STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 18, 2014

Burundi yafufua matumaini michuano ya CHAN 2014

http://www.yeswefoot.com/medias/burundi-team.jpg
Burundi
WAWAKILISHI wa CECAFA katika michuano ya CHAN 2014 inayoendelea Afrika Kusini, Burundi imefufua matumaini yake ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya muda mfupi uliopita kuicharaza Mauritania kwa mabao 3-2 na kuongoza kwenye msimamo wa kundi lao la D.
Ely Ould Voulany aliishtukiza Burundi kwa kuifungia Mauritania bao dakika ya pili ya mchezo huo kabla ya Abdoul Razak Fiston kusawazisha katika dakika ya 11 kutokana na kazi nzuri ya Suleiman Ndikumana, ambaye alifunga pia bao dakika ya 25 lakini lilikataliwa na mwamuzi na kuzifanya timu ziende mapumziko zikiwa nguvu sawa ya kufungana bao 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa Burundi kupata bao la pili lililofungwa na Nduwarugira katika dakika ya 61 akitengeneza pande na Fiston kabla ya Mauritania kusawazisha dakika ya 70 kupitia Demma kabla ya Ndikumana kufunga bao la ushindi dakika za nyongeza za pambano hilo na kuifanya Burundi kuiengua Gabon kileleni licha ya kulingana nao pointi nne ila wanatofautiana mabao ya kufungwa na kufungwa.
Kipigo hicho cha Burundi limeifanya Mauritania kuwa timu ya tatu kuaga mashindano hayo ikiungana na timu za Msumbiji na Ethiopia zilizotangulia mapema katika makundi yao.
Kesho mechi za lala salama za raundi ya tatu ya makundi hayo zitaanza kwa Nigeria kuvaana na wenyeji wao Afrika Kusini katika pambano la kundi A na Msumbiji kuvaana na Mali, mechi zote zikichezwa wakati mmoja majira ya saa 2 usiku.

Abdi Kassim 'Babi' katika uzi wa UiTM ya Malaysia

Abdi Kassim 'Babi' (kulia-mbele) akiwa na wachezaji wenzake wa UiTM ya Malaysia, kiungo huyo mshambuliaji ametua katika timu hiyo mwishoni mwa mwaka jana kwa mkataba wa mwaka moja na tayari ameshaana kuonyesha makeke kwa kuifungia mabao kwenye mechi za kirafiki kujaindaa na Ligi kuu ya nchi hiyo.

Kado achekelea, akiapa kung'ara zaidi duru la pili

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiKEuWViBK1RvB2yszF1PxMhJ9oTDno9k9KRhyphenhyphennGjTRqcXKe0NrFPYNxFI7dlXI-3QjjBAfOVRNac5XEfoN6LD1rlraERS80n6_P6-mFCCORYMcAFnD-PqwN8vj-h31im-AGNf1Pg774b8/s640/shaaban+kado.jpg
Shaaban Kado 'Baba Munira'
KIPA wa kutaminiwa wa klabu ya Coastal Union, Shaaban Kado amesema anajisikia fahari kubwa kuweza kukaa langoni kwa muda wa dakika 1125 na kufungwa idadi ndogo ya mabao katika duru la kwanza la Ligi Kuu Tanzania Bara,. huku akijitabiria kung'ara zaidi katika duru lijalo litakaloanza wikiendi hii.
 
Aidha kipa huyo aliyepo nchini Oman na kikosi cha timu yake kikifanya mazoezi kujiandaa na duru hilo la pili, amekiri duru lililopita lilikuwa lenye ushindani na kutabiria duru lijalo litakuwa gumu zaidi kutokana na usajili wa dirisha dogo na klabu zinavyojiandaa kwa sasa.
 
Akizungumza na MICHARAZO kwa njia ya mtandao kutoka Oman, Kado alisema anajisikia fahari kubwa kuona amesimama kwenye milingoti mitatu ya klabu yake kwa mechi zote 13 akitumia dakika 1125 na kuifanya Coastal kuwa timu iliyofungwa idadi ndogo ya mabao katika duru lote la kwanza.
 
Kado alisema alicheza dakika zote 90 katika mechi 12 kabla ya mechi yao na Mbeya City kudaka kwa dakika 45 na kutoka kumpisha Said Lubawa aliyekuja kufungwa bao la kusawazisha la penati la Mbeya.
 
"Kwa kweli najisikia fahari sana kuona nimeidakia Coastal kwenye duru la kwanza karibu mechi zote na kufungwa mabao sita, nadhani duru lijalo kwa mazoezi ninayoendelea kuyafanya huku nitang'ara zaidi na kuipaisha timu yangu kwenye ligi," alisema Kado.
 
Kado alisema ligi ya msimu huu kwa ujumla imeonekana ngumu kutokana na ushindani uliopo na kukiri huenda duru lijalo likawa gumu zaidi kwa sababu timu zimepata nafasi yakupumzika na kurekebisha makosa yao kwa kusajili kwenye dirisha dogo na pia kujiandaa vyema wengine wakienda nje ya nchi.
 
Ukiondoa Coastal waliomaliza duru la kwanza katika nafasi ya nane ikiwa na pointi 16 waliopo Oman, Yanga nao wamejichimbia Uturuki ikifanya mazoezi huku Kagera Sugar yenyewe ikijifua nchini Uganda.

Arsenal, Man City zaua zikifukuzana England

Edin Dezko
Dzeko akitupia bao la kuongoza

Santi Cazorla (centre) scores the opener for Arsenal against Fulham
Arsenal ilipoiadabisha Fulham kwa mabao 2-0

MABAO mawili ya Santiago Cazorla yaalitosha kuiwezesha Arsenal kuendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya England na kujichimbia kileleni, huku wapinzani wao wa karibu Manchester City wakiwapumulia nyuma yao baada ya jioni ya leo kutoa kipiogo kingine kizito kwa wapizani wao kwenye ligi hiyo.
Arsenal iliyokuwa nyumbani iliinyoa timu ya Fulham kwa mabao 2-0 kwenye uwanja wake wa Emirates yote yakiwekwa kimiani na Cazorla katika kipindi cha pili na kuifanya timu hiyo ifikishe pointi 51 na kujikitga zaidi kileleni.
Timu inayokamata nafasi ya pili, Man City, iliendelea kugawa dozi kwa wapinzani wake ikipata ushindi wa mechi saba mfululizo baada ya kuinyonyoa Cardiff City kwa mabao 4-2 mabao yaliyofungwa na Edin Dzeko, Jesus Navaz, Yaya Toure na Sergio kun Aguero.
Ushindi huo umeifanya City kufikisha pointi 50, moja nyuma ya vinara Arsenal.
Katika mechi nyingine, Newcastle United ilipata ushindi wa mabao 3-1 ugenini dhidi ya West Ham United, huku Sunderland ikiendelea kuimarika na kutoka mkiani kwa kulazimisha sare ya 2-2 na Southampton, huku Crystal Palace ikikwanyua Stoke City kwa bao 1-0, huku Norwich City ikipata ushindi kama huo mbele ya wageni wao Hull City.
Hivi sasa Liverpool ikiwa nyumbani inapepetana na Aston Villa na matokeo ni sare ya mabao 2-2 baada ya Liverpool kusawazisha hivi punde ikitoka mapumziko ilipokuwa nyuma kwa mabao 2-1.

Coastal yalazimishwa sare na Seeb Oman










Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’, leo wametoka suluhu tasa dhidi ya Seeb SC inayoshiriki ligi kuu ya Oman.
Mechi ya leo ambayo ni ya kirafiki imeisha kwa matokeo ya 0-0 ambayo inakuwa mechi ya nne tangu kuwasili nchini hapa Januari 9, kwa ziara ya wiki mbili kujiandaa na ligi mzunguko wa pili Tanzania Bara.
Coastal Union, imeonyesha uhai katika kipindi cha pili ambapo kipindi cha kwanza walishindwa kuonyesha makeke yao baada ya wachezaji wa Seeb, kujazana katikati hali iliyowafanya Wagosi kushindwa kumiliki mpira.
Aidha, golikipa wa Wagosi, Shaaban Kado alipoiona kasoro hiyo akawa anatumia muda mwingi kupiga mipira katikati kila inapomjia kwa lengo la kuamsha mashambulizi ili viungo wake wachangamke.
Kipindi cha kwanza kiliisha timu zote kizitoka vichwa chini kutokana na kukosa nafasi za kuonyeshana uwezo waliofundishwa na walimu wao.
Kipindi cha pili Seeb Club, walifanya mabadiliko kwa kutoa wachezaji wawili wa ndani na mlinda mlango. Coastal Union waliendelea kucheza bila kufanya mabadiliko.
Katika dakika za awali kipindi cha pili Seeb walionyesha uhai na kulisumbua sana lango la Wagosi, lakini kufuli za Juma Nyoso na Othman Tamim ziliendelea kuwa imara kuulinda mlango wa Shaaban Kado.
Aidha ilipofika dakika ya 76, kocha Yusuf Chipo alifanya mabadiliko ya haraka haraka kwa kutoa wachezaji wane na kuingiza wane ndani ya dakika 15 zilizosalia.
Alianza kutoka Othman Tamim akaingia Abdi Banda, baadae akatoka Danny Lyanga akaingia Mohammed Miraji. Halafu zikiwa zimesalia dakika chache mchezo kuisha alitoka Atupele Green akaingia Suleiman Kassim Selembe, halafu akamalizia mabadiliko kwa kumuingiza Abdullah Othman ‘Ustadh’ akatoka Yayo Kato.
Listi ya leo ilikuwa: Shaaban Kado, Hamadi Juma, Othman Tamim, Juma Said ‘Nyoso’, Mbwana Kibacha, Jerry Santo, Ally Nassor ‘Ufudu’, Danny Lyanga, Atupele Green, Haruna Moshi ‘Boban’, na Yayo Kato.
Coastal Union tangu iwasili Oman imeshacheza mechi nne, imeshinda mechi mbili kati ya Oman Club na Al Mussannah kwa mabao 2-0 kila mechi. Halafu ikafungwa bao 1-0 na Fanja Club, leo imetoka suluhu ya bila kufungana na Seeb Club.
COASTAUNION

Simba yadonyolewa kimoja na Mtibwa Sugar kirafiki

KIKOSI cha vijana wa Msimbazi, Simba jioni ya leo imejikuta ikipokea kipigo cha pili chini ya Kocha Zdravko Logarusic baada ya kukwanyuliwa na Mtibwa Sugar kwa bao 1-0 katika pambano la kirafiki lililochezwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Bao pekee lililoinyamazisha Simba iliyotoka kupokea kipigo cha b aoa 1-0 toka kwa KCC ya Uganda katika fainali ya Kombe la Mapinduzi liliwekwa kimiani na Masoud Ally ‘Chile’ katika dakika ya 64 akimaliza kazi ya Jamal Mnyate.
Kikosi hicho cha Mtibwa Sugar kesho itashuka tena dimbani kwa kuvaana na AShanti United katika pambano jingine la kujiandaa na duru la pili la Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza wiki ijayo.

DR Congo wanyukwa kimoja CHAM 2014

http://mtn.ensight-cdn.com/content/RD-Congo-v-Libye-RD-Congo-T~1.jpg
DR Congo
 BAO pekee lililofungwa dakika ya pili na Erwin N'Guema Obame wa Gabon lilitosha kuizima DR Congo katika pambano la Kundi D la michuano ya Kombe la CHAN lililochezwa jioni hii.
N'Guema alifunga bao hilo akimaliza kazi nzuri iliyofanywa na Samson Mbingui na kuifanya timu yake kuibuka na ushindi huo na kuchupa hadi kileleni mwa kundi hilo kwa kufikisha pointi nne baada ya mchez wake wa awali dhidi ya Burundi kumalizika kwa sare pacha ya 0-0.
DR Congo yenyewe imesaliwa na pointi zake tatu ilizopata kwa kuilaza Mauritania ambayo baadaye itavaana na Burundi katika mchezo wa pili wa kundi hilo kuhitimisha mechi za raundi ya pili kwa makundi yote manne kabla ya mzunguko wa tatu kujua timu zitakazotinga robo fainali kufahamika rasmi.
Kwani mpaka sasa hakuna timu hiyo iliyojihakikisha kutinga hatua hiyo kutokana na timu 16 zinazoshiriki michuano hiyo kubanana vilivyo japo nchi mbili za Msumbiji na Ethiopia zenyewe zimeshaaga mashindano kwa kufungashiwa virago baada ya kupoteza mechi zao mbili za awali katika makundi yao.

Wahabeshi kuwahukumu Yanga kwa Wakomoro

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Somalia kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Komorozine Sports ya Comoro.
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya mchujo itafanyika jijini Dar es Salaam kati ya Februari 7 na 9 mwaka huu wakati ile ya marudiano itachezwa kisiwani Comoro kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.


Mwamuzi wa kati atakuwa Hassan Mohamed Hagi wakati wasaidizi wake ni Hamza Hagi Abdi, Bashir Abdi Suleiman na Bashir Olab Arab. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Eugene Musoke kutoka Uganda.

Timu ambazo zimeingia moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa ni Coton Sport ya Cameroon, El Ahly (Misri), TP Mazembe (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), El Hilal (Sudan), Club Sportif Sfaxien (Tunisia) na Esperance (Tunisia)

Nayo mechi ya kwanza ya raundi ya mchujo kati ya Azam ya Tanzania na Ferroviario Da Beira ya Msumbiji itakayofanyika Dar es Salaam kati ya Februari 7 na 9 mwaka huu itachezeshwa na waamuzi kutoka Sudan.

Waamuzi hao ni Mutaz Abdelbasit Khairalla atakayepuliza filimbi, Waleed Ahmed Ali, Aarif Hasab Elton na El Fatih Wadeed Khaleel. Kamishna wa mechi hiyo ni Hassan Mohamed Mohamed kutoka Somalia. Mechi ya marudiano itachezwa Msumbiji kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.

Timu zilizotinga moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo ni Asec Mimosas ya Ivory Coast, Ismailia (Misri), Wadi Degla (Misri), Djoliba (Mali), MAS (Morocco), Bayelsa United (Nigeria), El Ahly Shandy (Sudan), E.S.S. (Tunisia), C.A.B. (Tunisia) na Zesco United (Zambia).

Ethiopia yaaga CHAN, Burundi ikijaribu bahati leo

http://www.futaa.com//images/350x300/ethiopia_1.jpg 
WAKATI Ethiopia ikipoteza matumaini ya kutamba kwenye michuano ya CHAN inayoendelea nchini Afrika Kusini baada ya jana kukubali kipigo cha pili, wawakilishi wengine wa CECAFA, Burundi leo itatupa karata yake ya pili kwa kuvaana na Mauritania.
Ethiopia ililala kwa bao 1-0 jana kwa Jamhuri ya Kongo, wakati Libya na Ghana zikishindwa kutambiana kwa kutoka sare ya 1-1 katika mechi zao za Kundi C zilizochezwa kwenye uwanja wa Free State.
Kwa kipigo hicho Ethiopia ni kama imefungasha virago na inasubiri tu pambano la kukamilisha ratiba kwani hata ikishinda haiwezi kuzivuka pointi ilizonazo timu za Ghana na Libya zenye pointi nne kileleni.
Wakati Ethiopia ikiaga, Burundi leo itashuka dimbani kuumana na Mauritania katika mechi ya kundi D huku  DR Congo ikivaana na Gabon mapema jioni hii.
Katika mechi yao ya kwanza Burundi ililazimishwa suluhu na Gabon, huku DR Congo ikishinda 1-0 dhidi ya Mauritania.
Mpaka sasa mchezaji Bernard Parker wa Bafana Bafana ndiye anayeongoza kwa kufunga mabao matatu akifuatiwa na wachezaji wawili wenye mabao mawili kila mmoja akiwamo Mganda, Yunus Sentamu.
Mataifa yote hayo mawili yalishinda katika michezo yao ya ufunguzi Jumatatu usiku mjini Bloemfontein.
Ushindi kwa yoyote baina yao itakuwa unawapa nafasi ya kusonga mbele katika robo fainali ya michuano hiyo na la muhimu zaidi kumaliza katika nafasi ya juu katika kundi C.
Mshindi wa kwanza wa kundi hili atakutana dhidi ya mshindi wa nafasi ya pili wa kundi D, kundi ambalo linaonekana kama mchekea katika michuano hiyo.

Yanga kuwavaa KS Flamurtari Vlore

MABINGWA wa soka nchini Young Africans leo itashuka dimbani kucheza na timu ya KS Flamurtari Vlore inayoshika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Albania, ikiwa ni sehemu ya mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kwa timu zote ambao utakaofanyika katika eneo la Side Manavagat.
Huu utakua ni mchezo wa tatu wa Young Africans wa kujipima nguvu dhidi ya timu hiyo ya Ligi Kuu nchini Albani baada ya kuwa imeshacheza michezo miwili na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ankara Sekerspor na 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK.
Taarifa kupitia mtandao wa klabu hiyo imesema kuwa Kocha mkuu wa klabu hiyo Hans Van Der Plyum ameendelea na mazoezi leo asubuhi na jioni ataendelea na mazoezi pia kuwaandaa vijana wake kuwa tayari kwa mchezo huo, lakini pia kuwaweka tayari kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
  
Baada ya mchezo dhidi ya timu KS Flamurtari Vlore kesho, Young Africans itakamilisha ziara yake ya kambi ya mafunzo nchini Uturuki kwa kucheza na timu ya Simurq PIK inayoshikri Ligi Kuu nchini Azerbaijan katikati ya wiki ijayo kabla ya kuanza safari ya kurejea nchini Tanzania. 
Hali ya hewa jijini Manavgat ni nzuri na sio ya baridi kali kiasi kwamba haiwalazimu wachezaji kuwaa vifaa vya michezo vya baridi kwani hali inawaruhusu kuweza kufanya mazoezi na kucheza bila kuwa na mataitzo yoyote.
Mpaka sasa hakuna katika kambi ya klabu ya Young Africans nchini Uturuki hakuna mchezaji yoyote majeruhi isipokuwa kiungo Hassan Dilunga ambaye anasumbuliwa na malaria na tayari anaendelea vizuri baada ya kupatiwa tiba na daktari wa timu Dr. Suphian Juma.

Waamuzi 8 waula michuano ya CAF

WAAMUZI nane wa Tanzania wameteuliwa kuchezesha mechi mbili za marudiano za raundi ya awali za Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) na Kombe la Shirikisho (CC) zitakazochezwa wikiendi ya Februari 14 na 16 mwaka huu.

Waamuzi hao walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni Israel Mujuni atakayechezesha mechi ya CL kati ya Rayon Sport ya Rwanda na AC Leopards de Dolisie ya Congo itakayofanyika jijini Kigali.

Mujuni atasaidiwa na Josephat Bulali, Samwel Mpenzu na Ramadhan Ibada, wakati Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Jean Marie Hicuburundi wa Burundi.

Naye Waziri Sheha ataongoza jopo lingine kwenye mechi ya CC kati ya FC MK ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na El Ahly Atbara ya Sudan. Mechi hiyo itachezwa jijini Kinshasa.

Sheha atasaidiwa na Ferdinand Chacha, John Kanyenye na Israel Mujuni. Kamishna wa mechi hiyo ni Chayu Kabalamula kutoka Zambia.

Semina ya kupandisha daraja waamuzi J'4

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi-_FZ5LRs-CTRVIXHK_m_6vV8Q1IZ_9ZBWFI-Ko3Z4SpHpeEOfVggBRF2mOT_cdJe_t_V-6Uu1gHzOT37cJMOyTDsa5h6LUHf22Ei-51zTgbJxEySpdogLZaNub5ZiVSb_s4_2fgkMyUU/s640/DSC04815.JPG
Semina kwa ajili ya kupandisha madaraja waamuzi itafanyika Januari 21 na 22 mwaka huu katika vituo vitatu vya Dodoma, Mwanza na Songea.

Waamuzi watakaoshiriki katika semina hizo ambazo pia zitahusisha mitihani ya utimamu wa mwili (physical fitness test) watajigharamia wenyewe na wanatakiwa kufika vituoni siku moja kabla. Waamuzi hao ni wa daraja la pili na tatu.

Kituo cha Dodoma kitahusisha waamuzi kutoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, Pwani, Singida na Tanga. Wakufunzi katika kituo hicho ni Paschal Chiganga, Said Nassoro na Soud Abdi.

Wakufunzi wa kituo cha Mwanza kwa ajili ya waamuzi wa mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Tabora ni Alfred Kishongole, Kanali Issarow Chacha, Saloum Chama na Zahra Mohamed.

Kituo cha Songea ni kwa ajili ya waamuzi kutoka Iringa, Lindi, Mbeya, Mtwara, Njombe, Rukwa na Ruvuma. Wakufunzi katika kituo hicho ni Charles Ndagala, Joseph Mapunda, Riziki Majala na Victor Mwandike.

Waamuzi wote wanatakiwa kwenda katika kituo walichapangiwa. Vilevile wanatakiwa kuwa na barua kutoka kwa makatibu wa Vyama vya Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) wa mikoa yao ikiwatambulisha pamoja na kuonesha madaraja yao.