Wamasai wakionyeshana umahiri wa kucheza ngoma |
WATU wawili wenye asili ya kabila la Kimasai wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, kwa tuhuma za kumbaka binti mwenye umri wa miaka 15 eneo la Goba, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa hao wametajwa kuwa ni Elisoloi
Leid (17) na Jackson James (12), wote wakazi wa Goba jijini Dar es
Salaam ambao wanatuhumiwa kumbaka mke wa mmasai mwenzao.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,
Wamasai hao walifanya kitendo hicho Jumatano wiki hii majira ya
asubuhi, muda mfupi baada ya mwenye mke kuondoka kwenda kwenye shughuli
zake.
Mmoja wa mashuhuda hao, John Isack alisema
kuwa, wamasai hao walikutwa wakimbaka binti huyo wakati mafundi ujenzi
walipofika asubuhi kuchukua vifaa vya ujenzi kwenye nyumba wanayoishi.
Alisema kuwa mafundi hao walikuta mlango
wa nyumba umefungwa na walipogonga bila kufunguliwa walisikia sauti ya
msichana ndani ikilia. Ndipo mmoja wa mafundi hao alipopiga teke mlango
na kuwakuta wamasai hao wakimbaka binti huyo.
Kufuatia tukio hilo, baadhi ya wananchi
eneo hilo walijitokeza na kuwazingira kwa kuwaweka chini ya ulinzi, huku
wengine wakiwa wameshika silaha mbalimbali za jadi kuwatishia
wasikimbie mpaka hapo polisi watakapokuja kuwachukua.
Wamasai hao walishikiliwa na wananchi hao
kwa muda wa nusu saa na baadaye pikipiki mbili zilikodiwa ambapo moja
ilimbeba binti huyo na nyingine watuhumiwa na kupelekwa kituo cha polisi
cha Kawe kwa hatua zaidi.
Shuhuda mwingine Amina Mohamed, alisema
kuwa unyama aliofanyiwa binti huyo umetokea siku chache baada ya kuja
jijini Dar es Salaam kuishi na mume wake.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni,
Camillus Wambura amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumtaja mume wa
binti huyo kwa jina moja la Saaya.
Kamanda Wambura alisema Saaya aliwaleta
watuhumiwa hao kutoka umasaini kwa lengo la kuwatafutia kazi za ulinzi.
Alisema siku ya tukio, aliondoka asubuhi na kuwaacha wakiwa na mke wake,
ndipo walipombaka. Kamanda alisema Saaya na mke wake waliondoka siku ya
pili yake baada ya kutoa maelezo polisi kuelekea kijijini kwao.
Wambura alisema wanaendelea kuwashikilia wamasai hao kwa uchunguzi zaidi na utakapokamilika watafikishwa mahakamani.
CHANZO:
NIPASHE