STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, September 25, 2014

Liverpool yaingia matatani Ulaya

http://cdn3-i.hitc-s.com/69/liverpool_wall_12402.jpgKLABU ya Liverpool ni moja ya vilabu kadhaa vinavyotarajiwa kufanyiwa uchunguzi kama wamekiuka Sheria ya Matumizi ya Fedha-FFP.
Kwa mujibu wa sheria za Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA vilabu vyote barani humo vinapaswa kuweka kikomo cha hasara kutofikia paundi milioni 35.4 kwa misimu miwili. 
Kuna adhabu hutolewa kwa wasiotimiza masharti hayo ambapo Manchester City tayari wameshakumbana nayo kwa kutozwa faini na kuwekewa kiwango cha matumizi katika usajili na kupunguziwa idadi ya wachezaji katika kikosi chake Mei mwaka huu. 
Lakini pamoja na kupata hasara ya paundi milioni 49.8 katika msimu wa mwaka 2012-2013 na paundi milioni 41 msimu wa mwaka 2011-2012, Liverpool wana uhakika wanaweza kuvuka kikwazo hicho bila adhabu. 
Liverpool sambamba na Monaco, Inter Milan na AS Roma ambazo zote hazikushiriki michuano ya Ulaya msimu uliopita tayari zimepeleka taarifa za akaunti zao Bodi ya Udhibiti wa Fedha ya Klabu-CFCB lakini kuna uwezekano wa kuagizwa kupelekea maelezo zaidi kuhusu fedha hizo. 
Msimu uliopita vilabu 76 viliingia katika uchunguzi wa FFP lakini vilabu tisa pekee ndio vilipewa adhabu kwa kukiuka sheria hiyo.

HAWA NDIYO WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA VYUO VIKUU 2014-2015




CHUNGULIA mwenyewe kwa kubofya jina la chuo kupakua faili lenye majina:
  1. BUGANDO BScN_2014.pdf (82.4 KB)
  2. BUGANDO MD.pdf (106.2 KB)
  3. BUGANDO MEDICAL LABORATORY SCIENCES.pdf (79.7 KB)
  4. BUGANDO PHARMACY.pdf (80.0 KB)
  5. BUGANDO NURSING.pdf (76.0 KB)
  6. IFM BACHELOR DEGREE 2014
  7. MAKUMIRA PROPOSED STUDENTS 2014/2015
  8. MUM Undergraduate Selection - Direct.pdf (561.3 KB)
  9. MUM Undergraduate Selection - Equivalent.pdf (202.0 KB)
  10. SAUT Selected Students.pdf (307.3 KB)
  11. ST. AUGUSTINE 2014
  12. ST Franscis MD Batch one (52.3 KB)
  13. ST Franscis MD Batch two (37.2 KB)
  14. ST Franscis MD Batch Three (49.5 KB)
  15. Stella Maris Mtwara.pdf (283.1 KB)
  16. UDSM 2014/2015 
  17. Mwenge Catholic University

Mechi ya Simba Yanga lapeperuka Oktoba 12

http://tff.or.tz/wp-content/uploads/2014/05/taifa-stars-2014.jpg
Stars iliyopeperusha pambano la Simba na Yanga Oktoba 12
PAMBANO la watani wa jadi kati ya Simba na Yanga 'limeota mbawa' Oktoba 12 kutokana na kuwepo kwa pambano la kimataifa kati ya Taifa Stars na Benin.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Stars itacheza na Benin katika mechi inayotambuliwa na FIFA.
Taarifa hiyo inaseme mechi hiyo itachezwa Oktoba 12 kwenye uwanja wa Taifa, siku ambayo Simba na Yanga zilikuwa ziumane kilingana na ratiba ya awali ya Ligi Kuu ambayo sasa inatarajiwa kufanyiwa marekebisho yatakayotangazwa kesho Septemba 26.
Taarifa kamili ya TFF inasomeka hivi:
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inashuka uwanjani Oktoba 12 mwaka huu kuikabili Benin katika mechi ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Programu ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa ajili ya mechi hiyo itatangazwa baadaye na Kocha Mkuu Mart Nooij.Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaendelea na taratibu nyingine kwa ajili ya mechi hiyo ikiwemo usafiri wa Benin kuja nchini, ambapo timu hiyo inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Oktoba 10 mwaka huu ikiwa na msafara wa watu 28.
Pambano la Stars na Benin litatanguliwa na mechi ya kudumisha upendo kati ya viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu.
 Wakati huo huo, kutokana na mechi hiyo ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inafanyiwa marekebisho madogo, na marekebisho hayo yatatangazwa kesho (Septemba 26 mwaka huu).
 RAIS MALINZI KUFUNGA KOZI YA WANAWAKE
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi anatarajia kufunga mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa vyama vya mpira wa miguu wa wanawake vya mikoa ya Tanzania Bara.
 Hafla ya kufunga mafunzo hayo itafanyika kesho (Septemba 26 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
 Mafunzo hayo ya siku tano yalishirikisha viongozi 34 wakiwemo baadhi ya waandishi wa habari na Meneja wa Twiga Stars, na yaliendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Henry Tandau.
 BONIFACE WAMBURA
KNY KATIBU MKUU
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA.

Simba yapata pigo, Ivo, Kiongera kuikosa Yanga Okt 12

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj8__24SqlWkKjcX7F8kwlm9XNcJcmuX00g5LSeJnhkhyvDdgaA_LOv5ObDUcs7DcWxwbUMiMiTANgKbV434hiewe8cAlv0KlOHhyuP0g6sM4YhdkxIkgyI8l30SjnEcyw_ja49lQ9HlEI/s1600/ivo.jpg 
WIKI mbili kabla ya kuvaana na watani zao, Yanga klabu ya Simba imepata pigo baada ya kipa wake namba moja, Ivo Mapunda kuvunjika kidole na hivyo kuwa nje ya dimba kwa wiki nane.
Kwa mujibu wa taarifa za klabu hiyo Ivo amevunjika kidole mazoezini Zanzibar jana asubuhi na anatakiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki nane.
Kuumia huko kunamfanya asiweze kusimama langoni wakati  wa pambano la watani wa jadi la Simba na Yanga la Oktoba 12.
Daktari wa Simba SC Yassin Gembe amenukuliwa akisema Ivo aliumia wakati anachupia mpira katika mazoezi ya asubuhi na kwa bahati mbaya mpira ukamgonga kwenye kidole kidogo cha mwisho mkono wa kulia.
Gembe amesema Ivo alitoka mazoezini baada ya tukio hilo na baadaye akapelekwa hospitali ya Mnazi Mmoja kisiwani humo ambako baada ya vipimo ikagundulika amevunjika sana.
"Si kuvunjika kwa mzaha, amevunjika sana na anatakiwa kupumzika kwa wiki nane, baada ya hapo aanze taratibu… ina maana makadirio ya kurudi tena uwanjani ni hadi baada ya miezi mitatu" – Gembe.
Kuumia kwa Ivo kunatoa nafasi kwa makipa chipukizi Hussein Sharrif  ‘Cassilas’ na Peter Manyika kujibidiisha ili kuziba pengo lake ambapo sasa Ivo anafanya idadi ya wachezaji majeruhi ambao ni tegemeo Simba kufikia wanne baada ya Paul Kiongera anayetakiwa kuwa nje wiki sita, Haroun Chanongo na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’.

Aisha Bui awaandalia mashabiki wake 'Asante' kumpokea

Aisha Bui katika pozi tofauti
NYOTA wa filamu nchini, Aisha Fat'hi  a.k.a Aisha Bui, yupo kwenye maandalizi ya kufyatua kazi mpya baada ya filamu yake ya 'Mshale wa Kifo' kufanya vyema sokoni.
Akizungumza na MICHARAZO, Aisha alisema anashukuru namna mashabiki walivyoipokea filamu yake hiyo ya kwanza kuitengeneza mwenyewe kupitia kampuni ya Bad Girl Entertainment na katika kuonyesha shukrani zake anajiandaa kuwatengenezea filamu nyingine kali zaidi.
Aisha alisema ingawa ni mapema kwa sasa kutaja jina la filamu hiyo, lakini alisema itawashirikisha wasanii kadhaa nyota kama alivyofanya katika 'Mshale wa Kifo' aliowashirikisha kina Mzee Chillo, Gabo na wengine.
"Nipo katika maandalizi ya kutengeneza filamu nyingine mpya, hii kama 'Mshale wa Kifo' itashirikisha pia wakali mbalimbali wa filamu nchini, lengo ni kuwapa burudani mashabiki wangu walioniunga mkono kupitia kazi yangu ya kwanza kuizalisha mwenyewe," alisema Aisha.
Kabla ya kutengeneza filamu yake mwenyewe, alishafanya vema katika filamu za wenzake zikiwamo za 'Saturday Morning', 'The Second Wife', 'Better Days', 'Not Without My Son', 'Continous Love', 'Revenge of Love', 'Mirathi', 'Pain of Love' na 'Crazy Love'.

Mashetani Wekundu kumpigia misele Gerard Pique

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjuyvOqEQPRTd8rb3TwgCrdwrkJv25RIrKO5tVEc69etf1RqMa9oRZknqbCqG35plalZ5O0rf0aHR1cMgKHEd_pd8Lj8yuoEqhsZrMY-HvGZKiXjbbOmdo3n2XiN6O5S24WwaeAbCk-xgKL/s1600/gerard+pique+wallpaper+barca+barcelona+photo+gallery+barcablog+barca+blog+2.jpg
IMEFAHAMIKA kuwa klabu ya Manchester United wana mpango wa kumrejesha Gerard Pique Old Trafford akitokea Barcelona.
Mlinzi huyo aliondoka United mwaka 2008 kwa uhamisho uliogharimu pauni milioni £5 ambapo amekuwa mchezaji wa kutumainiwa Katalunya tangu wakati huo ambapo ameisaidia kutwaa mataji manne ya ligi ya Hispania 'La Liga' mataji mawili ya ligi ya mabingwa Ulaya na mawili ya Copa del Reys.
Hata hivyo nyota huyo wa kimataifa wa Hispania mpaka sasa ameitumikia timu yake michezo mitatu tu huku bosi mpya wa Barcelona Luis Enrique akionekana kupendelea zaidi kumtumia Javier Mascherano na Jeremy Mathieu katika sehemu ya ulinzi.
Kwa mujibu wa gazeti moja la nchini Hispania la AS limearifu kuwa Manchester United inataka kutumia mwanya huo kuweka pendekezo la kutaka kumsajili Pique kurejea Old Trafford, licha ya kwamba mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 27 akiwa ndio kwanza amesaini mkataba wa nyongeza na Barca.
Bosi Louis van Gaal kwasasa analazimika kusaka namna ya kuimarisha eneo la ulinzi katika kikosi chake mwezi Januari wakati huu ambapo United ikiwa imekusanya alama tano tu katika michezo mitano tangu kuanza kwa msimu mpya wa Premier League huku ikiwa tayari imeshatolewa katika kombe la Capital One na MK Dons.

Algeria yajaribu bahati yake AFCON 2017

http://en.starafrica.com/football/files/2014/07/alg%C3%A9rie1.jpgNCHI ya Algeria imeamua kujitosa kuwania uenyeji wa Fainali za Afrika, AFCON 2017 baada ya kukosa nafasi ya uandaaji wa fainali za  2019, 2021 na 2023.
Shirikisho la Soka la Algeria limetangaza kutuma maombi ya kutaka uenyeji wa michuano hizo za 2017. 
Taifa hilo la kaskazini mwa Afrika litachuana na nchi za Ethiopia, Ghana, Kenya, Tanzania, Mozambique, Zimbabwe na Misri katika kugombea nafasi hiyo. 
Libya ilishindwa kuandaa michuano hiyo kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini humo toka uondolewe utawala wa Muamar Gaddafi. 
Mshindi katika kinyang’anyiro hicho anatarajiwa kutangazwa mapema mwakani na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF. 
Cameroon wao walishinda haki za kuandaa michuano hiyo mwaka 2019 wakati Ivory Coast na Guinea wao walipata nafasi ya kuandaa michuano ya mwaka 2021 na 2023.

Arsene Wenger apumua Arsenal wakijiandaa kuivaa Spurs

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhLx4Ctj5fXJAnEPWAnPQLE87dYZzsslg675yLAakU1-WpskYn3CW0mbJ2CIKGeRf5M4Yqi-eVxM6Pyv_R7oLwacXTN6v0ML9tDqP3gR9TEUBNLUbo6FhO2brnwFUrixY0Has-XeGIPRHE/s1600/guar.jpgMENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema anategemea Per Martesacker na Kieran Gibbs kurejea katika kikosi chake katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya mahasimu wao wa kaskazini mwa London Tottenham Hotspurs. 
Majeraha madogo madogo yalipelekea Martersacker na Gibbs kukosa mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Southampton na kupelekea Wenger kuwatumia mabeki wasio wazoefu akiwemo Hector Bellerin na Isaac Hayden. 
Kukosekana kwa Nacho Monreal kunamaanisha Calum Chambers ndio mchezaji pekee katika safu ya ulinzi mwenye uzoefu aliyechezeshwa na Wenger lakini kinda huyo amecheza katika mechi saba pekee za Arsenal toka alipojiunga akitokea Southampton. 
Katika mchezo huo Arsenal walitandikwa nyumbani mabao 2-1 na Southampton lakini Wenger ana uhakika kuwa mabeki wake wazoefu Matersacker na Gibbs watakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi. 
Safu ya ulinzi ya Arsenal ilizidi kupungua baada ya taarifa za Jumatatu kuwa beki wa kimataifa wa Ufaransa Mathieu Debuchy atakosekana dimbani kwa miezi mitatu kufuatia kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu wake wa kushoto.

Ronaldo akaribia rekodi ya Di Stephano Real Madrid

http://assets2.sportsnet.ca/wp-content/uploads/2014/01/ronaldo_cristiano.jpgCRISTIANO Ronaldo alifunga magoli manne katika ushindi wa Real Madrid wa 5-1 dhidi ya Elche katika Ligi Kuu ya Hispania juzi na kuwa 'hat-trick' yake ya 25 kwa Real Madrid.
Ilikuwa ni 'hat-trick' ya pili katika siku tatu baada ya kufunga magoli matatu katika ushindi wa 8-2 dhidi ya Deportivo la Coruna Jumamosi.
Ronaldo ndiye aliyesababisha penalti iliyowapa Elche goli la kuongoza baada ya kuukosa mpira na kumpiga teke Pedro Musquera wakati akijaribu kuokoa kutokea ndani ya boksi la Madrid. "Licha ya kwamba nililalamika kwa refa, ilikuwa ni penalti. Ni lazima niwe mkweli. Alikuja ghafla, lilikuwa ni shambulio ambalo sikulitarajia. Yalikuwa ni maamuzi sahihi ya refa," alisema Ronaldo.
"Nimefunga magoli manne katika mechi moja mara mbili ama tatu. Nina furaha mpira (wa 'hat-trick' nampelekea mwanangu," alisema.
'Hat-trick' hiyo ya 25 inamfanya kubakisha tatu kumfikia Alfredo di Stefano anayeshikilia rekodi ya Real Madrid ya kufunga 'hat-trick' 28. Pia ilikuwa ni ya 21 katika La Liga pekee, moja nyuma ya vinara wanaoshikilia rekodi, Di Stepano na Telmo Zarra, gwiji wa Athletic Bilbao.
Ronaldo tayari msimu huu amefunga magoli 13 katika michuano yote na kufikisha mabao 264 tangu ajiunge na Madrid, hivyo kubakisha magoli 59 kumfikia mshikarekodi wa zama zote klabuni hapo Raul aliyefunga magoli 323. Na kwa kuwa Madrid wana mechi 56 zilizobaki msimu huu, huenda akaivunja rekodi hiyo 2014-15. 

Hammer Q ana Kibakuli cha Mduara

MUIMBAJI mahiri wa muziki wa taarab, Hammer Q ameachiwa wimbo wake binafsi uitwao 'Kibakuli', wakati Rich Mavoko akiwaonyesha mashabiki wake video ya wimbo wake mpya uitwao 'Pacha Wangu'.
Hammer Q aliyewahi kutamba kwenye muziki wa kizazi kipya na wimbo wa 'Lady' kabla ya kuhamia kwenye taarab, ameachiwa wimbo huo uliopo kwenye mduara.
Wimbo huo umetengenezwa na mtayarishaji aitwae Anta Nation na  umeanza kutamba kwenye redio na mitandao ya kijamii.
Katika hatua nyingine Staa wa Roho Yangu, Rich Mavoko ameonjesha kionjo cha video yake mpya ya Pacha Wangu ambayo anatarajia kuachia siku ya leo pamoja na ngoma nyingine mpya.

Mbwa Mwitu wa Kajala azinduliwa, Lamata alalamika

BAADHI ya picha za matukio katika shughuli hiyo ya usiku wa jana
FILAMU ya Mbwa Mwitu ya msanii Kajala Masanja imezinduliwa kwa kishindo usiku wa jana kwenye ukumbi wa Sinema wa Mlimani City, huku mtunzi na muongozaji wake, Leah Richard 'Lamata' akilalamika ukiritimba unaofanywa na wasimamizi wa tasnia ya filamu nchini.
Lamata aliidokeza MICHARAZO mapema kuwa, kabla ya kuzindua filamu hiyo iliyotengenezwa na Kay Entertainment wakikumbana na vikwazo wakipigwa namna simulizi la filamu hiyo ya dakika 15 iliyogusa matukio ya kweli yaliyoikumba jamii hivi karibuni kutoka makundi ya wahalifu yaitwayo 'Mbwa Mwitu', 'Boda kwa Boda', 'Bad Face' na 'Watoto wa Mbwa'.
"Hii inkatisha tamaa lengo letu kuifundisha jamii juu ya kuepuka uhalifu kwani mwisho wake huwa siyo mwema, lakini 'mabosi' wanaosimamia fani hii wanadhani sisi tunaelimisha vibaya katika matukio yaliyopo ndani ya filamu hii ya 'Mbwa Mwitu'.
Lamata alisema bado wataendelea kutunga filamu zinazoigusa jamii sambamba na kuielimisha, kuionya na kuiburudisha kama sifa za fasihi ilivyo.
Ndani ya filamu hiyo wamo Kajala, Hemed Suleiman, Mama Kawele, Quick Racca na Mwinjuma Muumin 'Kocha wa Dunia'.
Nyota mbali walihudhuria onyesho hilo wakiwamo waigizaji Rich Richie, mtoto wa Kajala, Paula, Sandra, Odama na wengineo kibao waliompiga tafu Kajala.