Mchezaji na Kepteni wa zamani wa Timu ya
Taifa Stars, Jella Mtagwa (kushoto) akipokea cheti cha nyumba
aliyokabidhiwa na SHIWATA na eneo la robo ekari ambalo anatarajia kujenga
nyumba kubwa
Mwanachama huyu wa SHIWATA kulia ameamua kujijengea nyumba yake pole pole hapa akikabidhiwa cheti chake
Mmoja wa wanachama wa SHIWATA,
Emmanuel Ntumbii na mkewe wakipokea cheti cha kumilikishwa nyumba yake
akishuhudiwa na wanachama wenzake.
Mwandishi wa Habari, Josephine Joseph
akionesha cheti alichokabidhiwa na SHIWATA mbele ya nyumba yake katika
sherehe ya kukabidhi nyumba za wasanii,Mkuranga.
Mkuu wa wilaya mstaafu, Bw. Henry
Clemence akizungumza katika sherehe ya kukabidhi nyumba 38 za wasanii wa
Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) katika kijiji cha Mwanzega,
Mkuanga.
BAADA ya
kukabidhi nyumba kwa wanachama 38, SHIWATA inatoa shukurani kwa viongozi wa
kijiji cha Mwanzega Kata ya Mbezi, Tarafa ya Shungubweni,wanavijiji pamoja na
viongozi wa wilaya ya Mkuranga akiwepo Mkuu wa wilaya, Mercy Silla kwa
kufanisha sherehe ya ugawaji nyumba na vyeti.
Wanachama
zaidi ya 70 wamejitokeza kuchangia ujenzi wa nyumba ili wakabidhiwe Desemba 28,
2013 katika sherehe nyingine ya kukabidhi nyumba ambayo inatarajiwa kuhudhuriwa
na viongozi mbalimbali ambao waliomba udhuru sherehe ya awali.
SHIWATA
inawahimiza wanachama wake wasifanye mzaha na kudharau mpango wa kuchangia
ujenzi kwani utawanufaish na kuwamilikisha nyumba zao wenyewe kwa gharama
nafuu.
Mtandao wa
wasanii unatoa bure viwanja baada ya mwanachama kulipa gharama zote za kujiunga
uanachama ambaye ataruhusiwa kujenga mwenyewe au kuchangia ujenzi wa nyumba kwa
pamoja.
SHIWATA inakusudia kujenga Shule ya Msingi, Sekondari
na vyuo vya fani za utamaduni, Uandishi wa Habari na michezo mbalimbali ikiwemo
soka kwa malengo ya kupata wachezaji bora ambao watanyanyua viwango vya michezo
hiyo ndani na nje ya nchi ili kuwapatia vipato zaidi.
Pia
inawahitaji wasanii, wanamichezo, wanahabari wenye vipaji na elimu ya juu
katika fani zao wajiunge na SHIWATA ili waweze kuwa walimu wa sanaa na michezo
mbalimbali ambayo itaanza kufundishwa kutoka ngazi ya Shule ya Msingi,
Sekondari hadi Chuo katika kijiji cha Mwanzega.
Shule ya
msingi itakapoanzishwa itatoa kipaumbele kwa masomo ya sanaa na michezo ili
kupata wasanii na wanamichezo bora katika taifa letu.
SHIWATA pia
inatarajia kujenga viwanja vya michezo, kumbi za Maonesho na Studio za
kurekodia muziki na filamu zenye ubora ambazo zitauzwa ndani na nje ya nchi.