Suarez

KLABU ya Arsenal bado haijakata tamaa na nia yake ya kumng'oa mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay, Luis Suarez kutoka Liverpool kwa kudaiwa ipo tayari kuongeza dau hadi kufikia pauni Mil. 35 mradi iimnyakue mkali huyo wa mabao.
Suarez amekuwa chaguo la kwanza la kocha Arsene Wenger katika usajili wa majira ya joto na iko tayari kutoa dau zaidi ya ile ya awali ya pauni Mil.30 iliyokataliwa na Liverpool wanaotaka angalau pauni Mil 40.
Klabu hiyo ya London ya Kaskazini inachuana na Manchester City na Real Madrid zinazomfukizia pia 'mtukutu' ambaye amekuwa na wakati mgumu nchini England kutokana na kuandamwa na vyombo vya habari hasa kwa kadhia zake tata za hivi karibuni katika EPL.
Wenger amekuwa akimhitaji mshambuliaji huyo huku pia akimwinda Higuian Gonzalo ambaye bado haijafahamika kama itakuwa naye katika msimu ujao baada ya kuelezwa amejiunga na timu yake ya Real Madrid kuanza mazoezi.
Hata hivyo kuna kila dalili Arsenal kumnasa mshambuliaji huyo wa Argentina na iwapo itafanikiwa kuishawishi Liverpool kumuachia Suarez itakuwa imelamba dume baada ya kuwa misimu karibu nane isiyo na tija yoyote England na kimataifa.

TBL yakabidhi Simba fedha za mkutano wao



KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake maridadi ya Kilimanjaro Premium Lager, leo imekabidhi hundi ya Sh. Milioni 20 kwa klabu ya Simba kwa ajili ya mkutano mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika Julai 20, 2013 jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi hundi hiyo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema: “Tunakabidhi fedha hizi ikiwa ni mwendelezo kutekeleza majukumu yetu kama mdhamini mkuu wa Simba SC. Kwa kuzingatia hilo tungependa kuona maendeleo ya klabu ya Simba uwanjani na nje ya uwanja,”.
“Tunaiunga mkono klabu hii katika mkutano wake mkuu tukiamini kuwa mkutano huu utaimarisha uhusiano uliopo kati ya klabu na wanachama wake kwa kuwapa fursa ya kuhakiki mwelekeo wa klabu yao waipendayo,”alisema.
“Ikiwa na mamilioni ya mashabiki nchini, klabu hii imejengeka kutokana na rekodi nzuri ya mafanikio kwa muda mrefu – na Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kuwa sehemu ya klabu hii,”.
“Tunaamini kwamba mbali na wanachama, wapenzi na mashabiki wa Simba kuona timu yao ikishinda lakini pia tunatambua kwamba ni haki yao ya msingi kuwasiliana na klabu na kupata taarifa mbalimbali za mwenendo wa klabu,”.
“Kutokana na sababu hizi, sisi kama wadhamini wakuu wa klabu hii tunatoa mchango wa shilingi milioni ishirini ili kuunga mkono jitihada za klabu kuendelea kuwajibika kwa wanachama wake,”.
“Tunatambua wajibu wetu kama wadhamini wakuu wa Simba katika kutekeleza mkataba wetu, tutaendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha tunalipeleka soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio huku tukiwaburudisha na bia yenu muipendayo Kilimanjaro Premium Lager – Bonge la Kiburudisho”.

Rais JK awalilia wanajeshi waliokufa Darfur


Amir Jeshi Mkuu wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete
  Rais Jakaya Kikwete, ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ameeleza kushtushwa na kuhuzunishwa na mauaji ya wanajeshi saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliokuwa wanalinda amani Darfur, Sudan baada ya kushambuliwa na waasi wa Sudan.
Katika shambulizi hilo ambalo pia wanajeshi wengine 14 walijeruhiwa, pia ametuma salamu za rambirambi kwa JWTZ na kwa familia za wafiwa wote.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana ilisema kuwa Rais Kikwete anaungana na Watanzania wote na hasa maofisa na wapiganaji wa JWTZ na familia za wafiwa kuomboleza vifo vya askari hao na anawaombea walioumia katika tukio hilo wapone haraka na kuendelea na majukumu yao ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.
Katika salamu zake za rambirambi kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange na familia za wafiwa, Rais Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu amesema:
“Sina maneno ya kutosha ya kuelezea mshtuko, huzuni na masikitiko yangu makubwa kufuatia vifo vya vijana wetu hao ambao wamepoteza maisha yao katika shughuli muhimu sana ya utekelezaji wa majukumu ya Umoja wa Mataifa ya kulinda na kuleta amani katika eneo la dunia ambako maelfu kwa maelfu ya watu wamepoteza maisha yao kwa kushambuliwa na waasi.”

“Napenda kwa niaba ya Watanzania wenzangu niwahakikishieni kwamba hakuna shaka kuwa vijana wetu hao tokea walipokwenda  Darfur Februari mwaka huu, na kwa hakika tokea Tanzania ilipoanza kuchangia walinzi katika eneo hilo mwaka 2007, wamefanya kazi nzuri sana, kazi iliyoongozwa na weledi wa hali ya juu na kazi ambayo imeiletea nchi yetu heshima kubwa.
Tutaendelea kuwaenzi kwa kujivunia kazi yao,” amesisitiza katika salamu hizo. Kupitia kwa Jenerali Mwamunyange, ametuma salamu za rambirambi kwa maofisa wakuu na maofisa wadogo pamoja na wapigaji wote wa JWTZ kwa kupotelewa na wenzao.
“Aidha, kupitia kwako, nawatumia salamu zangu kwa wanafamilia za waliopotelewa na wapenzi wao na ndugu zao katika tukio hilo.
Wajulishe kuwa naungana nao katika kuomboleza. Wajue kuwa uchungu wao ni uchungu wangu pia na wa Watanzania wote na kuwa kwa pamoja tunamwomba Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.
Vile vile kwa pamoja tunamwomba Mwenyezi Mungu azilaze peponi roho za marehemu,” alisema.
Wanajeshi waliouawa na kujeruhiwa walikuwa sehemu ya askari 37 na ofisa mmoja ambao walikuwa wanasindikiza msafara wa waangalizi wa kijeshi huko Darfur kutoka eneo la Khorabeche kwenda Nyara waliposhambuliwa na waasi kiasi cha kilomita 20 kutoka Khorabeche saa tatu asubuhi Jumamosi iliyopita.
JWTZ YAPELEKA KIKOSI KUCHUNGUZA
Wakati guo huo, JWTZ  limetuma kikosi maalum kwenda  nchini Sudan  kufanya uchunguzi kuhusu mazingira ya kuuawa kwa wanajeshi saba wa Tanzania huko  Darfur.

Vile vile, Jeshi hilo limesema linaendelea kufanya mawasiliano na Umoja wa Mataifa (UN),  kuangalia namna ya kuongeza uwezo wa kujilinda na mashambulizi pindi kikosi cha Tanzania cha kulinda amani kinapokabiliana na mashambulizi ya aina hiyo.

Akitoa taarifa ya awali kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaama, Msemaji wa Jeshi hilo ambaye ni Mkurugenzi  wa Habari na Uhusiano,  Kanali Kapambala Mgawe, alisema tukio hilo lilitokea juzi asubuhi baada ya kikundi cha askari 36 kutoka Tanzania akiwamo ofisa wao mmoja kushambuliwa na kikundi cha waasi wa Sudan.

Mgawe alisema  msafara huo uliojumuisha maafisa na askari kutoka mataifa mengine ambao pia walijeruhiwa,  ulishambuliwa  umbali wa kilomita  20 kutoka  Makao Makuu ya Kikosi hicho.

Mgawe alisema tukio hilo lilitokea katika eneo la sheria ya ulinzi wa amani (chapter 6) ambayo hairuhusu mashambulizi ya silaha.

“Kwa kuwa mazingira ya sasa  Darfur hayapo katika sheria inayoruhusu mashambulizi, hivyo tunaendelea kuwasiliana na UN  na kuwaomba kubadili sheria hiyo ili kuruhusu kutumika ile ya chapter 7 kwa ajili ya kukiwezesha kikundi chetu kujilinda pindi kinapokabiliwa na  mashambulizi ya aina hiyo,” alisema Mgawe

Kadhalika,  Mgawe alisema mpaka sasa taratibu zilizokwishafanyika ni kuhamisha miili ya marehemu kutoka eneo la tukio na kupelekwa Nyara ambako kuna  Hospitali kuu ya eneo la Operesheni kwa ajili ya kuhifadhiwa na majeruhi kupatiwa matibabu.

Pia alisema wanawasiliana na familia za marehemu hao,  na kwamba utaratibu huo ukikamilika majina ya askari hao yatatangazwa.

“Wanajeshi wetu wamepatwa na mkasa huo wakiwa katika utekelezaji wa jukumu lao la Umoja wa Mataifa la kulinda amani nchini Sudan eneo la Darfur,  kwa utaratibu wa Kijeshi hatuwezi kutangaza majina yao mpaka tuwasiliane na familia zao kwanza,” alisema.

Mgawe alisema taarifa hiyo ni ya awali na kwamba taarifa zaidi juu ya tukio hilo  zitaendelea kutolewa.

Hii ni mara ya pili kwa wanajeshi wa Tanzania kuuawa katika Jimbo la Darfur, ambapo Agosti mwaka jana , Kanali Mgawe alinukuliwa na vyombo vya habari akithibitisha kutokea kwa vifo vya askari watatu ambao gari lao lilizolewa na maji walipokuwa wa kivuka mto uliokuwa umefurika maji, huku wakiwa katika utekelezaji wa jukumu lao la Umoja wa Mataifa la kulinda Amani nchini humo.

CHANZO: NIPASHE

Mugabe atoa mpya, ataka mashoga, wasagaji wapeane mimba la sivyo...!

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe
 RAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe ametoa kali ya mwaka kwa kuwachimba mkwara Mashoga na Wasagaji kwamba wasipotiana mimba ni lazima atawafunga jela.
Mubabe ametoa kali hiyo Ijumaa  wakati akizindua kampeni za chama chake cha kwa ajili ya uchaguzi utakaofanyika mwezi.
Isome taarifa nzima ya rais huyo mwenye umri mkubwa aliye madarakani duniani na ambaye wazungu wanambloo kwa misimamo yake isiyoyumba.
 President Robert Mugabe on Friday threatened to jail gay and lesbian couples who fail to conceive any offspring as he launched his party’s campaign for this month’s general election.

The Zanu PF leader also attacked bitter rival and coalition partner Morgan Tsvangirai for his bed-hopping habits saying it was inconceivable that such a character could want to lead the country.

Mugabe, a rabid critic of homosexuality returned to the theme as he addressed thousands of supporters in Harare’s Highfield township.

He said he was shocked to learn that US President Barack Obama had called on African countries to embrace the practice.

The Zanu PF leader said in Shona: “Ndakanzva Obama achiti ah, dai muno muAfrica mabvuma kuti murume nemurume vachate, mukadzi nemukadzi vachate, ndikati nhai nhai, taitoti baba vako zvaari mutema, iwe uneruva neruzivo netsika dzevatema waakunotora zvevarungu futi!

Apparently joking Mugabe added: “So how would they (gay couples) have children?

“I should like to shut them-up in some room and see if they get pregnant; if they don’t then its jail because they have claimed they can have children. So, to that kind of rot, we say no, no, no, no!”

Continuously breaking into laughter as he warmed up to his gay bashing, Mugabe further criticised the Anglican Church for blessing homosexual marriages which he said was taboo among Africans.

He dared lesbians who assume the role of the husband in their relationships to prove that they were indeed ‘men’.

“Women are also engaged in this vile activity. We have some claiming to be men but what is it that makes you a man?

“Show us your manhood; you want to make other women your wives and you the husband? Well, that is madness; we refuse to accept that,” he said.

Polisi Tanga wanasa kete za dawa za kulevya

Baadhi ya dawa za kulevya vinazonaswa nchini
WIMBI la biashara ya dawa za kulevya linazidi kushika kasi baada ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limefanikiwa kukamata kete 46 za dawa za kulevya aina ya Cocaine baada ya kufanya msako kwenye maeneo yanayosadikiwa wanakaa watumiaji wa dawa hizo wilayani Pangani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constatine Massawe, alisema jana kuwa dawa hizo zilikamatwa Jumatano iliyopita baada ya polisi kuvamia eneo hilo na kuwakamata watumiaji wanne.
Alisema polisi walifanikiwa kukamata dawa hizo kutokana na taarifa walizopata kutoka kwa raia wema.
Aliwataja waliokamatwa katika tukio hilo ambao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kuwa ni Shaban Ramadhan (20), mvuvi na mkazi wa Malindi wilayani Pangani, Mohamed Kijiba, mkazi wa Fungoni na Iddi Hamdan (21), mkazi wa Fungoni mjini Pangani ambao wote ni wavuvi.
Kwa siku za karibu janga la dawa za kulevya limezidi kushika kasi na kuonyesha wazi 'vita' dhidi ya dawa hizo ni kama hazizai matunda kutokana na kila uchao kunaswa 'unga' ambao huingizwa nchini toka ng'ambo.

Mbishi Real ataka watanzania kuutakaa udini

Mbishi Real katika pozi
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Fred Kaguo 'Mbishi Real' ameibuka na kampeni mpya ya kuwahamasisha watanzania kuepuka vitendo vya kibaguzi vya udini na ukabila iitwayo 'Tanzania Tuukatae Udini'.
Akizungumza na MICHARAZO, Mbishi anayetamba na nyimbo kadhaa ikiwamo 'Tozi wa Mbagala' alisema kampeni hiyo ni maalum kwa kutaka kuwakumbusha Watanzania kuwa wote ni wa moja na hakuna aliye bora zaidi ya wengine.
"Hakuna asiyejua hali inayoendelea nchini kwa sasa japo ni kwa chinichini, hivyo kama msanii nimeona nitumia kipaji changu kuwahamasisha watanzania wenzangu kuukata udini ili kutovunja umoja wetu tuliokuwa nao kwa muda mrefu," alisema.
Mbishi alisema kampeni hiyop ambayo kwa sasa inatafutiwa wadhamini ili kuanza rasmi baada ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani utafanyika nchini nzima kwa kushirikisha maonyesho mbalimbali ya sanaa ikiwamo nyimbo toka wa wasanii na makundi tofauti.
"Ni kampeni niliyopanga kuifanya nchi nzima kuwahamasisha wenzangu na itaambatana na burudani mbalimbali, kwa sasa najiandaa kupeleka maombi serikalini na kwa wafadhili ili kufanikisha vyema kilichjokusudiwa kwenye kampeni hiyo," alisema Mbishi.
Mbishi alisema matrukio machache yaliyotokea katika baadhi ya maeneo ya nchi yenye kuhusiana na masuala ya kidini kama yale ya kugombea kuchinja na milipuko ya mabomu kanisani na kukojolewa na kuchanwa kwa Qur'an ni dalili mbaya kwa Tanzania yenye amani.


CHADEMA noma yaigaragaza CCM udiwani Arusha



 Polisi wakimsihi Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari  aondoke nje ya kituo cha kupigia kura cha Ofisi ya kata ya Kimandolu, pamoja na makada wa CCM hawako pichani ambapo walitakiwa kukaa mita 200 badala ya mita 100. Katika uchaguzi huo Chadema imeshinda katika kata zote nne. (Picha zote na Ferdinand Shayo)
 Polisi wakimsihi Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari  aondoke nje ya kituo cha kupigia kura cha Ofisi ya kata ya Kimandolu, pamoja na makada wa CCM hawako pichani ambapo walitakiwa kukaa mita 200 badala ya mita 100.
 Makarani wa uchaguzi wakiingiza masanduku ya kura katika ofisi ya kata ya Kimandolu kutoka  kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi kimandolu. 
Makarani wa uchaguzi wakiingiza masanduku ya kura katika ofisi ya kata ya Kimandolu kutoka  kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi kimandolu. 
 Polisi wakiimarisha ulinzi katika lango kuu la kuingilia  kituo cha kupigia kura cha Ofisi ya kata ya Kimandolu katika uchaguzi ulifanyika leo mjini Arusha. 
 Mkazi wa kata ya kimandolu akichomvya wino mara baada ya kukamilisha zoezi  la kumchagua diwani wa kata hiyo liliofanyika Julai 14 katika kituo cha kupigia kura cha ofisi ya kata.
 Mkazi wa Kata ya Kimandolu akitumbukiza kura yake wakati wa uchaguzi wa madiwani uliofanyika mjini Arusha.
 Mkazi wa kimandolu,Juliana Mosha akitumbukiza kura yake katika sanduku la kura katika uchaguzi wa madiwani uliofanyika jana kuziba nafasi  ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo,zoezi hili lilifanyika katika kituo cha kupigia kura cha ofisi ya kata
 Dina Naftal Mkazi wa kata ya kimandolu akitumbukiza kura yake katika sanduku la kura katika uchaguzi wa madiwani kuziba nafasi  ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo, zoezi hili lilifanyika katika kituo cha kupigia kura cha ofisi ya kata.
 Wakala wa chama cha siasa akihakiki kitambulisho cha mpiga kura kabla ya kuruhusiwa kupiga kura ya kumchagua diwani wa kata hiyo ya Kimandolu, zoezi hili lilifanyika katika kituo cha kupigia kura cha ofisi ya kata
 Wakazi wa kimandolu wakifuatilia majina yao kwa makini ili kufahamu vyumba husika vya kupigia kura.
 Wakazi wa kimandolu wakifuatilia majina yao kwa makini ili kufahamu vyumba husika vya kupigia kura.
Wakazi wa kimandolu wakifuatilia majina yao kwa makini.
 Wakazi wa kimandolu wakifuatilia majina yao.
Polisi akiwasogeza wananchi waliokuwa karibu na kituo cha kupigia kura cha Shule ya msingi Kimandolu ambapo walitakiwa kukaa umbali wa mita 200 na sio mia 100 kama ilivyozoeleka.

Benki ya CRDB yafuturisha wateja Znz


Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB ya Benki, TullyEsther Mwambapa akizungumza katika hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake.
 Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum Zanzibar Machano Othman Said akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha wateja wa benki ya CRDB iliyofanyika mjini Zanzibar.
 Wadau mbalimbali wakipata futari.
 Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakijumuika pamoja.
Baadhi ya wateja wa benki ya CRDB katika hafla ya kufuturisha.
Baadhi ya wateja wa benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum Zanzibar Machano Othman Said akizungumza katika hafla hiyo.
Meneja wa benki ya CRDB tawi la zanzibar, Nassor Uzigo akipata Chai.
 Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakishiriki katika hafla ya kufuturisha iliyofanyika mjini Zanzibar.
 Wafanyakazi wa benki ya CRDB pamoja na wateja wakipata futari.
 Baadhi ya wateja wa benki ya CRDBwakipata futari.
Wadau wakipata futari.
 Meneja Mahusiano wa Benki  ya CRDB, Godwin Semunyu akigawa futari kwa wateja wa benki hiyo katika hafla ya kufuturisha iliyofanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort
Wateja wa benki ya CRDB wakipata futari.
 Wadau mbalimbali wakipata futari.
 Meneja wa benki ya CRDB tawi la Zanzibar, Nassor Uzigo lililopo eneo la Mkunazini mjni Zanzibar akipata chai wakati wa hafla ya kufuturisha  iliyoa andaliwa na ben
Sheikh akiomba duah.
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum Zanzibar Machano Othman Said akishiriki katika uomba dua wakati wa hafla hiyo.
Picha ya pamoja.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB pamoja na wadau wa benki hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwaza wa Rais Fatma Abdull Habib Fereji (wa tatu kulia) 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwaza wa Rais Fatma Abdull Habib Fereji (kulia) akizungumza mara baada ya hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki ya CRDB mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB ya Benki, TullyEsther Mwambapa (wa pili kushoto) akimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwaza wa Rais Fatma Abdull Habib Fereji wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki ya CRDB kwa ajili ya wateja wake.