STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 4, 2013

CATHERINE FOUNDATION YATOA MKONO WA IDD KWA YATIMA ARUSHA

 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha na Mkurugenzi wa Taasisi ya Catherine Foundation, Catherine Magige akikabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa watoto yatima wa kituo cha Help for the Maasai kilichopo kwa Mrefu mkoani Arusha ikiwa ni sehemu ya zawadi za Mkono wa Idd El Fitiri kwa yatima na wasio jiweza.
 Catherine (kulia) akizungumza na baadhi ya viongozi na wasimamizi pamoja na watoto wa kituo cha Help for the Maasai kilichopo kwa Mrefu mkoani Arusha
 Watoto wa kituo cha Help for the Maasai kilichopo kwa Mrefu mkoani Arusha walipata zawadi mbalimbali kwaajili ya siku Kuu ya Iddi.
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Arusha na Mkurugenzi wa Taasisi ya Catherine Foundation, Catherine Magige akiwa katika picha na watoto mara baada ya kutoa msaada wa vyakula na vitu vingine mbalimbali kituo cha Help for the Maasai kilichopo kwa Mrefu mkoani Arusha leo.
Catherine Magige akiwa na Mwandishi wa Channel 10 mjini Arusha, Jamilah Omar.

Azam watua salama Sauzi kuivaa Kaizer Chiefs kesho

Wachezaji wa Azam wakijiandaa kuanza mazoezi nchini Afrika Kusini

KLABU ya soka ya Azam imetua salama nchini Afrika Kusini na imeanza kujifua kwa mazoezi ya kambi yao na panapo majaliwa kesho itashuka dimbani kuvaana na Mabingwa wa nchini humo, Kaizer Chiefs katika pambano lao la kwanza kati ya manne itakayocheza huko.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa klabu hiyo, Jafar Idd alisema kuwa timu hiyo imefika salama na kwamba vijana wao walishaanza mazoezi kwa ajili ya mechi ya kesho itakayochezwa jioni.
Jafar alisema baada ya mechi ya kesho timu yao itapumzika siku moja kabla ya kurudi tena dimbani kuvaana na Orlando Pirates kisha kukwaruzana na Mamelodi Sundowns na kumalizia ziara yao Agosti 12 dhidi ya Moroka Swallows.
Mechi yao ya kesho itachezwa kituo cha mazoezi cha kaizer kitwacho Machorena na Meneja wa timu hiyo ya Azam, Jemedari Said amenukuliwa akisema kuwa kambi yao ipo katika hadhi ya hali ya juu kuwawezesha kujiweka vyema kwa michuano iliyopo mbele yao ikiwamo Ligi Kuu na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika itakayoshiriki kwa marea ya pili mfululizo mwakani.

Watanzania wahimizwa kuwasaidia yatima kila mara badala ya sikukuu tu

Mlezi wa timu ya Golden Bush, Onesmo Waziri 'Ticotico' akizungumza baada ya kukabidhi msaada katikia kituo cha kulelea yatima cha New Life Orphans Home mapema leo (Agosti4) Wengine picha mezani toka kushoto ni Katibu wa Golden Bush, Herri Morris, Katibu wa kituo hicho, Hamad Kombo na Abuu Ntiro ambaye ni miongoni mwa viongozi wa timu hiyo.

Baadhi ya misaada iliyotolea na Golden Bush (mwenye shati la mistari) ni nyota wa zamani wa Yanga na Reli, Yahya Issa

Katibu wa Golden Bush, Herri Morris akizungumza huku viongozi wenzake 'Ticotico na Abuu Ntiro wakiwa makini.

Juma Kaseja akiwa katika picha ya yatima wa kituo cha New Life Orphans Home. Kipa huyo alikuwa kivutio kwa watoto hao ambapo hakuhitaji kujitambulisha kwani watoto walisema wanamjua kuwa ni JK wa Taifa Stars
Ticotico (mwenye miwani) pamoja na wachezaji wa Golden Bush wakiwa katika picha ya pamoja na yatima wa kituo cha New Life Orphans Home cha Kigogo walipoenda kuwapa msaada wenye thamni ya Sh Laki 3.5.
WATANZANIA wamehimizwa kuwasaidia yatima kila mara wapatapo nafasi badala ya kusubiri kufanya hivyo kipindi cha sikukuu kwa kugawa misaada kwa kile kinachoelezwa watoto hao hawahitaji katika kipindi hicho tu bali kila siku kutokana na kukosa wazazi na walezi wa kuwalea kama watoto wengine.
Wito huo umetolewa na Mlezi wa klabu ya Golden Bush, Onesmo Waziri 'Ticotico' wakati walipokitembelea na kutoa msaada katika kituo cha kulelea yatima cha New Life Orphans Home, kilichopo Kigogo Dar es Salaam.
Ticotico alisema yatima ni wahitaji wa kila siku hivyo ni vyema jamii ikawa na utamaduni wa kujitolea kuwasaidia kila mara badala ya kusubiri vipindi vya sikukuu kana kwamba wakati huo pekee ndipo watoto hao hula na kunywa au kuhitajia misaada zaidi.
"Huu umekuwa kama utamaduni kila wakati wa sikukuu kama za Pasaka, Krismasi au Idd ndipo utaona watu wakipigana vikumbo kuwasaidia yatima, huu sio utamaduni mzuri, watoto hawa wanahitaji misaada kila siku hivyo jamii iwe inawatupia macho kuwafanya wajihisi vyema na kufarijika," alisema.
Alisema ingawa hiyo ni mara yao ya kwanza kukitembelea kituo hicho, lakini klabu yao ya Golden Bush imekuwa na kawaida ya kufanya hivyo kwa vituo vingine na wakati kwa siri kwa kutambua jukumu la kuwasaidia yatima ni la kila mtu na yeye kama mwanajamii anawajibika kufanya hivyo kwa siri na dhahiri.
Ticotico alisema anaamini kuwasaidia watoto hao kunawafanya wasijisikie vyema na kujiona kama watoto wengine na kuahidi kuwa bega kwa bega na kituo hicho baada ya kuelezwa matatizo yao ikiwemo kutaka kumalizia jengo lao lililopo Boko-DAWASA.
Naye Katibu wa kituo hicho alishukuru msaada huo uliopelekwa kituoni hapo na wachezaji wa timu hiyo wengi wao wakiwa ni mastaa wa kandanda nchini kama akina Juma Kaseja, Salum Swedi, Abuu Ntiro, Salum Athuman 'Majani', Herry Morris, Aman Simba, Kudra Omar, Wazir Mahadhi na wengine.

Cheki ajali ya lori la mafuta lililoanguka jana Mbalizi-Mbeya na watu walivyokuwa wakijizolea mafuta bila kuhofia kitu

 Lori lenye namba za usajili  T97 AJL lenye tela namba T746 BKF lilipo acha njia na kupinduka na kuziba njia

Lori  likishindwa kupita baada ya Mafuta kumwagika Barabarani na kusababisha barabara kushindwa kupitika
Magari yakipita kwa shida baada ya Lori kudondoka
Askari wakijitahidi kukabiliana na watu waliokuwa wanachota mafuta
Shughuli za uokoaji zikiendelea kulia ni Dereva wa Lori hilo baada ya kunusurika
Dereva wa gari hilo Hassan Abdi (35) akiwa haamini kilicho tokea baada ya Kunusurika kifo


YALE YALE!!! Wananchi  wenye ndooo Haya.... Wenye Madumu haya .... wenye Masefuria haya... wote walikuwepo kuchota Mafuta kama inavyo onekana ... bila kujali kama yaweza kulipuka 
Wananchi Mbalimbali wakiwa wanapata shida kupita baada ya Lori kudondoka

Askari wa zima moto wakiwa wanaendelea na Juhudi za kuondoa mafuta barabarani kwa maji 
Wananchi mbalimbali wakiwa wanaondoka na Mafuta... huku wengine wakiendelea kuchota
Wakina mama... Watoto... Vijana na wazee wakiwa wanapata shida jinsi ya kupita baada ya ajali

Kushoto ni Tingo Saimoni Msovela (23) na dereva wake Hassan Abdi wakijitahidi kuziba mafuta yasiendelee kuvuja
 
veta
Tingo wa Lori hilo la mafuta baada ya kuokolewa kutoka kwenye Gari.


Ezekiel Kamanga
WATU wawili wamenusurika kifo baada ya lori la mafuta lenye namba za usajili T 978 AJL lenye tela namba T 746 BKE Aina ya SCANIA walilokuwa wakisafiria kutoka DAR ES SALAAM kwenda ZAMBIA kuacha njia na kupinduka katika mteremko wa MBALIZI barabara MBEYA TUNDUMA.
Dereva ametambuliwa kwa jina la HASSAN ABDI 35 na msaidizi wake SAIMON SOVELA 23 ambao walikuwa wametokea DAR ES SALAAM kuelekea ZAMBIA likiwa limejaa shehena ya mafuta
Kwa mujibu wa Dereva amesema kuwa gari hilo ghafla lilipoanza kuteremka mteremko liliharibika mfumo wa breki na mbele yake kukiwa na magari matano baada ya kuona kuwa angesababisha maafa makubwa aliamua kulichepusha pembeni ndipo lilipoacha njia na kupinduka na kumwaga shehena ya mafuta.
Kikosi cha zimamoto kilifika eneo la tukio na kuhakikisha usalama wa eneo hilo kuhofia mlipuko wa moto ambao ungeweza kutokea kutokana na baadhi ya wananchi kuanza kuchota mafuta yaliyokuwa yanatiririka.
Pamoja na juhudi za Jeshi la Polisi kudhibiti wananchi kutochota mafuta lakini wananchi walikaidi na kuendelea kuchota mafuta.
Ajali hiyo ilisababisha adha kubwa kwa wasafiri waliokuwa wana pita barabara hiyo wakiwemo wagonjwa na waliokuwa wanawahi usafiri wa ndege majira ya saa saba mchana.

WABUNGE WACHAPANA NGUMI ZA KAVU KAVU BUNGENI


Uuuh aaaah!
PICHANI ni baadhi ya  wabunge wa Taiwan 'walivyokuwa wakiadabishana' jana baada ya kupishana lugha kufuatia mpango wa kupiga kura ya maoni iliyoazimia kuidhinisha umaliziwaji wa mradi wa nne wa Nyuklia katika kisiwa ambacho kinakaliwa na watu wapatao milioni 23. Wabunge wa Tanzania ambao wamekuwa wakichimbana mkwara bungeni...wakifikia huku sijui itakuwaje? 
Acha mshikaji mnaharibu! Ngoja nimfunze adabu
Kuja hapa weweee!

Bahanuzi, Javu waizamisha Mtibwa Sugar Taifa

 Beki wa Mtibwa Sugar, Salvatory Ntebe akichuana na mshambuliaji wa Yanga wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga imeshinda 3-1. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
 Beki wa Mtibwa Sugar, Ally Lundega akimiliki mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
 Mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Hassan Ramadhan wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 


 Kikosi cha Mtgibwa Sugar.
Kikosi cha Yanga.
 Mashabiki wa Yanga waklifuatilia mtanange huo.

Young Africans leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wakata miwa kutoka Morogoro timu ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu uliofanyika katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Ikiwatumia wachezaji wake wapya iliyowasajili kwa ajili ya msimu huu kikosi cha mholanzi kiliingia uwanjani kwa lengo la kuhakikisha wanapata ushindi na kuendeleza heshima kwa timu wanazokutana nazo.
Dakika ya sita ya mchezo mshambuliaji mpya Shaban Kondo almanusura aipatie Young Africans bao baada ya kupokea krosi safi ya Said Bahanuzi kutoka upande wa kulia lakini kutokua makini kwa mshambuliaji huyo kulimfanya mlinda mlango wa Mtibwa Sugar Hussein Sharrif kuokoa hatari hiyo.
Said Bahanuzi aliwainua washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Yanga dakika ya 24 ya mchezo baada ya kuukwamisha mpira wavuni kufuatia mlinzi wa mtibwa kuokoa kwa kichwa mpira wa Jerson Tegete ulikokuwa ukielekea wavuni.
Mara baada ya bao hilo Mtibwa Sugar waliongeza kasi ya mashambulizi kwa lango la Yanga ili waweze kupata bao la kusawazisha laikini harakatia zao zilishia mikononi mwa mlinda mlango Deogratius Munishi 'Dida' 
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 1 - 0 Mtibwa Sugar.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ambapo Yanga iliwaingiza golikipa Ally Mustapha 'Barthez, Rajab Zahir, David Luhende, Bakari Masoud, Hussein Javu, na Abdallah Mguhi 'Messi, mabadiliko ambayo yaliongeza kasi ya mchezo.
Dakika ya 57 ya mchezo Shaban Kisiga aliipatia Mtibwa Sugar bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati kufuatia mlinzi Rajab Zahir kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari na Kisiga kufunga penati hiyo na kupata bao la kusawazisha.
Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 80 ya mchezo kufuatia mlinzi wa kati wa Mtibwa Sugar Salvatory Ntebe kumkwatua Tegete na mwamuzi kuamuru penati ambayo aliipiga Tegete na kuukwamisha mpira wavuni.
Huku washabiki wa soka wakianza kutoka nje na wengine wakiwahi kufuturu Hussein Javu aliifungia Yanga bao la tatu na la ushindi dakika ya 87 ya mchezo kufuatia mpira aliorudhishiwa golikpa Said Mohamed kushindwa kuuondoa na Javu kuuwahi na kuhesabu bao la tatu kwa watoto jangwani.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 3 - 1 Mtibwa Sugar.
Mara baada ya mchezo kocha mkuu wa Yanga Ernie Brandts amesema kikosi chake kinaendelea kuimarika na wachezaji wanaonekana kushika vizuri mafunzo yake, anaendelea na mazoezi kwa hizi wiki mbili kabla ya kucheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya timu ya Azam FC Agosti 17 2013.
Young Africans: 1.Deogratius Munishi 'Dida'/Ally Mustapha 'Barthez', 2.Juma Abdul, 3.Oscar Joshua/David Luhende, 4.Nadir Haroub 'Cannavaro'/Rajab Zahir, 5.Issa Ngao, 6.Athuman Idd 'Chuji/Bakari Masoud, 7.Said Bahanuzi/Abdallah Mguhi 'Messi', 8.Salum Telela, 9.Jerson Tegete, 10.Shaban Kondo/Hussein Javu, 11.Haruna Niyonzima.

Twanga Pepeta kumtambulisha Ige Moyaba na wengine Mango Garden siku ya Idd Pili

Ige Moyaba aliyerejea tena Twanga atatambulishwa Idd Pili
BENDI ya African Stars “Twanga Pepeta” itatambulisha wanamuziki wapya pamoja na warembo watakaoshiriki Miss Ilala siku ya Iddi Pili Katika ukumbi wao wa Mango Garden, Kinondoni.
Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka alisema jana kuwa onyesho hilo limeandaliwa na Bob Entertainment na kudhaminiwa na Konyagi, Freddito Entertainment, Saluti5 na Twitter Pub.
Alisema wanamuziki watakaotambulishwa siku hiyo maalum ni wanenguaji wapya, muimbaji Ige Moyaba ambaye alikuwa mwanamuziki wa bendi hiyo kabla kwenda Ufaransa kuendeleza kipaji chake.
 “Tumeamua kuleta wanenguaji wapya kabisa, wenye damu changa ili kuleta mapinduzi kwenye muziki wa dansi. Madansa wetu ni mabinti warembo, pia tuna  wanenguaji watanashati,” alisema Asha na kuongeza kuwa awameamua kubadilisha wanenguaji ili kuenda na wakati pamoja na soko la muziki.
Kwa upande wa Ige Moyaba aliyetamba kwenye albamu ya ‘Mtu Pesa’ katika mwaka wa 2004,  Asha alisema ameanda vitu vipya kuwapa mashabiki wa bendi hiyo inayotamba kwa staili ya Kisigino.
“Kwa kweli hi siyo onyesho la kukosa kwani itakuwa ni zawadi yetu ya Idd kwa mashabiki wetu,” mkurugenzi huyo alisema.
Mwezi uliyopita Twanga Pepeta walizindua albamu yao ya 10 lijulikanayo kana “Nyumbani ni Nyumbani”.
Albamu zingine ambazo zitapigiwa siku hiyo ni Jirani, Fainali Uzeeni, Chuki Binafsi, Ukubwa Jiwe, Mtu Pesa, Safari, Password, Mtaa Wa Kwanza, Mwana Dar es Salaam na Dunia Daraja.
Naye mratibu wa onyesho hilo Joseph Kapinga alisema kuwa warembo watakoshiriki kwenye shindano la kumtafuta Redds Miss Ilala pia watatambulishwa siku hiyo.
BENDI ya African Stars “Twanga Pepeta” itatambulisha wanamuziki wapya pamoja na warembo watakaoshiriki Miss Ilala siku ya Iddi Pili Katika ukumbi wao wa Mango Garden, Kinondoni.
Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka alisema jana kuwa onyesho hilo limeandaliwa na Bob Entertainment na kudhaminiwa na Konyagi, Freddito Entertainment, Saluti5 na Twitter Pub.
Alisema wanamuziki watakaotambulishwa siku hiyo maalum ni wanenguaji wapya, muimbaji Ige Moyaba ambaye alikuwa mwanamuziki wa bendi hiyo kabla kwenda Ufaransa kuendeleza kipaji chake.
 “Tumeamua kuleta wanenguaji wapya kabisa, wenye damu changa ili kuleta mapinduzi kwenye muziki wa dansi. Madansa wetu ni mabinti warembo, pia tuna  wanenguaji watanashati,” alisema Asha na kuongeza kuwa awameamua kubadilisha wanenguaji ili kuenda na wakati pamoja na soko la muziki.
Kwa upande wa Ige Moyaba aliyetamba kwenye albamu ya ‘Mtu Pesa’ katika mwaka wa 2004,  Asha alisema ameanda vitu vipya kuwapa mashabiki wa bendi hiyo inayotamba kwa staili ya Kisigino.
“Kwa kweli hi siyo onyesho la kukosa kwani itakuwa ni zawadi yetu ya Idd kwa mashabiki wetu,” mkurugenzi huyo alisema.
Mwezi uliyopita Twanga Pepeta walizindua albamu yao ya 10 lijulikanayo kana “Nyumbani ni Nyumbani”.
Albamu zingine ambazo zitapigiwa siku hiyo ni Jirani, Fainali Uzeeni, Chuki Binafsi, Ukubwa Jiwe, Mtu Pesa, Safari, Password, Mtaa Wa Kwanza, Mwana Dar es Salaam na Dunia Daraja.
Naye mratibu wa onyesho hilo Joseph Kapinga alisema kuwa warembo watakoshiriki kwenye shindano la kumtafuta Redds Miss Ilala pia watatambulishwa siku hiyo.

Wanahabari wa Habari Group watoa msaada kwa yatima


Diwani wa Viti Maalumu na Mwenyekiti Mtendaji wa Aisha Sururu Foundition, Bi. Aisha Sururu kulia akiwakabidhi sehemu ya msaada alioutoa kwa ajili ya kuchangia yatima kwa wanachama wa kikundi cha Habari Group, Rabia Bakari (kushoto) na Asha Bani kwa ajili ya kupeleka kwa yatima katika vituo mbalimbali  Misaada mingine ilitolewa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, January Makamba, Mmiliki wa Maduka ya Silva Botique, Madam Nora, Katibu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa kiislam Sheikh  Khamisi Mataka, na Mkurugenzi wa Kampuni ya QUALITY Printers And Stationers Amani Soko

Diwani wa Viti Maalumu na Mwenyekiti Mtendaji wa Aisha Sururu Foundition, Bi Aisha Sururu (kushoto) akiwakabidhi sehemu ya msaada alioutoa kwa ajili ya kuchangia yatima kwa wanachama wa kikundi cha Habari Group Rabia Bakari na Asha Bani kwa ajili ya kupeleaka kwa yatima wa vituo mbalimbali.

Wanachama wa kikundi cha Habari Group, Rabia Bakari (kulia) na Asha Bani wakiangalia baadhi ya vyakula na vitu mbalimbali walivyokabidhiwa kwa ajili ya kwenda kugawa kwa  yatima.
Sehemu ya misaada hiyo

Wanachama wa Habari Group wakia katika picha ya pamoja na na mwenyekiti mtendaji wa Aisha Sururu Foundition Bi. Aisha Sururu
Moja ya kituo cha kilichopewa misaada na Habari Group Leo

Mwanachama wa Kikundi cha Habari Group, Asha Bani (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada  walioutoa kwa  Katibu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Hidaya Orphans Center and Tahfidhil-qur-an cha Buguruni Bw. Abubakari Simba jijini Dar es salaam leo.

Baadhi ya wanachama wa kikundi cha habari Group wakiwa katika picha ya pamoja na  yatima wanaolelewa katika Kituo cha Al-Hidaya Orphans Center and Tahfidhil-qur-an cha Buguruni baada ya kutoa misaada mbalimbali leo

Mwanachama wa Kikundi cha Habari Group, Asha Bani kulia akikabidhi sehemu ya msaada walioutoa kwa  Katibu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Hidaya Orphans Center and Tahfidhil-qur-an cha Buguruni Bw. Abubakari Simba Dar es salaam leo.

Mwanachama wa Kikundi cha Habari Group, Asha Bani (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada  walioutoa kwa  Msimamizi Mkuu wa kituo cha kulelea yatima cha Al Furqan Islamic Center cha Chanika Bw. Hamisi Omari  Dar es salaam leo
Baadhi ya wanachama wa kikundi cha habari Group wakiwa katika picha ya pamoja na  yatima wanaolelewa katika kituo cha Al Furqan Islamic Center cha Chanika baada ya kutoa misaada mbalimbali leo.