WAKATI Ethiopia ikipoteza matumaini ya kutamba kwenye michuano ya CHAN inayoendelea nchini Afrika Kusini baada ya jana kukubali kipigo cha pili, wawakilishi wengine wa CECAFA, Burundi leo itatupa karata yake ya pili kwa kuvaana na Mauritania.
Ethiopia ililala kwa bao 1-0 jana kwa Jamhuri ya Kongo, wakati Libya na Ghana zikishindwa kutambiana kwa kutoka sare ya 1-1 katika mechi zao za Kundi C zilizochezwa kwenye uwanja wa Free State.
Kwa kipigo hicho Ethiopia ni kama imefungasha virago na inasubiri tu pambano la kukamilisha ratiba kwani hata ikishinda haiwezi kuzivuka pointi ilizonazo timu za Ghana na Libya zenye pointi nne kileleni.
Wakati Ethiopia ikiaga, Burundi leo itashuka dimbani kuumana na Mauritania katika mechi ya kundi D huku DR Congo ikivaana na Gabon mapema jioni hii.
Katika mechi yao ya kwanza Burundi ililazimishwa suluhu na Gabon, huku DR Congo ikishinda 1-0 dhidi ya Mauritania.
Mpaka sasa mchezaji Bernard Parker wa Bafana Bafana ndiye anayeongoza kwa kufunga mabao matatu akifuatiwa na wachezaji wawili wenye mabao mawili kila mmoja akiwamo Mganda, Yunus Sentamu.
Mataifa yote hayo mawili yalishinda katika michezo yao ya ufunguzi Jumatatu usiku mjini Bloemfontein.
Ushindi kwa yoyote baina yao itakuwa unawapa nafasi ya kusonga mbele
katika robo fainali ya michuano hiyo na la muhimu zaidi kumaliza katika
nafasi ya juu katika kundi C.
Mshindi wa kwanza wa kundi hili atakutana dhidi ya mshindi wa nafasi ya
pili wa kundi D, kundi ambalo linaonekana kama mchekea katika michuano
hiyo.
No comments:
Post a Comment