STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 23, 2013

Polisi Dar wanamnasa msanii Bongo Movie kisa picha za utupu alizopiga na mademu na kusambaza mitandaoni


 
 JESHI la polisi kanda ya Dar es Salaam linadaiwa kumtia mbaroni msanii anaetuhumiwa kupiga picha chafu na wanawake mchanganyiko wakiwema mamiss maarufu na baadae kusambaza kwenye mitandao yote ya kijamii pamoja na kuripotiwa kwenye magazeti mbalimbali
 
Mwandishi wetu amefanikwa  kuzinasa  picha  za  Manaiki  akiwa chini ya ulinzi wa  polisi huku akiwa amevishwa pingu na kurukishwa kichurachura.
 
Manaiki mbaroni-Udaku

Mbongo mwingine anaswa na dawa za kulevya Dubai, watatu wauwawa Afrika Kusini

WAKATI kukiwa na taarifa kwamba watanzania watatu wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya kuuwawa kwa kufyatuliwa risasi nchini Afrika Kusini, Tanzani imeendelea kuaibika baada ya Mbongo mwingine kutiwa mbaroni akiingiza 'unga' Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE)

Mtanzania huyo aliyenaswa umangani, inaelezwa lidakwa tarehe 19/8/2013 baada ya Polisi mjini Sharjah na wale wa Dubai kuwakamata watu watano mmoja akiwa ni raia wa Tanzania.
Watuhumiwa hao walinaswa na kilo kilo 19 za heroin na kilo 4 za bangi na kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo wanaonaswa na 'unga' adhabu yake ni kifungo cha maisha
Isome mwenyewe habari juu ya aibu hiyo nyingine kwa Tanzania ambayo imekuja huku kukielezwa Watanzania watatu wanaohusika na 'unga' wameuwawa Afrika Kusini kwa kufyatuliwa risasi.

The anti-narcotics department of police and other police teams have tracked down and arrested a five-strong gang accused of smuggling a large amount of drugs into the country.The group members, including three Emirati men, one man from the Comoros Islands and another from Tanzania, were arrested and charged with smuggling and possession of 19kg of heroin and four kilograms of marijuana.
The group is accused of smuggling drugs in order to sell them.
The arrest was made after the anti-narcotics department was able to gather information through confidential sources about a group of people who were in possession of a large amount of drugs.

Sharjah Police, in collaboration with Dubai Police and the anti-narcotics departments of the Ministry of Interior and Ajman Police, were able to track down two of the offenders who were in possession of two kilograms of marijuana along with 150 grams of heroin.

The other three suspects were tracked down and arrested soon after, along with a larger quantity of drugs that were found buried in the desert in Sharjah and Ajman.

Major General Humaid Mohammad Al Hudaidi, commander in chief of Sharjah Police, said that collaboration of all the police teams in the UAE led to tracking down of the suspected drug smugglers and distributors.

He said that through the use of strategic tools and sources, police were able to disclose the group’s plan to distribute and sell the drugs to young people in the country.
source -jamii forums

Hawa ndiyo waombaji Uchaguzi Mikuu TFF, Wambura 'aingia' mitini

Athuman Nyamlani aliyejitosa kwenye Urais
Jamal Malinzi naye yumo
 Na Boniface Wsambura
KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imebandika rasmi kwenye ubao wa matangazo majina ya waombaji uongozi kwenye uchaguzi wa TFF na Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ili kutoa fursa kwa pingamizi.

Kipindi cha pingamizi kinaanza kesho (Agosti 24 mwaka huu) hadi sas 10 kamili jioni ya Agosti 26 mwaka huu ambapo waweka pingamizi wanaruhusiwa kupitia taarifa za wale wanaokusudia kuwawekea pingamizi kabla ya kuwasilisha pingamizi husika.

Kwa mujibu wa tangazo la uchaguzi, Agosti 27 hadi 29 mwaka huu ni wawekaji pingamizi na wawekewa pingamizi kufika mbele ya Kamati ya Uchaguzi kwa ajili ya kusikiliza pingamizi.

Waombaji kuwania uongozi katika TFF ambao majina yao yamebandikwa ni Athuman Jumanne Nyamlani, Jamal Emil Malinzi, Omari Mussa Nkwarulo na Richard J. Rukambura (urais). Nafasi ya Makamu wa Rais ni Imani Omari Madega, Ramadhan Omari Nassib na Walace John Karia.

Walioomba nafasi za ujumbe kuwakilisha kanda ni Kanda Namba Moja (Kagera na Geita) ni Abdallah Hussein Mussa na Kaliro Samson. Kanda Namba Mbili (Mara na Mwanza) ni Jumbe Odessa Magati, Mugisha Mujwahuzi Galibona, Samwel Nyalla na Vedastus Kalwizira Lufano.

Kanda Namba Tatu (Shinyanga na Simiyu) ni Epaphra Amana Swai, Mbasha Matutu Mong’ateko na Stanslaus Haroon Nyongo. Kanda Namba Nne (Arusha na Manyara) ni Ally Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omari Walii Ali.

Kanda Namba Tano (Kigoma na Tabora) ni Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamisi Kitumbo. Kanda Namba Sita (Katavi na Rukwa) ni Ayoub Nyaulingo, Blassy Mghube Kiondo, Nazarius A.M. Kilungeja. Kanda Namba Saba (Iringa na Mbeya) ni Ayoub Shaibu Nyenzi, Cyprian Charles Kuyava, David Samson Lugenge, Elias Lusekelo Mwanjala, Eliud Peter Mvella na John Mwachendang’ombe Kiteve.

Waombaji wa Kanda Namba Nane (Njombe na Ruvuma) ni James Patrick Mhagama, Kamwanga Rajabu Tambwe na Stanley William Lugenge. Kanda Namba Tisa (Lindi na Mtwara) ni Athuman Kingome Kambi, Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee Damoder.

Kanda Namba Kumi (Dodoma na Singida) ni Charles Komba, Hussein Zuberi Mwamba na Stewart Ernest Masima. Kanda Namba 11 (Morogoro na Pwani) ni Farid Salum Mbarak, Geoffrey Irick Nyange, Juma Abbas Pinto, Riziki Juma Majala na Twahil Twaha Njoki.

Wanaowania kuteuliwa kugombea kupitia Kanda Namba 12 (Kilimanjaro na Tanga) ni Davis Elisa Mosha na Khalid Abdallah Mohamed wakati Kanda Namba 13 (Dar es Salaam) ni Alex Chrispine Kamuzelya, Muhsin Balhabou, Omar Isack Abdulkadir, Shaffih Dauda Kajuna na Wilfred Mzigama Kidao.

Kwa upande wa TPL Board waliotangazwa kuomba kuwania uongozi wa juu ni Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti) na Said Muhammad Said Abeid (Makamu Mwenyekiti).

Wajumbe wa Kamati ya Uendeshaji ni Kazimoto Miraji Muzo, Michael Njunwensi Kaijage, Omari Khatibu Mwindadi, Salum Seif Rupia na Silas Masui Magunguma.

Mmoja wa wagombea machachari aliyewahi kuongoza Shirikisho hilo enzi za FAT, Michael Wambura hajajitokeza safari hii kuwania nafasi yoyote bila kufahamika kitu gani kilichomkuta.

Golden Bush Veterani, Mwanza United kuvaana Jumapili


Kikosi cha Golden Bush
WAKALI wa soka la jijini Dar es Salaam, Golden Bush Veterani Jumapili inatarajiwa kushuka dimbani kuvaana na Mwanza United inayoundwa na wakali wa zamani kama George Masatu.
Kwa mujibu wa msemaji wa Golden Bush, Onesmo Waziri 'Ticotico', pambano hilo litachezwa asubuhi kwenye uwanja wa Kines, maarufu kama St James Park.
Ticotico alisema kikosi chao kipo imara kwa ajili ya pambano hilo ambalo Mwana Utd inatarajiwa kusheheni wakali kama Masatu, Benjamin Magadula, Aaron Nyanda, George Nyanda Emmanuel Switta na wengineo.
"Baada ya kutoa vipigo kwa wapinzani wetu wengine wakifikia hatua ya kugoma kucheza nasi, Jumapili tutavaana na Mwanza United hivyo mashabiki waje waone soka la kutakata," alisema.
Ticotico alisema mashabiki wake washuhudie beki kisiki, Masatu akatavyokuwa na kazi ya kuwazuia washambuliaji hatari wa Golden Bush ambayo inaundwa na nyota wa zamani wa Simba, Yanga na Taifa Stars pamojana wakongwe wanaoendelea kucheza sasa.

Tiketi za Elektroniki kutumika mzunguko wa nne

Rais wa TFF leodger Tenga
Na Boniface Wambura
TIKETI za elektroniki zitaanza kutumika katika mzunguko wa nne wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) utakaoanza Septemba 18 mwaka huu. Tayari benki ya CRDB ambayo ndiyo ilishinda tenda hiyo imeshakamilisha ufungaji wa vifaa kwa ajili ya matumizi ya tiketi hizo katika viwanja vyote.

Hivi sasa Serikali ambayo ndiyo inamiliki Uwanja wa Taifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na CRDB zinashughulikia mfumo wa tiketi hizo kwenye uwanja huo ambao ndiyo ulikuwa haujakamilika kwa matumizi katika upande huo.

Mfumo (system) iliyoko kwenye uwanja huo inapishana na ule utakaotumiwa na CRDB, hivyo pande husika zinashughulikia suala hilo ili mifumo hiyo iweze kuingilia.

Pia mashine za kuchapia (printer) kwa ajili ya tiketi ambazo CRDB wameziagiza kutoka nje ya nchi zinatarajiwa kuwasili mwishoni mwa mwezi huu.

Hivi sasa CRDB inashughulikia ufungaji wa vifaa vya matumizi ya tiketi za elektroniki iwemo turnstiles kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ambao mwanzoni hakuwemo kwenye mpango huo kutokana na Mkoa wa Tabora kutokuwa na timu ya Ligi Kuu.

Kivumbi cha Ligi Kuu kuanza kesho, Yanga, vijana wa Ashanti hapatoshi Dar

Mabingwa watetezi Yanga watakaoanza kibarua dhidi ya Ashanti United iliyorejea ligi Kuu tena
Na Boniface Wambura
PAZIA la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2013/2014 litafunguliwa kesho (Agosti 24 mwaka huu) katika viwanja saba tofauti ambapo mabingwa watetezi Yanga wakianza kutetea ubingwa wao kwa kuikaribisha Ashanti United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Azam ya Dar es Salaam na wenyeji Mtibwa Sugar. Oljoro JKT itaikaribisha Coastal Union kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.

Mgambo Shooting itaoneshana kazi na JKT Ruvu ambayo hivi sasa iko chini ya Kocha Mbwana Makata. Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Rhino Rangers itakwaruzana na Simba katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Mbeya City iliyopanda VPL msimu huu itapimana ubavu na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya huku Ruvu Shooting ikiialika Mabatini, Mlandizi timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya.

Mzunguko wa pili wa ligi hiyo utachezwa Agosti 28 mwaka huu. Baada ya hapo ligi itasimama kupitisha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Gambia na Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul. VPL itaingia mzunguko wa tatu Septemba 14 mwaka huu.

Kumekucha BSS, Fainali zake kufanyika Nov.17

Madam Ritha akiwa na mshindi wa mwaka jana Walter Chilambo

FAINALI za mashindano ya kusaka vipaji vya kuimba ya Epiq Bongo Star Search (EBSS) mwaka huu zitafanyika Novemba 17 jijini Dar es Salaam, waandaaji walisema jana.
Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Productions, Ritha Poulsen, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa wamejipanga kuboresha mashindano hayo na wadau watarajie kushuhudia fainali zilizoandaliwa katika kiwango cha kimataifa.
Alisema kuwa awali walipata washiriki 50 lakini sasa baada ya kuwachuja wamebaki 20 ambao wataingia kambini na kupewa mafunzo mbalimbali ya muziki kabla ya kuwachuja na kubaki wanane watakaoingia fainali.
“Lengo la kuanza kambini mapema ni kuwapa fursa washiriki kujifunza zaidi vitu muhimu katika muziki na hii itawasaidia kuboresha vipaji vyao," alisema mratibu huyo.
Alisema kuwa washiriki hao waliopatikana wametoka katika mikoa sita ya Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar.
Naye mshindi wa shindano hilo kwa mwaka jana, Walter Chilambo, aliwataka vijana kuondoa aibu ili wajiandae kutimiza ndoto zao za maisha.
“Vijana wengi wamejitokeza msimu huu ila wameonekana kuwa na aibu baada ya kuwaona majaji, hali hii si nzuri na huwezi kufikia malengo," alisema mshindi huyo.
Naye Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, alisema wamejipanga kuhakikisha shindano hilo linakuwa la aina yake mwaka huu kupitia udhamini wa kampuni yake.
Alisema pia bado washiriki wanaendelea kusailiwa kupitia namba ya simu  0901551000 au kutuma ujumbe mfupi kwenda 15530 kama ilivyokuwa kwa mshiriki Meninah Abdulkarim aliyepatikana kwa njia huyo wakati wa mchakato wa mwaka jana.

Mtikisiko katia Dansi! Mzee Gurumo ang'atuka kwenye muziki

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi wa bendi ya Msondo Ngoma, Mzee Muhidin Gurumo, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wake wa kustaafu rasmi kazi ya muziki aliyoifanya kwa muda wa miaka 53 sasa. Gurumo alitoa kauli hiyo leo katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. Picha na Magreth Kinabo.
************************************
Na Jennifer Chamila, Maelezo.
MWANAMUZIKI mkongwe wa bendi ya Msondo Ngoma Mzee Muhidin Gurumo amestaafu rasimi kazi ya muzika alioifanya kwa muda wa miaka 53.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mzee  Gurumo mwenye umri wa miaka 73 amesema ameamua kustaafu kazi hiyo kwa hiari yake mwenyewe kutokana na umri wake kuwa mkubwa.
“Muziki kwangu umekuwa kama asili yangu na kazi yangu lakini nimeamua kustaafu kutokana na umri wangu na nitabaki kuwa mshauri tu kwa mwanamuziki yeyote atakayetaka ushauri wangu,”alisema  Mzee Gurumo.
Pamoja na kufanya kazi ya muziki Gurumo alisema kuwa hakupata mafanikio makubwa zaidi ya kujenga nyumba anayoishi na familia yake.
 “Mimi  nimeimba kwa muda mrefu sana lakini hata baiskeli sina,”alisema Mzee Ngurumo. Hata hivyo alisema  nashukuru kuwa ana nyumba ya kuishi na familia.
Vilevile Mzee Gurumo amewaasa vijana kuwa wabunifu na kuupenda mziki wa zamani kwani ndio chimbuko la bongofleva na kuwashauri wanamuziki wa sasa kuwa wavumilivu kukaa muda mrefu kwenye bendi moja ili hata wanapoondoka mchango wao uthaminiwe.
 Mzee   Gurumo  ambaye ana mke na watoto wanne alisema kuwa katika maisha yake ya muziki alifanikiwa kutunga nyimbo 60,000 na anavutiwa zaidi na mwanamziki Hussein Jumbe na Hassani Lehan Bichuka na kwa wanamuziki wa kizazi kipya anavutiwa na Nassibu Abdul ’Diamond’. 
Mwanamuziki huyo mkongwe alianza kufahamika katika tasnia ya muziki wa dansi kwenye miaka ya 1960 ambapo mwaka 1964 alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa bendi ya Nuta Jazz na Mlimani Park.
Alidumu na Mlimani Park mpaka mwaka 1985 na kuhamia Safari Sound aliyofanya nayo kazi mpaka mwaka 1990 na kujiunga na Msondo Ngoma mpaka sasa alipoamua kutangaza rasmi kustaafu kazi hiyo ya Kimuziki.

Twanga Pepeta, ROMA kupamba tamasha la Gym kesho K'Nyama


KATIKA kuhakikisha Watanzania wanakuwa na afya bora, kinywaji kisicho na kilevi cha Vita Malt, kimeandaa bonanza maalumu litakalowashirikisha wafanya mazoezi na litakalofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Vinywaji visivyo na Vileo katika Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Consolata Adam alisema, wameamua kuandaa bonanza hilo ili kuwakutanisha pamoja wafanya mazoezi wote, ambao mara nyingi wanafanyia katika vituo maalumu (gym).

Consolata alisema, bonanza hilo la aina yake kwa Dar es Salaam litafanyika katika Viwanja vya Posta vilivyopo Kijitonyama kuanzia saa 12 asubuhi hapo kesho (Jumamosi).

“Tumeamua kuandaa bonanza linalowakutanisha wanamichezo mbalimbali hasa wafanya mazoezi ili kuweza kukutana na kufanya mazoezi kwa pamoja.

“Siku hiyo katika Viwanja vya Posta kutakuwa na gym kumi na mbili zilizo maarufu ambazo zitashiriki na kutakuwa na wakufunzi kumi ambao wataongozwa na mkufunzi wa kimataifa SAAS,” alisema, huku akidai mtu anatakiwa kwenda tu kwani mazoezi hayo yatakuwa bure.

Alisema, lengo kuu kuu la bonanza  ni kuhamasisha jamii nzima kutambua umuhimu wa kufanya mazoezi ili kujenga afya bora za miili yao na pia kujenga umoja imara wa gym zilizopo nchini.

Consolata alisema, katika kuhakikisha bonanza hilo linakuwa bora na la kufana jumla ya gym kumi na mbili zitashiriki ambazo ni Better Life, Genessis ya Kijitonyama, Segerea Gym, Rio Gym,Genessis ya Kimara, Azula ya Mikocheni na Serena Gym.

Alisema pia baa zilizoshinda katika kuchoma nyama katika mashindano yaliyofanyika hivi karibuni za Fyatanga ya Tegeta na Kisuma Bar ya Temeke, zitaonyeshana umwamba kwa kuchoma nyama bomba kwa kipindi chote hicho.

“Tumeweka burudani za kila aina kwani kutakuwa na michezo mbalimbali ya kufurahisha kama soka, netiboli, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, Sehemu za watoto kuchezea pia na zawadi nyingi toka Vita Malt zitakuwepo.”

Naye Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa TBL, Edith Mushi alisema mbali na hayo kutakuwa na burudani mbalimbali toka kwa bendi African Stars ‘Twanga Pepeta’ na msanii mkali wa Hip hop, Roma Mkatoliki sambamba na burudani nyingine nyingi kwa kipindi chote cha tamasha.

“Hii ni siku ya familia napenda kuwajulisha watanzania wote na wapenda michezo kote nchini kuwa waje mapema na familia zao siku ya Jumamosi, hakutakuwa na kiingilio chochote na vinywaji vyote toka TBL vitakuwepo.

“Lakini pia watu wa kawaida na wa rika zote siku hiyo hakutakuwa na kikwazo chochote cha kufanya mazoezi, kwani ni bure kabisa, hivyo nawashauri tufike kwa pamoja ili tuweze kupata pia ushauri mbalimbali juu ya kupunguza uzito na aina ya mazoezi yanayotakiwa,” alisema.

Vita Malt ni kinyaji kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).