STRIKA
USILIKOSE
Friday, June 3, 2016
Ngeleja wenzake wapewa kifyagio na Malinzi
Mhe. Ngeleja |
Malinzi |
Rais huyo wa TFF amepongeza uongozi wa timu hiyo uliochaguliwa mjini Dodoma, ambapo Ngeleja alitwaa kiti akimrithi Idd Azan ambaye alishindwa kurudi bungeni katika Uchaguzi Mkuu wa Taifa wa 2015.
Mbali na Ngeleja, wengine waliopewa kifyagio hicho na Malinzi ni Makamu Mwenyekiti, Esther Matiko; Meneja wa Klabu, John Kadutu pamoja Wajumbe Neema Mgaya, Faida Bakari, Cosato Chumi, Anna Lupembe na Grace Kihwelu.Malinzi amewatakia kila la kheri Bunge Sports Club na kuwaahidi ushirikiano kutoka TFF katika kuendeleza klabu yao na michezo kwa ujumla nchini.
Kwa Buku 5 tu inaiona Stars, VIP nako bwerere Taifa
MSHINDWE wenyewe. Viingilio vya kuliona pambano la kuwania kwenda kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Mafarao wa Misri zimewekwa hadharani.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio hivyo, ambapo kile cha bei ya chini kabisa ni buku tano tu. (Sh 5,000) wakati cha juu kikiwa ni Sh. 10,000. Mnataka nini tena?!
TFF ni kama kimesikia kilio cha mashabiki wa soka, kwa kutangaza viingilio hivyo katika mchezo huo wa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mwanangu toroka uje kwa sababu tiketi zimeanza kuuzwa mitaa mbalimbali ya jiji hilo.
TFF imesema watakaolipa Buku 5 watakaa mzunguko wa viti vya rangi ya Chungwa, Kijani na Bluu, wakati wanene wanaotaka kukaa kibosibosi yaani VIP B na C wenyewe watatoboka kiduchu kwa Mwekundu mmoja (Sh. 10,000).
Sasa unajua tiketi zenyewe zinapatikana wapi, wala usikonde ukienda Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam utapata, pale Ukumbi wa Burudani Mbagala Dar Live, Vituo cha mafuta cha Oilcom - Ubungo na Buguruni (Buguruni Shell) na Ofisi za Ukumbi wa burudani Bilicanas, nako utapata.
Halafu hata kesho Jumamosi Juni 4, 2016 tiketi zitauzwa kwenye vituo hivyo na vingine vya Mwenge, Mnazi Mmoja, Makumbusho, Chang’ombe na Mgahawa wa Brake Point ulioko mkabala makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Unangoja nini mwanangu, changamka bhana!
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio hivyo, ambapo kile cha bei ya chini kabisa ni buku tano tu. (Sh 5,000) wakati cha juu kikiwa ni Sh. 10,000. Mnataka nini tena?!
TFF ni kama kimesikia kilio cha mashabiki wa soka, kwa kutangaza viingilio hivyo katika mchezo huo wa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mwanangu toroka uje kwa sababu tiketi zimeanza kuuzwa mitaa mbalimbali ya jiji hilo.
TFF imesema watakaolipa Buku 5 watakaa mzunguko wa viti vya rangi ya Chungwa, Kijani na Bluu, wakati wanene wanaotaka kukaa kibosibosi yaani VIP B na C wenyewe watatoboka kiduchu kwa Mwekundu mmoja (Sh. 10,000).
Sasa unajua tiketi zenyewe zinapatikana wapi, wala usikonde ukienda Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam utapata, pale Ukumbi wa Burudani Mbagala Dar Live, Vituo cha mafuta cha Oilcom - Ubungo na Buguruni (Buguruni Shell) na Ofisi za Ukumbi wa burudani Bilicanas, nako utapata.
Halafu hata kesho Jumamosi Juni 4, 2016 tiketi zitauzwa kwenye vituo hivyo na vingine vya Mwenge, Mnazi Mmoja, Makumbusho, Chang’ombe na Mgahawa wa Brake Point ulioko mkabala makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Unangoja nini mwanangu, changamka bhana!
Maskini Muhammad Ali! Alazwa tena hospitalini
Muhammad Ali katika moja ya mapambano yake akimuadhibu mpinzani wake aliyelala sakafuni. |
Bondia huyo nyota mwenye umri wa miaka 74 aliyekonga nyoyo za wapenzi wa ndondi kote duniani anasemekana kuwa katika hali wastani alipolazwa hospitalini.
Hata hivyo familia yake ilipendekeza alazwe hospitali kama tahadhari kwa sababu mbali na maambukizi hayo Ali anaugua kiharusi.
Bondia huyo alipatikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka wa 1984 baada ya kustaafu mchezo huo wa ngumi za kulipwa.
Mara ya mwisho bondia huyo mkongwe alipolazwa hospitalini ilikuwa ni Januari mwaka uliopita baada ya kupatwa maambukizi ya njia ya mkojo.
Msemaji wa familia yake hata hivyo hakuwaambia wanahabari alikolazwa wala alilazwa lini.
Chanzo: BBC Swahili
Mara ya mwisho bondia huyo mkongwe alipolazwa hospitalini ilikuwa ni Januari mwaka uliopita baada ya kupatwa maambukizi ya njia ya mkojo.
Msemaji wa familia yake hata hivyo hakuwaambia wanahabari alikolazwa wala alilazwa lini.
Chanzo: BBC Swahili
Mkwasa aahidi raha Taifa, tunasubiri nini twendeni uwanjani
Kocha wa Stars, Boniface Mkwasa |
TWENDENI Taifa kesho Jumamosi, kwani Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa 'Master' ameahidi kuifanyizia Mafarao wa Misri katika pambano lao la kuwania Afcon 2017.
Stars kesho inashuka dimbani kucheza na Misri ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 3-0 iliyopata kwenye mchezo wa awali uliochezwa mji wa Alexandria, katika ufunguzi wa mechi za Kundi G.
Stars inahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kufuzu AFCON ya mwakani wakati Misri wao sare itawafanya wafikishe pointi nane ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine kwenye kundi lao.
Endapo
Tanzania itashinda mchezo huo itafikisha pointi nne kwani hadi sasa ina
pointi moja baada ya sare ya 0-0 na Nigeria nyumbani huku ikibakisha mchezo wa
marudiano na Nigeria ugenini baadaye Septemba mwaka huu..
Kundi hili
baada ya kujitoa kwa Chad limebaki na timu tatu ambazo ni Misri wenye pointi
saba, Nigeria pointi nne na Tanzania yenye inashika mkia ikiwa na pointi moja lakini Misri na Nigeria
zimebakiza mchezo mmoja mmoja, wakati Tanzania ina faida ya mechi mbilim huu wa
leo na mwingine ni dhidi ya Nigeria utakaochezwa Septemba.
Akizungumza
na Wanahabari Kocha Mkwasa alisema
mchezo wa keshoni mgumu kwani ni sawa na
fainali hivyo wanahitaji kushinda ili kujiweka pazuri kwani Misri wanakuja
wakihitaji sare.
“Wachezaji
wako vizuri, wako kwenye morali nzuri na tumefanya mazoezi na
wachezaji wote 26 na mimi nimefanya marekebisho kwa makosa yaliyojitokeza
kwenye mchezo dhidi ya Kenya na kinachosubiriwa ni dakika 90 tu”, alisema
Mkwasa.
Pia Mkwasa
alisema anatambua Misri ni timu nzuri kwani waliifunga Tanzania mabao 3-0 kwao
na anajua wanakuja kucheza mfumo wa kujilinda kuliko kushambulia kama ilivyo
desturi kwa timu za kiarabu lakini wao wamejiandaa kushambulia.
“Tuna deni
kubwa kwa watanzania hivyo tunajua tunatakiwa kupata matokeo mazuri ili kuwapa
faraja na kufufua matumaini ya kwenda AFCON hivyo tutashambulia sana”, alisema
Mkwasa
Mkwasa
aliwashukia watu wanaojiita wachambuzi wa soka akisema wamekuwa wakiwavunja
moyo wachezaji na kuwataka waangalie namna wanavyofanya uchambuzi kwani
wanawakatisha tamaa wachezaji na kuwaasa uchambuzi mzuri ni ule ambao unafanywa
baada ya mchezo.
Manji amkimbiza Alloyce Komba Kamati ya Uchaguzi ya TFF
Alloyce Komba |
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji |
MWENYEKITI
wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la
Soka Tanzania, (TFF), Aloyce Komba, amejiondoa kwenye mchakato wa uchaguzi wa
klabu Yanga uliopangwa kufanyika Juni 25 , mwaka huu.
Hatua hii
imekuja baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji kumtuhumu kumhujumu hivyo
anakaa pembeni kupisha uchunguzi
Akizungumza
na wanahabari leo Ijumaa, Komba alisema Manji anasema nahusika kupanga
mikakati ya kupewa rushwa ili akate jina
lake na tuhuma hizi kwake ni nzito ukizingatia taaluma yake ya sheria.
“Manji ananituhumu
mimi kupanga mikakati ya kupewa rushwa ili nikate jina lake, tuhuma hizi kwangu
ni nzito ukizingatia taaluma yangu ya sheria, sitaki kuwa chanzo cha mgogoro
Yanga”, alisema Komba
Pia Komba
alisema wanasheria nguli Said El Maamry, Alex Mgongolwa, Mapande na baadhi ya wabunge ni watu
anaowaheshimu na wamemshauri juu ya suala hili hivyo kwa busara ameamua kukaa
pembeni uchaguzi ufanyike.
“Sauti zinazosemwa sizitambui, sizijui, halafu
najiuliza wanapanga kwa manufaa ya nani? Kwanini Manji katishika kuchukua fomu TFF wakati ameonyesha uwezo mkubwa wa
kuongoza Yanga?”, alihoji Komba.
Komba
alisema alitegemea Manji angemrahisishia kazi lakini matokeo yake anachafuka
kwa vitu ambavyo si vya kweli.
Mchakato wa
uchaguzi TFF unaendelea chini ya Makamu Mwenyekiti Wakili Domina Mideli, ingawa uongozi wa Yanga nao unaendesha zoezi lao makao makuu kabla ya kufanya uchaguzi wao Juni 11.
UEFA Euro Cup 2016 itakuwa tamu si mchezo
Rashford |
Ronaldo atafanya nini safari hii huko Ufaransa |
MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Ulaya 'UEFA Euro 2016' itaanza wiki ijayo nchini Ufaransa kwa kushuhudiwa nyota wa nchi mbalimbali barani humo wakionyeshana kazi mpaka Julai 10 atakapopatikana bingwa wake.
Hispania ndio watetezi wa taji hilo ikilishikilia kwa mihula miwili mfululizo tangu mwaka 2008 na kutetea mwaka 2012.
Michuano hiyo itafanyika huku kukiwa na rekodi kadhaa ambazo zinahitajiwa kuvunjwa ikiwamo ya mchezaji alitefunga mabao mengi katika fainali moja, iliyowekwa na aliyekuwa nyota wa Ufaransa, Michel Platini mwaka 1984.
Katika michuano hiyo Platini aliyekuwa Rais wa Uefa kabla ya kufungiwa na FIFA kwa tuhuma za kifisadi, alifunga mabao 9, huku pia akitupia hat-trick mbili ikiwa ni rekodi tena zilizofululiza, mbali na bao la mapema la michuano la dakika 18.
Unajua kuwa ni nchi mbili tu za Ujerumani na Hispania ndizo zilizotwaa mara nyingi, zikifanya hivyo mara tatu kila moja, hivyo ni wakati wao wa kuzidiana ujanja au kuzubaa na kukutwa na Ufaransa inayowafukizia ikitwaa mara mbili tangu michuano ilipoasisiwa mwaka 1960.
Pia michuano hiyo ilimpa ujiko Cristiano Ronaldo mwaka 2004 alipokuwa mchezaji mwenye umri mdogo kucheza fainali akifanya hivyo mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 19 na siku 150.
Kwa kifupi kina Marcus Rashford na makinda wenzake wanapaswa kufanya mambo ili kufikia rekodi mbalimbali ambazo zimedumu kwa miaka mingi bila kuvunjwa.
Samatta akimaliza kazi Taifa, kupewa kiwanja chake Mkuranga
Na Rahma Junior
MBWANA Samatta kesho Jumamosi ataiongoza Taifa Stars kuvaana na Misri, kwenye pambano la kuwania kwenda Gabon katika fainali za Afcon 2017, lakini Jumapili atakuwa katika sherehe moja kamambe.
Nahodha huyo wa Stars, atakuwa anakabidhiwa kiwanja cha ekari tano kilichopo kijiji cha wasanii
Mwanzega, Mkuranga.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii
Tanzania (SHIWATA), Cassim Taalib 'Teacher' alisema jijini Dar es Salaam kuwa
maandalizi yamekamilika na Mbwana amewasili nchini kwa mechi ya timu ya
TAifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Misri utakaochezwa Jumamosi.Hivi ndivyo Copa America 2016 itakavyopigwa USA kuanzia leo
#no. | Date | Time in IST | Match | Score | |
---|---|---|---|---|---|
1 | 04-06-2016 | 07:00am | USA vs Colombia | -- | |
2 | 05-06-2016 | 02:30am | Costa Rica vs Paraguay | -- | |
3 | 05-06-2016 | 05:00am | Haiti vs Peru | -- | |
4 | 05-06-2016 | 07:30am | Brazil vs Ecuador | -- | |
5 | 06-06-2016 | 02:30am | Jamaica vs Venezuela | -- | |
6 | 06-06-2016 | 05:30am | Mexico vs Uruguay | -- | |
7 | 07-06-2016 | 04:30am | Panama vs Bolivia | -- | |
8 | 07-06-2016 | 07:30am | Argentina vs Chile | -- | |
9 | 08-06-2016 | 05:30am | USA vs Costa Rica | -- | |
10 | 08-06-2016 | 08:00am | Colombia vs Paraguay | -- | |
11 | 09-06-2016 | 05:00am | Brazil vs Haiti | -- | |
12 | 09-06-2016 | 07:30am | Ecuador vs Peru | -- | |
13 | 10-06-2016 | 05:00am | Uruguay vs Venezuela | -- | |
14 | 10-06-2016 | 07:30am | Mexico vs Jamaica | -- | |
15 | 11-06-2016 | 04:30am | Chile vs Bolivia | -- | |
16 | 11-06-2016 | 07:00am | Argentina vs Panama | -- | |
17 | 12-06-2016 | 04:30am | USA vs Paraguay | -- | |
18 | 12-06-2016 | 06:30am | Costa Rica vs Colombia | -- | |
19 | 13-06-2016 | 04:00am | Ecuador vs Haiti | -- | |
20 | 13-06-2016 | 05:00am | Brazil vs Peru | -- | |
21 | 14-06-2016 | 05:30am | Mexico vs Venezuela | -- | |
22 | 14-06-2016 | 07:30am | Uruguay vs Jamaica | -- | |
23 | 15-06-2016 | 05:30am | Panama vs Chile | -- | |
24 | 15-06-2016 | 07:30am | Argentina vs Bolivia | -- |
2016 Copa America Centenario Quarter Final Match
#no. | Date | Time in IST | Match | Score | Winner |
---|---|---|---|---|---|
25 | 17-06-2016 | 07:00am | Group A1 vs Group B2 | -- | |
26 | 18-06-2016 | 05:30am | Group B1 vs Group A2 | -- | |
27 | 19-06-2016 | 04:30am | Group D1 vs Group C2 | -- | |
28 | 19-06-2016 | 07:30am | Group C1 vs Group D2 | -- |
2016 Copa America Centenario Semi Final Match Schedule
#no. | Date | Time in IST | Match | Score | Winner |
---|---|---|---|---|---|
29 | 22-06-2016 | 06:30am | Winner M25 vs Winner M27 | -- | |
30 | 23-06-2016 | 05:30am | Winner M26 vs Winner M28 | -- |
2016 Copa America Centenario Final Match Schedule
#no. | Date | Time in IST | Match | Score | Winner |
---|---|---|---|---|---|
31 | 26-06-2016 | 05:30am | Looser M29 vs Looser M30 | -- | |
32 | 27-06-2016 | 05:30am | Winner M29 vs Winner M30 | -- |
Liverpool asikuambie mtu baba'ake imepania si utani!
KLABU ya Liverpool ambayo ilikaribia kutwaa taji la UEFA Europa League kama sio kuteleza kwa Sevilla ya Hispania, imedaiwa inaongoza mbio za kuwania saini ya chipukizi wa kimataifa wa Uturuki na klabu ya Nordsjaelland, Emre Mor.
Mor mwenye umri wa miaka 18, anatajwa kama mmoja wa wachezaji bora wanaochipukia Ulaya kwasasa baada ya kuonyesha kiwango bora katika Ligi Kuu ya Denmark na kumfanya kuitwa katika kikosi cha Uturuki kwa ajili ya michuano ya Euro 2016 inayoanza Juni 10 nchini Ufaransa.
Klabu za Manchester United, Borussia Dortmund na Ajax Amsterdam nazo zinatajwa kuwa zinamwania chipukizi huyo anayemudu kiungo mshambuliaji lakini Liverpool ndio inaelezwa kuwa inaongoza mbio hizo.
Dogo huyo amefunga mabao mawili na kusaidia mengine mawili mechi 13 alizoichezea klabu yake msimu huu.
Mor mwenye umri wa miaka 18, anatajwa kama mmoja wa wachezaji bora wanaochipukia Ulaya kwasasa baada ya kuonyesha kiwango bora katika Ligi Kuu ya Denmark na kumfanya kuitwa katika kikosi cha Uturuki kwa ajili ya michuano ya Euro 2016 inayoanza Juni 10 nchini Ufaransa.
Klabu za Manchester United, Borussia Dortmund na Ajax Amsterdam nazo zinatajwa kuwa zinamwania chipukizi huyo anayemudu kiungo mshambuliaji lakini Liverpool ndio inaelezwa kuwa inaongoza mbio hizo.
Dogo huyo amefunga mabao mawili na kusaidia mengine mawili mechi 13 alizoichezea klabu yake msimu huu.
Subscribe to:
Posts (Atom)