STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 26, 2015

YANGA KUANIKA SILAHA ZAKE MBELE YA WAZIRI PINDA



http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/02/Mizengo-Pinda1.jpgSTRAIKA Donald Ngoma wa FC Platinum ya Zimbabwe alitarajiwa kutua nchini jioni ya leo na ilitarajiwa jioni ya kesho angeishuhudia Yanga inayotaka kumsajili ikitambulisha nyota wake wapya katika pambano dhidi ya Sc Villa ya Uganda.
Hata hivyo mchezaji huyo imeshindikana kutua leo, lakini hakuna kilichoharibika kwani Yanga itatambulisha nyota wake wote mbele ya Waziri Mkuu na Mtangaza Nia ya Urais, Mhe. Mizengo Pinda. Waziri Pinda atakuwepo katika pambano hilo ili kubariki silaha hizo mpya za Jangwani wakati wa mchezo huo maalum wa kuchangisha fedha za Ujenzi wa Majengo ya Watoto Wanaoisha katika Mazingira Magumu.
MKurugenzi wa asasi wa Nyumbani Kwanza, Mossy Magere aliiambia MICHARAZO MITUPU kuwa, Yanga itavaana na SC Villa ambapo pia kutakuwa na burudani ya kutosha kwa watakaohudhuria.
Mossy alisema kuwa, Waziri Pinda ndiye mgeni rasmi katika pambano hilo ambalo Yanga watalitumia kutambulisha nyota wake wapya na kusindikizwa na burudani ya muziki toka kwa kundi la Yamoto Band.
"Maandalizi yamekamilika na kwamba wageni mbalimbali tumewaalika, ila Waziri Pinda ndiye atakayekuwa mgeni rasmi na atabariki kikosi hicho cha kocha Hans Pluijm," alisema Mosi.
Mosi alisema kuwa SC Villa walitua juzi jioni wakiwa na kikosi cha wachezaji 18 na viongozi watano na kwamba jana walipasha misuli kwenye Uwanja wa Taifa kabla ya leo kuivaa Yanga.
Yanga ambao imetoka kuichapa Friends Rangers kwa mabao 3-2 katika mechi ya mazoezi, inauchukuliwa kwa uzito mkubwa mchezo huo wa leo kwani ni sehemu ya maandalizi ya ushiriki wao wa michuano ya Kagame na kocha atataka kupima uwezo wa wachezaji wao mbele ya Villa.
Baadhi ya wachezaji wapya wa Yanga ambao watakuwa majaribuni ni Malimi Busungu, Geofrey Mwashiuya na kipa Benedict Tinocco kwani Mwinyi Haji Ngwali na Deus Kaseke wapo kambi ya Taifa Stars kujiandaa na pambano la marudiano la kuwania Chan dhidi ya Uganda The Cranes.
Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha alinukuliwa juzi kuwa, huenda akawashtukiza mashabiki wa klabu hiyo katika mchezo huo wa kesho, bila kufafanua lakini imebainika ni kwamba Donald Ngoma alipangwa kuwepo uwanjani kuwashuhudia wenzake kwani angetua nchini ili kumalizana na klabu hiyo.

Jennifer Mgendi kufanya tamasha kubwa Dar Jumapili

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj7CxGiIU1N594esKNg1xe0mepyXDXaYznz92rl6kyK9TGgAbFQXUuEIonXEf3N5HWzU5AqbhmndSU2qveH5Qc0NqREOL9nlP95F4KqStJZMwq-XxH4wfAbnkufcoKfvtHZZh7_jyqffWUi/s1600/MGENDI.JPG
Jennifer Mgendi
MUIMBAJI nyota wa muziki wa Injili ambaye pia ni muigizaji na mtayarishaji wa filamu nchini, Jennifer Mgendi anajiandaa kuifanya tamasha kubwa kwa ajili ya Kumshukuru Mungu kwa kuweza kudumu kwenye fani hizo kwa miaka 20 sasa.
Jennifer alidokeza kuwa Tamasha hilo lililopewa jina la 'Tamasha la Miaka 20 ya Shukrani litafanyika kwenye Kanisa la DCT lililopo Tabata Shule karibu na Kituo cha Polisi Tabata siku ya Jumapili Juni 28 na kusindikizwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa Injili nchini.
"Natarajia kufanya tamasha la Shukran ya Miaka 2o, litakalofanyika Juni 28 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Askofu Mkuu wa TIG, Dk Barnabas Mtokambali na waimbaji mbalimbali watanisindikiza akiwamo Bahati Bukuku, Bonny Mwaitege, Cosmas Chidumule, Ency Mwalukasa, Mchungaji Charles Jangalason na wengineo," alisema Jennifer.
Jennifer alisema ana haki ya kumshukuru Mungu kwa kumwezesha kumpa kipaji na kumwezesha kudumu katika huduma ya uimbaji kwa miaka hiyo yote 20.
Muimbaji huyo kwa sasa anatamba na albamu nane za muziki wa Injili tangu alipojitosa kwenye fani hiyo mwaka 1995 na katika tamasha hilo ataizundua video ya albamu yake inayotamba sasa ya 'WEMA NI AKIBA'.
Mbali na kwenye muziki, Jennifer pia anatamba kwenye filamu akiwa anakimbiza kwa sasa na kazi zake kadhaa ukiwamo 'Teke la Mama', 'Chai Moto', 'Pigo la Faraja', 'Mama Mkwe' na nyinginezo ambazo zimemfanya kuwa matawi ya juu licha ya kwamba hana makeke kama wasanii wengine.

Unyama! Watu 17 wauwawa hotelini

UNYAMA dhidi ya wanadamu umeendelea tena baa da ya Watu wenye silaha wameshambulia hoteli moja ya kitalii iliyoko kwenye pwani ya Tunisia na kuwauwa watu 27.
Maafisa wa serikali ya Tunisia wamesema kuwa mmoja wa washambuliaji hao aliuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa ulinzi na kuwa waliosalia bado wanasakwa na polisi.
Shambulio hilo lilitokea katika mji wa Sousse, ambao huwavutia maelfu ya watalii kutoka bara Ulaya na Afrika ya Kaskazini.
Hili lilikuwa shambulizi la pili dhidi ya hoteli ya watalii nchini Tunisia katika kipindi cha miezi michache iliyopita.
Inaaminika kuwa washambuliaji hao waliwavamia watalii ufukweni.
Mnamo mwezi Machi mwaka huu, wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki waliwauawa zaidi ya watu 26 katika makavazi ya Bardo, iliyoko katika mji mkuu wa nchi hiyo Tunis.
Makavazi hayo ya Bardo hilo lilikuwa maarufu sana kwa watalii.
October mwaka wa 2013, mlipuaji wa kujitoa, alijilipua nje ya nyumba moja mjini Sousse, baada ya maafisa wa polisi kutibua jaribio lake la kutaka kuingia ndani na kuishambulia.
BBC

Simba waiwahi TFF kuhusu makocha wa makipa

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi-ErV4LDze29At9zLOJ5-K7zmESxzpny61EoTZ3Oj0BwcGnaHSSYJesvEuGbG8W3_LmcXp-5IKsJPPyMBUZZ6N0_rCe840K_0q4lFxI8OEaEgFOGs4iLDRaMuGeQX20S4EGDP4_CFZ-_A/s1600/Simba+logo+white.jpg
SIMBA wajanja sana, wakati Shirikisho la Mpira wa Mpira wa Miguu nchini (TFF) likitoa agizo na kuvioomba klabu zote zinavyoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kuwasilisha jina la kocha wa magolikipa kufikia jumatatu ya tarehe 29 Juni, 2015 katika ofisi za TFF, tayari klabu hiyo imeshamleta kocha wake kutoka Kenya, Abdul Salim.
TFF imeandaa kozi ya magolikipa hivyo inahitaji kupata jina la kila kocha wa magolikipa ili kuweza kushiriki kwenye kozi hiyo itakayoanza tarehe 13 - 17 Julai, 2015 jijini Dar es Salaam kwa mpango huo Simba itakuwa imeikatia denge TFF mapema. Coastal Union nayo ilifanya yao mapema juzi baada ya kumsainisha kocha wa zamani wa KCC ya Uganda, Lumu Fred ili kuwanoa makipa wa timu hiyo itakayokuwa chini ya Kocha Mkuu, Jackson Mayanja pia wa Uganda aliyekuwa akiinoa Kagera Sugar katika msimu uliopita.

SITA ZAPANDA DARAJA, MADINI ARUSHA NAO WAMO!

KLABU za Abajalo FC ya Tabora, Alliance FC (Mwanza), Changanyikeni Rangers FC (Dar es Salaam), Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya), Madini SC (Arusha), na Sabasaba United FC (Morogoro) ndizo timu zilizopanda kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu wa 2015/2016.
Timu hizo zimepanda daraja baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) iliyomalizika hivi karibuni kwenye vituo vya Lindi, Manyara na Rukwa na kushirikisha jumla ya timu 27.

SDL inayoshirikisha timu 24 zilizogawanywa katika makundi manne inatarajia kuanza kutimua vumbi Oktoba 17 mwaka huu. Ligi hiyo itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini, na timu itakayoongoza kundi ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa msimu wa 2016/2017.

Kundi A lina timu za Abajalo FC (Tabora), Green Warriors (Dar es Salaam), Milambo FC (Tabora), Mvuvumwa FC (Kigoma), Singida United (Singida) na Transit Camp (Dar es Salaam).

Kundi B lina timu za AFC (Arusha), Alliance FC (Mwanza), Bulyanhulu FC (Shinyanga), JKT Rwamkoma FC (Mara), Madini SC (Arusha) na Pamba SC (Mwanza).

Wakati kundi C lina timu za Abajalo FC (Dar es Salaam), Changanyikeni Rangers FC (Dar es Salaam), Cosmopolitan (Dar es Salaam), Kariakoo FC (Lindi), Mshikamano FC (Dar es Salaam) na Villa Squad (Dar es Salaam).

African Wanderers ya Iringa, Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya), Mkamba Rangers (Morogoro), Sabasaba United FC (Morogoro), Town Small Boys (Ruvuma) na Wenda FC ya Mbeya ndizo zinazounda kundi D.

Dirisha la usajili wa wachezaji limeshafunguliwa tangu Juni 15 mwaka huu, na litafungwa Agosti 6 mwaka huu.

TFF yavichimba mkwara vyama vya soka mikoani

KUFUATIA pendekezo la sekretariet ya TFF ambalo baadae lilipitishwa na Mkutano Mkuu wa TFF kila mkoa unatakiwa kuwa na kituo chake cha kulea na kukuza vipaji vya mpira wa vijana umri kuanzia miaka 8-17.

Kwa mikoa ambayo tayari ina kituo ambacho inakiendesha yenyewe TFF inaonba ipatiwe taarifa hiyo ikiwa ni pamoja na kufahamishwa jina la kituo, jina la mwalimu na sifa zake na utaratibu wa mafunzo.

Kwa mikoa ambayo haina kituo TFF inagiza mikoa hiyo kuingia ubia na kituo kimoja ambacho tayari kina program ya kukuza na kuendeleza vipaji ili kijulikane kuwa ni kituo maalum cha mkoa husika.

Katika hilo TFF inaagiza kamati ya utendaji ya mkoa husika iandae muhtasari wa kikao cha utendaji cha chama cha mkoa wa kupitisha maamuzi hayo, MoU (makubaliano rasmi) yasainiwe kati ya chama cha mkoa na kituo husika na hati hiyo nakala yake iletwe TFF.

MoU hiyo ionyeshe majukumu ya chama cha mpira cha mkoa kama kutoa vifaa, kutoa mwalimu, usimamizi nk na pia kuonyesha majukumu ya mwenye kituo kama kutoa uwanja,ulinzi nk. MoU itaonyesha pia nani atafaidika na vipaji vitakavyoibuliwa kati ya mzazi,kituo na chama cha mkoa.

TFF itaandaa MoU ya mfano kwa ajili ya vyama vyote vya mikoa na ingependa kufikia tarehe 31/Desemba/2015 kila mkoa uwe umetekeleza jambo hilo
.

Stars ya Kwanza yaanza kujifua jijini Dar

Kocha wa Stars, Boniface Mkwasa (kulia)
KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimeanza mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa Boko Veterani kujiandaa na mchezo wa marudaino kuwania kufuzu kwa CHAN dhidi ya uganda mwishoni mwa wiki ijayo.

Stars inayonolewa na makocha wazawa, Charles Mkwasa na msaidizi wake Hemded Morocco, itakua ikifanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja huo wa Boko Veterani, huku timu ikiweka kambi yake katika hoteli ya Kiromo mjini Bagamoyo.

Wachezaji wote walioitwa wameripoti kambini tangu jana na leo wamefanya mazoezi asubuhi isipokua Aggrey Morris ambaye ni majeruhi nafasi yake imekuchukuliwa na Vicent Andrew (Mtibwa Sugar) na Jonas Mkude aliyekwenda kufanya majaribio Afrika Kusini nafasi yake ikizibwa na Mudathir Yahya (Azam FC).

TFF yafunga kozi ya Makocha wa Vijana

Viongozi wa TFF, Rais Jamal Malinzi na Katibu Mkuu, Celestine Mwesigwa
SHIRIKISHO la Soka Nchini (TFF) leo limefungua kozi ya makocha wa mpira wa miguu kwa watoto na vijana kwa nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha vijana wengi wanapata nafasi ya kufundishwa mpira na kuucheza mpira kuanzia katika umri mdogo.

Akifungua kozi hiyo, Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine amesema ili nchi/Taifa lifanikiwe katika soka ni lazima kuwekeza katika mpira wa watoto na vijana ambao makocha hao ni sehemu ya uwekezaji huo.

“Tumekua na mashindano ya Taifa U-13, kikosi cha timu ya Taifa ya U-15 ambayo inashirikisha vijana wadogo, vijana hao wanapaswa kupata malezi na mafunzo yenu waalimu ili wafikiapo kuchezea timu za Taifa wawe wamekua kwenye msingi bora wa kuujua mpira wa miguu” alisema Mwesigwa.

Naye mkufunzi wa FIFA wa kozi hiyo ya makocha kutoka nchini Ujerumani, Eric Muller amesema hata ujerumani imefanikiwa baada ya kuwekeza katika soka la vijana, mwaka 2000 kwenye fainali za Euro nchi yao ilishika nafasi ya mwisho katika msimamo kundi lao kwa kupata poniti moja, lakini uwekezaji walioufanya kwenye soka la watoto na vijana umewapelekea kutwaa Ubingwa wa Dunia mwaka 2014.

Washiriki wa kozi hiyo ni makocha wa timu za vijana za mikoa yoye Tanzania, ambao watashirki na timu zao za mikoa katika michuano ya Copa Coca Cola mwaka huu.

Kozi hiyo ya makocha wa timu za watoto/vijana inayoendeshwa na wakufunzi wa FIFA, Ulric Mathews kutoka shelisheli na Eric Muller kutoka nchini Ujerumani itamalizika jumatatu tarehe 29 Juni, 2015
.

Kazi imeanza, makocha Simba watua

Alianza huyu wa Kenya kwanza
Mwishowe wakakutana wote kwa pamoja
KLABU ya Simba imeonyesha haina utani baada ya makocha wake wapya Dylan Kerr kutoka Uingereza na Abdul Salim kutoka Kenya atakayewanoa makipa kutua nchini mchana huu wakitokea makwao.
Makocha hao wamelamba shavu la kuinoa Simba baada ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo, Goran Kopunovic kushindwa kuelewana na uongozi wa Rais Evans Aveva.
Kocha wa kwanza kutua nchini alikuwa Mkenya aliyewahi kuzinoa timu mbalimbali ikiwamo Gor Mahia na AFC Leopard ambaye alitua majira ya saa nane mchana kabla ya Kerry kutua saa 10 kwa Ndege ya Shirika la Emirates.
Makocha hao wametua tayari kuanza yao katika klabu hiyo ambayo kwa miaka mitatu sasa haijaonja taji la Ligi Kuu, huku ikiwa imebadilisha makocha wasiopungua watano tangu walipotwaa taji la mwisho msimu wa 2011-2012 ikiwa chini ya Cirkovic Milovan aliyefurshwa baadaye.
Kikosi cha wachezaji wa Simba kwa sasa wanajifua kwenye Gym ya Chang'ombe kabla ya kuanza rasmi mazoezi yao Julai Mosi ambapo Rais Aveva alidokeza kuwa itakuwa visiwani Zanzibar kwa muda wa majuma sita.
Hata hivyo Simba itaanza kambi hiyo bila baadhi ya nyota wake kadhaa wakiwamo wale waliopo katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars inayojiandaa kuifuata Uganda the Cranes katika pambano la marudiano la kuwania fainali za CHAN-2016 zitakazofanyika Rwanda.
Wengine ambao hawatakuwapo ni Jonas Mkude aliyetimkia Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Afrika Kusini, huku Okwi akiwa kwao kwa ajili ya Fungate ya Arusi yao anayofunga kesho kwao Uganda na Raphael Kwireza akiwa amepewa mapumziko ya mwezi mmoja kusikilia majereha yake yanayomtibulia kukipiga Msimbazi licha ya kuwa na mkataba wa miaka miwili unaomalizika mwakani.