KLABU za Abajalo
FC ya Tabora, Alliance FC (Mwanza), Changanyikeni Rangers FC (Dar es
Salaam), Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya), Madini SC (Arusha), na Sabasaba
United FC (Morogoro) ndizo timu zilizopanda kucheza Ligi Daraja la Pili
(SDL) msimu wa 2015/2016.
Timu hizo zimepanda daraja baada ya
kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL)
iliyomalizika hivi karibuni kwenye vituo vya Lindi, Manyara na Rukwa na
kushirikisha jumla ya timu 27.
SDL inayoshirikisha timu 24
zilizogawanywa katika makundi manne inatarajia kuanza kutimua vumbi
Oktoba 17 mwaka huu. Ligi hiyo itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na
ugenini, na timu itakayoongoza kundi ndiyo itakayopanda daraja kucheza
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa msimu wa 2016/2017.
Kundi A lina
timu za Abajalo FC (Tabora), Green Warriors (Dar es Salaam), Milambo FC
(Tabora), Mvuvumwa FC (Kigoma), Singida United (Singida) na Transit Camp
(Dar es Salaam).
Kundi B lina timu za AFC (Arusha), Alliance FC (Mwanza),
Bulyanhulu FC (Shinyanga), JKT Rwamkoma FC (Mara), Madini SC (Arusha) na
Pamba SC (Mwanza).
Wakati kundi C lina timu za Abajalo FC (Dar es
Salaam), Changanyikeni Rangers FC (Dar es Salaam), Cosmopolitan (Dar es
Salaam), Kariakoo FC (Lindi), Mshikamano FC (Dar es Salaam) na Villa
Squad (Dar es Salaam).
African Wanderers ya Iringa, Coca-Cola
Kwanza FC (Mbeya), Mkamba Rangers (Morogoro), Sabasaba United FC
(Morogoro), Town Small Boys (Ruvuma) na Wenda FC ya Mbeya ndizo
zinazounda kundi D.
Dirisha la usajili wa wachezaji limeshafunguliwa tangu Juni 15 mwaka huu, na litafungwa Agosti 6 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment