Shaaban Kado 'Baba Munira' |
Aidha kipa huyo aliyepo nchini Oman na kikosi cha timu yake
kikifanya mazoezi kujiandaa na duru hilo la pili, amekiri duru
lililopita lilikuwa lenye ushindani na kutabiria duru lijalo litakuwa
gumu zaidi kutokana na usajili wa dirisha dogo na klabu zinavyojiandaa
kwa sasa.
Akizungumza na MICHARAZO kwa njia ya mtandao kutoka Oman, Kado
alisema anajisikia fahari kubwa kuona amesimama kwenye milingoti mitatu
ya klabu yake kwa mechi zote 13 akitumia dakika 1125 na kuifanya Coastal
kuwa timu iliyofungwa idadi ndogo ya mabao katika duru lote la kwanza.
Kado alisema alicheza dakika zote 90 katika mechi 12 kabla ya mechi
yao na Mbeya City kudaka kwa dakika 45 na kutoka kumpisha Said Lubawa
aliyekuja kufungwa bao la kusawazisha la penati la Mbeya.
"Kwa kweli najisikia fahari sana kuona nimeidakia Coastal kwenye
duru la kwanza karibu mechi zote na kufungwa mabao sita, nadhani duru
lijalo kwa mazoezi ninayoendelea kuyafanya huku nitang'ara zaidi na
kuipaisha timu yangu kwenye ligi," alisema Kado.
Kado alisema ligi ya msimu huu kwa ujumla imeonekana ngumu kutokana
na ushindani uliopo na kukiri huenda duru lijalo likawa gumu zaidi kwa
sababu timu zimepata nafasi yakupumzika na kurekebisha makosa yao kwa
kusajili kwenye dirisha dogo na pia kujiandaa vyema wengine wakienda nje
ya nchi.
Ukiondoa Coastal waliomaliza duru la kwanza katika nafasi ya nane
ikiwa na pointi 16 waliopo Oman, Yanga nao wamejichimbia Uturuki
ikifanya mazoezi huku Kagera Sugar yenyewe ikijifua nchini Uganda.
No comments:
Post a Comment