STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, May 8, 2014

Mtanzania mwingine adakwa na 'Unga' Kenya

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiR-x2JlYi-ME1lAl7jUW45J716UnmxnN8WsOfegN9uP6qvMV4KtGzI7jM1XI2MSs7NO-TZu6netj0h9WyxrA0gGDLL8gOBxxjoXB7-IKGAVWAxgYcak7eG3R2X_9MqLqw0zOwxdthyphenhyphenN8T8/s640/Drugs(3).jpgMWANAMME mmoja Mtanzania amekamwata katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi Kenya akiwa amebeba dawa za kulevya akiwa njiani kuelekea Antananarivo ambapo mzigo huo ulitokea Tanga kisha ukapita Mombasa na baadae kwa ndege mpaka Nairobi.
Mzigo wenyewe ni wa cocaine na Heroin ambazo zote zina thamani ya zaidi ya shilingi milioni 24 za Kitanzania na dawa hizo alikua  ameziingiza katika njia ya haja kubwa.
Mkuu wa kitengo cha CID katika uwanja huo Joseph Ngisa amesema mshukiwa alikamatwa JKIA na akawekwa kwenye chumba cha uchunguzi na baadae akatoa tembe za cocain na tembe za Heroin na tayari ameshapelekwa Mahakamani.

Mwezi March mwaka huu watanzania wanne walikamatwa katika uwanja huohuo walipopatikana na heroin yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 75 za Kitanzania na wote walifikishwa mahakamani na kukiri kosa.
Wanawake watatu na mwanaume mmoja kila mmoja akishtakiwa kando kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya na walikua wameingia Kenya kupitia Namanga na walikamtwa wakiwa njiani kuelekea Hong Kong.
Kuanzia March 2014 mpaka leo hii May ni jumla ya Watanzania watano wamekamatwa kwenye kiwanja cha ndege Nairobi wakiwa kwenye pilika za kusafirisha dawa za kulevya kwenda kwenye mataifa mengine.

Real Madrid bado watesa kwa Utajiri Duniani

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2013/02/11/article-2277207-17848A69000005DC-464_964x505.jpgKLABU ya Real Madrid bado imeendelea kung'ang'ania kileleni katika orodha ya vilabu vyenye thamani zaidi duniani(Most Valuable Football Clubs) kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Katika orodha hiyo klabu ya Manchester United imeendelea kuwa juu ya vilabu vya England licha ya kufanya vibaya msimu huu.
Manchester United imeshuka thamani kwa 11% tangu ilipomuajiri David Moyes kama kocha wake mkuu.

Chini ya Moyes Manchester United imepata hasara ya £181.5m, huku majirani zao Manchester City wao wamepanda thamani kwa 25%
Orodha kamili ya Klabu hizo Tajiri Duniani ni;

Yanga waitana kuijadili katiba yao



UONGOZI wa klabu ya Young Africans Sports Club umeitisha mkutano mkuu wa wanachama wa mabadiliko ya Katiba ili wanachama waweze kutoa maamuzi kwenye baadhi ya vipengele vilivyoongezwa kabla ya kuelekea kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa viongozi.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu mitaa ya Twiga/Jangwani, Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema wamefikia kuitisha mkutano huo wa mabadiliko ya Katiba ili wanachama wapate fursa ya kupitisha baadhi ya vipengele kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
“Tumekua na mawasiliano na TFF juu ya kuongezwa baadhi ya vipengele kwenye Katiba yetu kabla ya kufanya uchaguzi mkuu wa viongozi, baada ya hapo ni nafasi kwa wanachama wa Yanga sasa kukutana na kuweza kupitisha hivyo vipengele vitakavyoongezwa kwenye Katiba Mpya” alsiema Beno.
Aidha Beno amesema wanachama wakishapitisha/kukubaliana juu ya hivyo vipengele ndipo uoungozi utawasilisha mapendekezo hayo kwa TFF ambayo ikishayabariki, yatapelekewa kwa Msajili nae akiyapitisha ndipo itakua tayari ni Katiba halali ambayo itatumika kwwenye uchaguzi mkuu.
“Nawaomba wanachama wa Yanga wajitokeze kwa wingi kwenye mkutano wa mabadiliko juni mosi 2014  ili waweze kupitisha hivyo vipengele ambavyo vitapelekea kuwa na Katiba Mpya itakayotumika kwa  shughuli za kila siku za klabu ya Yanga SC” aliongea Beno. 
Eneo na Ukumbi utakapofanyika mkutano huo Juni Mosi 2014 utatangazwa hivi karibuni mara baada ya taratibu zote kukamilika.
CHANZO: TOVUTI YA YANGA

Yanga, TPB wapo kisasa zaidi kidigitali

Makamu Mwenyekiti wa kalbu ya Yanga SC Bw Clement Sanga (katikati) akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya Benki ya Posta, kulia ni mkurugenzi masoko wa Benki ya Posta Bw. Deo Kwiyukwa
Klabu ya Young Africans imeeingia makubaliano na Benki ya Posta nchini juu ya mabadiliko ya utengenezaji wa kadi za wanachama kutoka kwenye mfumo wa zamani (analogy) kwenda kwenye mfumo mpya wa kisasa (digital) ambapo sasa wanachama wake watakua wakitumia kadi zenye mfumo wa ATM.
Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Posta  nchini Bw. Deo Kwiyukwa amesema wamefikia makubaliano hayo baada ya kukaa na viongozi na kuona njia hiyo itaisaidia klabu kuongeza mapatao kwani wigo wake wa kuandikisha wanachama utakua ni mkubwa kwa nchi nzima na kwa muda mfupi.
“Badala ya wanachama kuja Dar es salaam makao makuu kujaza fomu za uanachama watakua wanaweza kufanya hivyo popote walipo kwa kwenda ofisi za Benki ya Posta na kujaza fomu hizo na baadae kupewa kadi ya uanachama” alisema Deo. 
Gharama za kujiunga na uanchama zitabakia zile zile Tshs 15,000/=, na ada ya mwaka elfu Tshs 12,000/= ambapo mwanachama wa Yanga atapata kadi ya TPB yenye logo ya timu yake ambayo pia ataitumia kwenye shughuli za kibenkI kwa huduma ya kuweka na kutoa fedha.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Clement Sanga amesema anaishukuru Benki ya Posta kwa kuweza kufikia makubalianao hayo, kwa kutumia mfumo huu wa kisasa tutaweza kujua idadi ya wachama wetu walio hai kwa wepesi zaidi na taarifa zetu zitaweza  kuwafikia wanachama kwa uharaka zaidi.
Uzinduzi rasmi wa kadi mpaya za uanachama utafanyika tarehe 16.05.2014 kwenye hoteli ya Hyatt Kempsinki eneo la Posta (zamani Kilimanjaro Hotel) na mara baada ya uzinduzi moja kwa moja zoezi la kuhamisha wanachama kutoka kwenye mfumo wa analogy kwenda digital utaanza.
CHANZO: TOVUTI YA YANGA

Kumekucha uchaguzi Simba

http://ptblog.pesatimes.com/wp-content/uploads/2014/05/ndumbaro-300x2531.jpg
WANACHAMA wa klabu ya soka ya Simba wataanza kuchukua fomu za kuwania uongozi wa klabu hiyo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Juni 29.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa klabu hiyo Damas Ndumbaro fomu zitatolewa kuanza kesho kuelekea kwenye kinyang'anyiro hicho cha uchaguzi unaokuja baada ya uongozi wa akina Ismail Aden Rage kumaliza muda wao kesho.

FIFA yaanika orodha mpya ya viwango duniani

http://www.dailyvedas.com/wp-content/uploads/2014/04/Team.jpgWAKATI Brazil ikipanda kwa nafasi mbili katika orodha ya viwango vya soka duniani hadi kuingia kwenye Top 4, Tanzania yenyewe imeendelea kung'ang'ania katika nafasi ya 122 duniani.
 Brazil wenyeji wa michuano ya Fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu, imezipiku nchi za Colombia na Uruguay waliokuwa wamewatangulia katika mwezi uliopita ikiwa nyuma ya Hispania inayooendelea kuongoza orodha ya FIFA iliyotangazwa leo.
Mbali na Hispania, nchi nyingine zilizoitangulia Brazil ni Ujerumani wanaoshika nafasi ya pili kama orodha ya Aprili na Ureno kadhalika wakiwa nafasi ya tatu.
Katika orodha ya 20 Bora, nyuma ya Brazil kuna Colombia, Uruguay, Argentina, Uswiss, Italiaa, Ugiriki, England, Ubelgiji, Chile, Marekani, Uholoanzi, Ufaransa, Ukraine, Russia, Mexico na Croatia iliyofunga ndimba.
Kwa orodha ya Afrika Ivory Coast imeendelea kuongoza orodha ikiwa katika nafasi ya 21 duniani ikifuatiwa na Misri wanaokamata nafasi ya 24, Algeria (25), Ghana (38), Cape Verde (42), Nigeria (44), Tunisia (49), Cameroon (50), Guinea (51) na Mali (59) waliofunga 10 Bora ya Afrika.
Ukanda wa CECAFA kama kawaida Uganda wameendelea kutisha wakishinda nafasi ya 18 Afrika na 86 Duniani, ikifuatiwa na  Ethiopia wanaokamata nafasi ya 101 Duniani na 27 Afrika.
Nyingine zinazozifuata timu hizo ndani ya CECAFA ni Kenya, Sudan, Tanzania, Burundi, Rwanda, Eritrea, Sudan Kusini, Somalia na Djibout inayoburuza mkia.

Hiki ndicho kikosi cha timu ya Ujerumani

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEibSP_Yg7CYyjdkHBV1ejPgbs7Bwfb81J1wLzQfBJrScwYqEj7mtWCc6wRXIWut4Ls_dd3I2MJM49ksFvcyOJZ-bQ18cGvhgJEf7NbxuRm8xDt7Fod8xS0VJKkv7m7IOZHJGV1JoIMiD6sf/s400/Germany+National+Football+Team+Fifa+World+Cup+2014+6.png
SIKU moja baada ya Brazil kutangaza kikosi chao cha ushiriki wa Fainali za Kombe la Dunia, Ujerumani nao wametengaza leo kikosi chake, huku klabu ya Arsenal ikifanikiwa kuwatoa wachezaji watatu akiwamo Kiungo Mesut Ozil.
Wengine walioteuliwa katika kikosi hicho kwa ajili ya Fainali za Dunia zitakazofanyika mwezi ujao nchini Mshambuliaji wa Chelsea, Andre Schurrle pia ameteuliwa katika kikosi hicho kilichotangazwa na kocha wa timu hiyo Joachim Low.
Kikosi kamili cha Ujerumani ni;
 Makipa: Manuel Neuer (Bayern Munich), Roman Weidenfeller (Borussia Dortmund) na Ron-Robert Zieler (Hannover)

Mabeki: Erik Durm (Borussia Dortmund), Jerome Boateng (Bayern Munich), Kevin Grosskreutz (Borussia Dortmund), Benedikt Howedes (Schalke), Mats Hummels (Borussia Dortmund), Marcell Jansen (Hamburg), Philipp Lahm (Bayern Munich), Per Mertesacker (Arsenal), Shkodran Mustafi (Sampdoria) na Marcel Schmelzer (Borussia Dortmund).
 
Viungo: Lars Bender (Bayer Leverkusen), Julian Draxler (Schalke), Matthias Ginter (Freiburg), Leon Goretzka (Schalke), Mario Gotze (Bayern Munich), Andre Hahn (Augsburg), Sami Khedira (Real Madrid), Toni Kroos (Bayern Munich), Max Meyer (Schalke), Thomas Müller (Bayern Munich), Mesut Ozil (Arsenal) na Marco Reus (Borussia Dortmund)

Washambuliaji: Lukas Podolski (Arsenal), Andre Schurrle (Chelsea), Miroslav Klose (Lazio) na Kevin Volland (Hoffenheim).

Kocha Mkuu Yanga asitisha mkataba, apata ulaji Saudia

Kocha wa Yanga, Hans aliyesitisha mkataba na klabu hiyo
TAARIFA ambazo inatolewa muda huu na Uongozi wa Yanga ni juu ya kuacha kazi kocha wa timu hiyo Hans Van Der Plujim ambaye aliungana na timu hiyo January 2014,sababu za kocha huyo kuacha kazi ni kile kilichoelezwa kuwa amepata dili nchi nyingine na mkataba wake na Yanga ulikua unamalizika July mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Yanga inasema kuwa, Hans Van Der Pluijm kocha mkuu wa timu ya Young Africans leo amewaaga rasmi wachezaji wake, viongozi, wapenzi  na wanachama baada ya kumalizaa wake wa miezi sita na sasa anakwenda kujiunga na timu Al Shoalah FC iliyopo Ligi Kuu nchini Saudi Arabia. 
Kocha huyo mdachi ambaye ameiongoza Young Africans kwa kipindi cha miezi mitano amesema anashukuru kwa sapoti aliyokua akiipata kutoka kwa wachezaji, viongozi, wapenzi na wanachama wa timu hii kwa kipindi chote alipokuwa nchini Tanzania.
"Najua wengi itawashangaza kuona naondoka lakini ukweli ni kwamba niikua na hiyo deal hata hata kabla ya kuja Yanga, nilikua na makubaliano na timu ya Al Shoalah FCmakubaliano ambayo yanaanza mwezi ujao hivyo nilikubaliana na viongozi wa Yanga kuja kufanya kazi kwa kipindi cha miezi sita tu, nashukuru tumefanya kazi salama na baada ya mkataba huo kuisha nipo tayari kurudi kuja kufanya kazi Tanzania" alisema Hans
Naipenda Yanga SC, nimejaza fomu kuomba uanachama hivyo mimi ni sehemu ya Yanga na katika usajili ujao nitawasaidia kuleta wachezaji wazuri ambao wataisaidia timu kwenye msimu ujao kwa Ligi ya Vodacom na mashindao ya Kimataifa.
Kocha Hans anaondoka leo nakwenda Ghana kisha baadae atakwenda nchini Saudu Arabia tayari kwa kujiandaa na maandalizi ya msimu ujao katika timu yangu hiyo ambayo nitaitumikia kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Kuhusu usajili kocha mkuu ameshakabidhi ripoti yake ya kiufundi jana, viongozi wanaifanyia kazi kisha baadae itawekwa wazi.

Michuano ya Beach Soccer yafikia patamu Dar

MICHUANO ya soka ya ufukweni (beach soccer) inayoendeshwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikishirikisha vyuo mbalimbali vya Dar es Salaam imeingia hatua ya robo fainali.
Robo fainali hiyo inayoshirikisha timu nane itachezwa Jumamosi (Mei 10 mwaka huu) kwenye ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni kuanzia saa 5 asubuhi, huku Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Taasisi ya Ustawi wa Jamii (SWI) zikicheza robo fainali ya kwanza.
Chuo Kikuu cha Ardhi (AU) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere watcaheza robo fainali ya pili kuanzia saa 6 kamili. Saa 8 kamili itaanza robo fainali ya tatu itakayozikutanisha Taasisi ya Uhasibu (TIA) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Robo fainali ya mwisho itakayoanza saa 9 kamili itakuwa kati ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Chuo cha Utumishi Magogoni. Washindi watacheza nusu fainali Jumapili (Mei 11 mwaka huu) kwenye ufukwe huo huo.
Mechi za kutafuta mshindi wa tatu, na ile ya fainali zitachezwa kwenye ufukwe huo huo wikiendi ya Mei 17 mwaka huu.