SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF) limeteua waamuzi kutoka Somalia kuchezesha mechi ya Ligi ya
Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Komorozine Sports ya
Comoro.
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya mchujo
itafanyika jijini Dar es Salaam kati ya Februari 7 na 9 mwaka huu wakati
ile ya marudiano itachezwa kisiwani Comoro kati ya Februari 14 na 16
mwaka huu.
Mwamuzi wa kati atakuwa Hassan Mohamed Hagi
wakati wasaidizi wake ni Hamza Hagi Abdi, Bashir Abdi Suleiman na Bashir
Olab Arab. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Eugene Musoke kutoka Uganda.
Timu
ambazo zimeingia moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya Ligi ya
Mabingwa ni Coton Sport ya Cameroon, El Ahly (Misri), TP Mazembe
(Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), El Hilal (Sudan), Club Sportif
Sfaxien (Tunisia) na Esperance (Tunisia)
Nayo mechi ya
kwanza ya raundi ya mchujo kati ya Azam ya Tanzania na Ferroviario Da
Beira ya Msumbiji itakayofanyika Dar es Salaam kati ya Februari 7 na 9
mwaka huu itachezeshwa na waamuzi kutoka Sudan.
Waamuzi
hao ni Mutaz Abdelbasit Khairalla atakayepuliza filimbi, Waleed Ahmed
Ali, Aarif Hasab Elton na El Fatih Wadeed Khaleel. Kamishna wa mechi
hiyo ni Hassan Mohamed Mohamed kutoka Somalia. Mechi ya marudiano
itachezwa Msumbiji kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.
Timu
zilizotinga moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo ni
Asec Mimosas ya Ivory Coast, Ismailia (Misri), Wadi Degla (Misri),
Djoliba (Mali), MAS (Morocco), Bayelsa United (Nigeria), El Ahly Shandy
(Sudan), E.S.S. (Tunisia), C.A.B. (Tunisia) na Zesco United (Zambia).
No comments:
Post a Comment