MABINGWA wa soka nchini Young Africans leo itashuka dimbani kucheza na timu ya KS
Flamurtari Vlore inayoshika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu
nchini Albania, ikiwa ni sehemu ya mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu
kwa timu zote ambao utakaofanyika katika eneo la Side Manavagat.
Huu utakua ni mchezo wa tatu wa Young Africans wa kujipima nguvu
dhidi ya timu hiyo ya Ligi Kuu nchini Albani baada ya kuwa imeshacheza
michezo miwili na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ankara
Sekerspor na 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK.
Taarifa
kupitia mtandao wa klabu hiyo imesema kuwa Kocha mkuu wa klabu hiyo
Hans Van Der Plyum ameendelea na mazoezi leo asubuhi na jioni
ataendelea na mazoezi pia kuwaandaa vijana wake kuwa tayari kwa mchezo
huo, lakini pia kuwaweka tayari kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Baada
ya mchezo dhidi ya timu KS Flamurtari Vlore kesho, Young Africans
itakamilisha ziara yake ya kambi ya mafunzo nchini Uturuki kwa kucheza
na timu ya Simurq PIK inayoshikri Ligi Kuu nchini Azerbaijan katikati ya
wiki ijayo kabla ya kuanza safari ya kurejea nchini Tanzania.
Hali
ya hewa jijini Manavgat ni nzuri na sio ya baridi kali kiasi kwamba
haiwalazimu wachezaji kuwaa vifaa vya michezo vya baridi kwani hali
inawaruhusu kuweza kufanya mazoezi na kucheza bila kuwa na mataitzo
yoyote.
Mpaka sasa hakuna katika kambi ya klabu ya Young Africans
nchini Uturuki hakuna mchezaji yoyote majeruhi isipokuwa kiungo Hassan
Dilunga ambaye anasumbuliwa na malaria na tayari anaendelea vizuri baada
ya kupatiwa tiba na daktari wa timu Dr. Suphian Juma.
No comments:
Post a Comment