STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 27, 2013

Hali ya Mzee Mandela bado tete

Mzee Mandela
BINTI wa Nelson Mandela anasema kiongozi huyo wa zamani wa Afrika kusini yupo katika hali mahututi.
Makaziwe Mandela alizungumza kwenye radio ya taifa Alhamis wakati wanafamilia walipokusanyika kwenye hospitali ya Pretoria Mediclinic Heart  ambapo Bwana Mandela amelazwa kwa siku ya 19 sasa.
Rais Jacob Zuma aliahirisha safari yake kuelekea Msumbiji Jumatano baada ya kumtembelea Mandela hospitali.
Wakati huo huo Rais wa Marekani Barack Obama yupo nchini Senegal kwenye kituo chake cha kwanza katika ziara yake barani Afrika ya kuhamasisha biashara, uwekezaji na usalama wa chakula.
Ajenda zake alhamis zinajumuisha mikutano na dhifa rasmi ya chakula cha jioni na Rais wa Senegal Macky Sall pamoja na mazungumzo ya utawala wa sheria na viongozi wa mahakama katika eneo.
Bwana Obama na mke wake Michelle pia watatembelea kisiwa cha Goree, eneo la UNESCO World Heritage ambalo kutoka karne ya 15 hadi 19 lilikuwa kituo kikubwa cha biashara ya utumwa kwenye pwani ya Afrika.
Kutoka nchini Senegal, bwana Obama anapanga kuelekea Afrika kusini na kutembelea kisiwa cha Robben, gereza ambalo rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela alifungwa kwa takribani miongo miwili. Pia atasimama nchini Tanzania kabla ya kurejea nyumbani nchini Marekani. 
 
VOA

Mwanamke matatani kwa kumuua mumewe kisa debe la Karanga


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani

Na Esther Macha, Mbeya
MWANAMKE mmoja mkazi wa kijiji cha Iganduka wilayani Mbozi Mkoani Mbeya makrina Simbowe (42) anashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani hapa kwa kosa la kumuua mumewe aitwaye Rodrick Mwaipasi (55)baada ya mwanamke huyo kuuza karanga debe mbili bila idhini ya mume wake.
Tukio la kifo cha mwanaume huyo linatokana na marehemu kuhoji kwa mke wake juu ya kuuza karanga debe mbili bila idhini yake na hivyo mwanamke huyo kumsukuma mume wake ambaye aliangukia kisogo na kufariki papo hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Bw.Diwani Athuman alisema tukio hilo limetokea juni 24 mwaka huu majira ya saa 2.00 usiku katika kijiji cha Iganduka wilayani hapa
Baada ya marehemu kusukumwa alidondoka na kupelekwa katika hospitali mbozi mission ambapo hata hivyo alikuwa ameshafariki kutokana na kuangukia kisogo.

Aidha Diwani alisema chanzo cha mzozo huo ugomvi wa kifamilia uliotokea kati yao kisha marehemu kusukumwa na mke wake na kufariki dunia.

Hata hivyo Kamanda Athuman alisema kuwa mtuhumiwa amekamatwa na taratibu zinafanywa ili afikishwe mahakamani ,na kutoa wito kwa jamii kutatua matatizo/migogoro yao kwa njia ya mazungumzo badala ya kujichukulia sheria mkononi kwa kutumia hasira na nguvu.

Safisha Jiji yaendelea kuwaliza wafanyabiashara Dar


ASKARI WA MANISPAA YA  YA KINONDONI WAKISHIRIKIANA ASKARI JESHI LA POLISI LA KUZUIA GHASIA FFU WALIFANYA OPERESHENI SAFISHA JIJI KATIKA ENEO LA STANDI YA MABASI YA DALADA MWENGE LEO









Opresheni safisha jiji inayoendelea jijini Dar imeendelea kuwaacha wamachinga na wafanyabiashara wengine wakitimuliwa katika maeneo waliyozoea kujipatia riziki kaa inavyoonekana pichani hali ilivyokuwa Mwenge baada ya majuzi kufanywa hivyo eneo la Manzese siku chache operesheni hiyo ilipofanyika Posta.

Njemba yaua mtu kwa kisu, kisa...!

Na Esther Macha, Mbeya
JESHI la polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mkazi wa kijiji cha Saman’ombe wilayani Momba Mkoani hapa livingstone mulyatete (42) kwa kosa la kumuua kwa kumchoma kisu Patrick Yohana (30)baada ya marehemu kumtania mtuhumiwa kuwa amenunua piki piki mbovu.
Akizungumza na waandishi wa habari  Kaimu Kamanda wa polisi Mkoani hapa Bw. Barakael Masaki alisema kuwa tukio hilo limetokea juni 26 mwaka huu majira ya saa 12.30 mchana katika kijiji cha Samang’ombe .
Bw. Barakael alisema kuwa chanzo cha ugomvi huo kati ya marehemu na mtuhumiwa ni ugomvi uliotokea kati yao baada ya marehemu kumtania mtuhumiwa kuwa piki piki yake ni mbovu ndipo alipochukua kisu na kumchoma katika ubavu wa kulia na kusababisha kifo chake papo hapo.
Alisema kuwa taratibu zinafanywa ili mtuhumiwa aweze kufikishwa mahakamani mara moja na kujibu tuhuma hizo dhidi yake.
Aidha Kamanda Masaki ametoa wito kwa jamii kudhibiti hasira zao ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

Basi la Sabena lapaja ajali na kuua kichanga Mbeya


Mtambo wa Wachina ukinyenyua gari la Kampuni ya Sabena baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi.






Baadhi  ya abiria walionusurika  wakihamisha mizigo yao kutoka katika gari lililopata ajali ya Kampuni ya Sabena baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi.

Wachina wanaojenga barabara ya Chunya wakishangaa gari la Kampuni ya Sabena baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi.
Majeruhi wa ajali hiyo Ramadhani Kipese (45) akiwa na majeraha kichwani.

Kondakta wa gari la Kampuni ya Sabena Seif Salum (34) akisaidia kuokoa mizigo ya abiria baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi.

Gari la Polisi likiwa eneo la tukio kuokoa mizigo ya majeruhi walolazwa katika Hospital ya Rufaa ya Mbeya.
                             ********************************************
KICHANGA cha Miezi 6 kimefariki dunia papo hapo na wengine zaidi ya 60 wamenusurika kufa  katika ajali mbaya iliyohusisha Basi kampuni ya Sabena baada ya kuacha njia na kutumbukia katika Mtaro  pembezoni mwa Barabara eneo la Maji mazuri Kawetere nje kidogo ya Jiji la Mbeya.
  Kwa mujibu wa Wahanga wa ajali hiyo iliyotokea jana wamesema imetokana na mwendokasi ambapo Dereva alishindwa kulimudu basi hilo lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Mwanza.
Wamesema ajali hiyo imetokea majira ya Saa moja asubuhi  ambapo katika ajali hiyo watu kadhaa walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya huku wengine wakipatiwa huduma ya kwanza kisha kuendelea na safari baada ya kubadilishiwa gari.
Gari hilo lenye namba za usajili T 887 AYG liliharibika vibaya na kushindwa kuendelea na safari ndipo lilipoletwa basi lingine kampuni hiyo hiyo ya Sabena kwa ajili ya kuendelea na Safari.
Kondakta wa Basi hilo Seif Salum(34) amesema chanzo cha ajali hiyo ni ubovu wa gari uliosababisha kupasuka kwa mpira wa Breki hivyo gari kushindwa kusimama na kutumbukia mtaroni.
Amemtaja Dereva wa basi hilo kuwa ni Suddy Hussein ambaye inasadikika kuwa alikimbia baada ya ajali hiyo ingawa kondakta alitoa taarifa kuwa kafuata matibabu Hospitalini.
 Picha na Mbeya yetu.

Tevez atangulia Juve, Kolarov njiani kumfuata

Aleksandar Kolarov and Carlos Tevez - Manchester City v Aston Villa - Capital One Cup Third Round
Kolarov, Tevez wakiwa na Balotelli walipokuwa wote Manchester City
MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya Manchester City, Carlos Tevez ametua kwa mabingwa wa Italia, Juventus, huku 'kibibi' hicho cha Turin kikiamini kuwa kitafanikiwa kumchukua Aleksandae Kolarov ili kuichezea klabu yao.
Tevez aliyekuwa akiwindwa na klabu mbalimbali ikiwemo Ac Milan, ametua Juventus na kukabidhiwa jezi namba 10 baada ya kufaulu vipimo vya afya.
Juventus inaamini baada ya kumnyakua Muargentina huyo, mchezaji mwingine atakayetua Turin ni Mserbia Kolarov, 27 aliyesajiliwa na City kwa thamani ya pauni Mil 16 miaka mitatu iliyopita akitokea Lazio ya Italia.
City haijaweka wazi mipango ya kumuachia beki huyo, lakini hiyo tgayari kocha mpya wa timu hiyo  amefua wazi kutokuwa na mpamngo na beki huyo na kutoa nafasi ya kumfuata Tevez Juventus kirahisi.Tevez alinukuliwa akifurahia kutua kwake Juve ambayo msimu huu iling'olewa kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.
Mshambuliaji huyo atakuwa mchezaji wa kwanza kuvaa jezi namba 10 tangu ilivyovuliwa na Alessandro del Piero.

Kisura wa Miss Utalii ang'ara Kosovo, Bodi yampongeza


Mrembo Mwanakombo Kessy akipata kiburudisho baada ya kazi nzuri nchini Kosovo
Mwanakombo Kessy akiwa na warembo wenzake baada ya shindano la Miss Freedom of the World na kutwaa taji la Best Model


MSHINDI namba tano wa shindano la Miss Utalii Tanzania, Mwanakombo Kessy amefanikiwa kunyakua tuzo ya 'Mwanamitindo Bora' katika mashindano ya Miss Freedom of the World 2013 lililofanyika mwishoni mwa wiki nchini Kosovo na Bodi ya Miss Utalii Tanzania imepongeza.
Mrembo huyo alishinda taji hilo Juni 24  na kuwa taji la sita la kimataifa kwa Tanzania kunyakua kupitia shindano la Miss Utalii.
Kwa ushindi huo kisura huyo amevuna mkataba mnono wenye thamani ya Sh Mil 64 na kampuni ya kimataifa ya Johns Jonson ya Massimo Buttiglieriom.
Kutokana na mafanikio hayo Bodi ya Miss Utalii imemmiminia pongezi kisura huyo na kufurahia kazi kubwa aliyoenda kuifanya Kosovo na kudai ni muendelezo wa rekodi nzuri la shindano lao anga za kimataifa.
Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo 'Chipps', alisema wamefurahi mno kwa tuzo aliyopewa Mwanakombo na wanampongeza kwa kazi kubwa aliyofanya ya kuipeperusha vyema bendera ya tanzania na kuonyesha shindano lao sivyo linavyochukuliwa hapa nchini.
"Ushindi huu ni kwa Taifa zima la Tanzania, watanzania wote hata wale wabaya wetu, wapika majungu wetu, wazushi wetu na wazee wa fitina. Tunatambua ushindi huu wa taji la 6 la kidunia, na mafanikio yetu kila mwaka katika mashindano ya Dunia, " alisema Chipps.
Chipps alisema wanampongeza mrembo wao na wanamsubiri kwa hamu atakaporejea nchini kwa ajili ya kumpa mapongezi ya heshima kwa alichokifanya ikiwa ni siku chache baada ya kushika nafasi ya tano katika shindano lililofanyika jijini Tanga.

Rais Obama apeperusha Tamasha ya wasanii Mkuranga

Rais wa Marekani, Barrack Obama anayetarajiwa kutua nchini wiki ijayo
 TAMASHA la Mastaa Chipukizi lililokuwa lifanyike Jumamosi Juni 29 kijiji cha wasanii Mwanzega Mkuranga limeahirishwa ili kutoa nafasi kwa  wasanii na viongozi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika maandalizi na mapokezi ya  Rais wa Marekani, Baraka Obama.
 
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Caaasim Taalib alisema jana kuwa wanachama wengi waliokuwa washiriki tamasha hilo watakuwa katika maandalizi ya ujio wa Rais Obama hivyo litafanyika mwezi Agosti baada ya sikukuu ya Idd el Fitri.
 
Taalib alisema anawaomba radhi wananchi wa Mkuranga, viongozi mbalimbali na wasanii washiriki wa tamasha hilo waliokuwa wamejiandaa kuonesha vipaji vyao katika tamasha hilo .
 
‘Tumeamua kutoa nafasi hii kwa wanachama wa SHIWATA ili washiriki kikamilifu kudumisha amani katika wakati huu ambao tunatembelewa na Rais Obama na wasanii washiriki kikamilifu, tunaomba tutoe taarifa katika vyombo vya dola mara tunapoona kuna unjifu wa amani’ alisema Taalib.
 
 
Mwenyekiti huyo alisema mgeni rasmi aliyekuwa ameandaliwa, Naibu Waziri wa Kilimo, Adam Malima amepelekewa ujumbe huo pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wabunge wa Dar es Salaam nao wamearifiwa kuhusu kusogezwa mbele tamasha hilo .
 
Alisema sambamba na tamasha hilo, SHIWATA ilikuwa ikabidhi nyumba kwa mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Jellah Mtagwa na wasanii wengine 14 ambao wamekamilisha michango ya ujenzi  wa nyumba zao katika kijiji chao cha Mwanzega Kimbili, Mkuranga.
 
Wengine watakaokabidhiwa nyumba zao ni msanii maarufu nchini, Lumole Matovola ‘Big’ wa Bongo movie ambaye ni wanachama wa SHIWATA wangine ni Mwandishi wa Habari, Josephine Moshi, Farida Ndimbo wa Jeshi la Magereza, Flora Kafwembe wa JKT Mgulani na Nyanza Kisadugwa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).  
 
 Mpaka sasa SHIWATA imejenga nyumba 24 kwa ajili ya wasanii katika eneo la hekari 300 na wanajiandaa kulima shamba la hekari 500 walizonazo ili kujikwamua kimaisha.
 

Watu 10, 799 wanaswa na dawa za kulevya Tanzania

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Mizengo Pinda

WATU 10,799 wamenaswa wakijihusisha na dawa za kulevya katika kipindi cha miaka mitano pekee na kuonyesha namna gani biashara ya dawa hizo lilivyo tatizo nchini.
Kwa mujibu wa hutuba ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda, iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Urasimu na Bunge) William Lukuvi katika Siku ya Kupiga vita Dawa za Kulevya Duniani ni kwamba biashara ya dawa za kulevya ni tatizo nchini.
Pinda alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.
Aidha, amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la biashara haramu ya dawa za kulevya nchini.
“Vile vile katika kipindi hicho jumla ya Watanzania 240 walikamatwa katika nchi mbalimbali, zikiwamo Brazil, Pakstani na Afrika Kusini,” alisema Pinda.
Alisema hali hiyo imekuwa ikiharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu,  masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.
Pinda alisema hali hiyo inatokana na sifa mbaya inayojengeka kwa Watanzania wanaosafiri katika nchi hizo.
Alisema zipo dalili kwamba, endapo biashara hiyo itaachwa iendeleee, athari zaidi, zikiwamo kuingiliwa kwa misingi ya kiutawala na wafanyabiashara wa dawa kwa manufaa binafsi, kuongezeka kwa waathirika wa rushwa.
Aidha, alisema uwapo wa biashara hiyo huongeza mzunguko wa fedha haramu na kusababisha mfumko wa bei na hivyo kuongeza hali ya umaskini.
Pinda alisema kwa mujibu wa vyombo vya dola, takwimu zinaonyesha viwango vya Heroin na Cocaine zinazoendelea kukamatwa nchini, kuanzia mwaka 2000 ni vikubwa kuliko vile vilivyokamatwa miaka 10 iliyopita.
Alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na nchini .
Kwa mujibu wa Pinda, jumla ya kilo 914 za Heroin zilikamatwa na kikosi kazi cha kuzuia uharamia cha Jeshi la Kimataifa.
Alisema askrimu, mikate na maandazi vilivyofanyiwa uchunguzi katika moja ya shule jijini Dar es Salaam vilibainika kuwa na kiasi kidogo cha dawa hizo za kulevya.
Aliwataka walimu na walezi kuwa makini na watu wanaouza vyakula katika maeneo karibu na shule ili kuepuka wauzaji hao kuwafundisha wanafunzi kutumia dawa za kulevya.

Mwanamke akamatwa kwa sangoma akidaiwa kupanga mauaji


MWANAMKE aliyetajwa kwa jina la Magreth Simon Nkwera ambaye andaiwa ni mtoto wa kwanza wa Mnadhimu Mkuu wa kwanza wa JWTZ Brig Gen Simon Nkwera amekamatwa kwa Mganga wa kienyeji akijaribu kutekeleza jaribio la mauaji.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimepenyezwa kwa blogu hii pamoja na picha zinasema kuwa mwanamke huyo alifumwa 'live' kwa sangoma akifanya mipango ya kutekeleza mauaji kwa njia ya kishirikina dhidi ya watoto wa mumewe na baadhi ya ndugu zake huko Kibaha Maili Moja, Pwani.
Kwa sasa mwanamama huyo anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Maili Moja akisubiri kupandishwa kizimbani kwa kosa linalomkabili.
Mtuhumiwa akiwa ndani ya  chumba cha mganga na mganga wake aitwae Yahaya tayari kwa mauwaji
 Mtuhumiwa huyo akiwa ndani ya gari la polisi pamoja na mganga wake aitwae, Yahaya tayari.
 Mtuhumiwa huyo akiwa ndani ya gari la polisi baada ya kukamatwa
Mtuhumiwa akiwa anahojiwa na mzee wa ukoo wa shirima Ofisa Polisi Jeshi daraja la Kwanza (woii mstaafu) Joseph Shirima mara baada ya kumkamata live kwa sangoma.

Yanga kuanza kujifua kwa msimu mpya Julai 2


Kikosi cha mabingwa wa Ligi Kuu, Yanga
MABINGWA wa kandanda nchini, Yanga inatarajiwa kuanza kujifua kwa mazoezi Julai 2 kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na hasa pambano lao la Ngao ya Jamii dhidi ya Azam.
Mazoezi hayo yataanza baada ya wiki mbili za mapumziko walizopewa wachezaji na benchi zima la ufundi la klabu hiyo na yatafanyikia kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola, Mabibo Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya mtandao wa klabu hiyo, wachezaji wote na benchi la ufundi wataanza mazoezi siku ya Jumanne Julai 02 majira ya saa 2 asubuhi kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu inayotarajiwa kuanza rasmi Agosti 24 mwaka huu.
Taarifa hiyo inasema Kocha Mkuu wa timu hiyo, Ernie Brandts ambaye yupo kwao nchini Uholanzi kwa mapumziko ya wiki mbili, anatarajiwa kurejea nchini Julai Mosi na siku itakayofuata ataongoza mazoezi ya timu yao akishirikiana na kocha msaidizi, Fred Felix Minziro.
Yanga inaanza mazoezi mapema ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuhakikisha inatetea ubingwa wake na kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, awali Yanga ilianza mazoezi june 3 kujianda na mashindano ya kombe la Kagame ambalo serikali ilizizuia timu za Tanzania kushiriki mashindano hayo kutokana na hofu ya usalama nchini Sudan.

BFT yasisitiza uchaguzi wake upo palepale Julai 7

Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga
SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), limesisitiza kuwa Uchaguzi Mkuu wake uliopangwa kufanyika Julai 7 upo pale pale jijini Mwanza.
Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema kuwa kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika juzi chini ya Rais wao, Joan Minja kimeamua kuwa uchaguzi huo utafanyika kama ulivyopangawa licha ya kuwepo na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya wadau wa ngumi.
"BFT inasisisiza kuwa uchaguzi upo kama kawaida Julai 7 licha ya aliyewahi kuwa kiongozi kati ya wale waliojiuzulu kutokana na kashfa ya dawa za kulevya, Anakoly Godfrey kupotosha kwamba uchaguzi huo hautafanyika," alisema Mashaga.
Katibu huyo alisema fomu za uchaguzi huo zilianza kutolewa Juni 4 kwenye ofisi za BMT na jijini Mwanza na mwisho wa kuzirudisha ni Julai 4 na siku inayofuata itakuwa siku ya usaili.
"Julai 6 itakuwa siku ya kupitia mapingamizi na kutolea maamuzi na Julai 7 ni siku ya uchaguzi wa BFT kupata viongozi wapya baada ya uongozi wetu kumaliza muda wake tangu Aprili," alisema.
Mashaga alitoa wito kwa watu wote wenye sifa, nia, moyo na uwezo wa kuongoza wajitokeze kuchukua fomu za kugombea uongozi ili kuweza kupata nafasi ya kuiongoza BFT na kuanza maandalizi ya kuiandaa timu kwa ajili ya michuano ya Ndondi ya Afrika itakayofanyika Septemba nchini Mauritius.

Snake Boy Jr kuzichapa Julai 6

Mohammed Matumla 'Snake Boy Jr'
BONDIA Mohammed Matumla pichani anatarajia kupanda ulingoni julay 6 mwaka huu katika ukumbi wa DDC Keko kwa ajili ya kupambana na Hamis Mohamed kutoka GYM YA MZAZI  mpambano huo wa raundi nane utakuwa mkali sana kutokana na kuwa mabondia wote wana uzoefu wa kutosha Matumla anaetokea katika familia yenye vipaji lukuki vya masumbwi Hamisi anatokea katika GYM iliyojihakikishia wanachukua mikanda yote nchini na nje ya nchi

Akizungumza na mwandishi wetu mwandaaji wa mpambano huo Shabani Adios 'Mwaya mwaya' amesema mpambano huo utasindikizwa na mabondia mbalimbali wanaotamba katika masumbwi

Mabondia hawo ni Shafii Ramadhani atakayemenyana na Juma Fundi huku Swaleh Mkalekwa akipambana na Cosmas Kibuga

mpambano huo unaotarajiwa kuwa wa kukata na shoka wa raundi sita umekuwa wa kusisimua na kuzagaa katika vinywa vya mashabiki wa mchezo huo

Huku bondia Mohamed Matumla akimtahadhalisha mpinzani wake kuwa siku hiyo ato kuwa na msalia mtume kwani kawaida yake inajulikana Matumla mpaka sasa amepambana mapambano 13 akidroo matatu na kushinda 10 ata hivyo ame sisitiza kumuhangamiza mpinzani wake mapema kadri iwezekanavyo na kuwaomba wapenzi wa mchezo huo waje mapema kushudia anavyo mmaliza vinginevyo watakosa uhondo wa masumbwi Mbali na kuwepo na mpambano huo Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' atasambaza DVD za mafunzo ya mchezo wa masumbwi
 
CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika masumbwi

DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata dvd hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo
 
katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo ya mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD


mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali 
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D. 

Brazil yatangulia fainali za Mabara, waisubiri Hispania au Italia

Delight: Fred celebrates his strike in front of the adoring fans in Belo Horizonte
Neymar na mchezaji mwenzake wakishangilia bao la Brazili jana

Response: Edinson Cavani equalised for Uruguay early in the second half
Edinson Cavani akishangilia bao lake la kusawazisha jana
WENYEJI wa michuano ya Kombe la Mabara, Brazil usiku wa kuamkia leo walitangulia Fainali za michuano hiyo baada ya kuisasambua Uruguay kwa mabao 2-1 katika pambano kali la nusu fainali.
Bao la  kichwa la dakika za 'jioni' lililofungwa na Paulinho liliivusha Brazil katika hatua hiyo na kusubiri mshindi wa mechi ya leo kati ya Hispania na Italia zitakazoumana katika nusu fainali ya pili.
Uruguay itajilaumu kwa kushindwa kuibuka na ushindi katika mechi hiyo baada ya kuanza kipindi cha kwanza na kupata penati iliyopotezwa na mshambuliaji wake, Diego Forlan kabla ya Brazil kujipatia bao la kuongoza dakika ya 41 kupitia Fred.
Bao hilo lililotokana na shuti kali la Neymer kusindikizwa wavuni na Fred lilidumu hadi wakati wa mapumziko.
Hata hivyo iliwachukua dakika tatu tu Uruguay kulirejesha bao hilo katika kipindi cha pili kilipoanza baada ya Edinson Cavani alipofunga bao baada ya kuiwahi pasi ya Thiago Silva na kufanya pambano kuwa gumu zaidi hadi dakika ya 86 Paulinho alipofunga bao hilo la ushindi.
Hiyo ni mechi ya nne mfululizo kwa Brazil kushinda ikiwa chini ya kocha Luiz Felipe Scolari katika michuano hiyo ambayo ni ya kuikaribisha fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyikia nchini humo mwakani.
Wakati Brazil ikiwa imeshatangulia kwenye fainali timu nyingine ya pili itakayopumana nayo itafahamika usiku wa leo wakati Hispania itakapoumana na Italia ambayo itawakosa nyota wake kadhaa akiwemo Mario Balotelli.
Pambano hilo la Italia na mabingwa wa Ulaya na Dunia, Hispania itakumbusha fainali za Euro 2012 timu hizo zilipokutana na Italia kucharazwa mabao 4-0.