STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 30, 2013

Baada ya kutemeshwa Uhai Cup, Azam sasa wajifariji


Baadhi ya nyota wa Azam waliopo Kilimnajrao Stars, Murad, Mao na Kussi wakikabana na Mari Kiemba wa Simba

LICHA ya kuyaaga mashindano ya uhai Cup katika ngazi ya nusu fainali baada ya kufungwa 1-0 na Coastal Union, wanafainali wa Uhai Cup mwaka jana ambapo kombe lilichukuliwa na Azam Academy, bado Azam Academy imekuwa timu ya mfano na kujivunia baada ya kutoa wachezaji wanne kwenye kikosi cha timu ya taifa Kilimanjaro Stars inayoshiriki mashindano ya GoTV CECAFA Challenge Cup

Huenda kutolewa kwa Azam Academy kumechangiwa na kukosekana kwa nyota hao ambao haiyumkini uwepo wao ungeisaidia sana Azam Academy, lakini uongozi wa Azam FC bado unajivunia kikosi chake cha timu ya vijana.

Uongozi wa Azam FC haumlaumu kocha kim Poulsen kwa kuchukua wachezaji wake bali unajisikia faraja kuona vijana wake wakipata nafasi ya kuwakilisha nchi kwani hilo ndilo lengo kuu la Azam FC (Mapinduzi ya Soka la Tanzania)

Aishi Salum Manula, mmoja wa magolikipa bora nchini na mlinda mlango namba mbili wa kikosi cha kwanza cha Azam FC anatoka kwenye academy hii na hii ni faida zaidi ya kutwaa Uhai Cup.

Lakini si Aishi pekee, Farid Mussa Malik na mchezaji bora wa vijana wa Gazeti la Mwanaspoti Joseph Kimwaga ambaye goli lake la dakika ya 90 lilitosha kuipa ushindi Azam FC dhidi ya Yanga wamo kwenye kikosi cha timu ya taifa na hili linaifanya Academy ya Azam FC iwe na maaana zaidi ya academy nyingize zilizopo nchini.

Katika kikosi kilichopo Nairobi, kocha Kim Paulsen amemjumuisha Ismail Adam Gambo kikosini na kufanya wachezaji kutoka Azam Academy kufika wanne.

Lakini utasema nini kuhusu Braison Raphael? Huyu ni zaidi ya lulu kwenye soka la Tanzania, moyo wake wa kupambana, ushujaa wa kujitolea na safari zake kwenye dimba la soka kunamfanya awe mchezaji wa kipekee… ni dhahiri Braison Raphale atapaa kwenda kikosi cha kwanza hivi karibuni kama ilivyo kwa Gardian Michale ambae kama ilivyo kwa Braison, wameonesha kiwango kikubwa sana.

Wachezaji wengine walioonesha kiwango kikubwa kwenye mashindano haya ni, beki wa kati Yaruk Dizana na winga teleza mwenye uwezo mkubwa na kuuchezea mpira Erick Haule….

Wawili hawa watapata mafanikio makubwa sana kama watapata nafasi ya kujiendeleza.

Azam Academy pia inajivunia uwepo wa Mudathir Yahya kwenye kikosi cha kwanza ambaye ameungana na Samih Haji Nuhu na Himid Mao Mkamy ambao walipandishwa miaka mitatu iliyopita.

Kutokana na hayo licha ya Azam FC kusononeka kutokana na kutolewa kwenye hatua ya nusu fainali za Uhai Cup, lakini mafanikio haya ya kuzalisha vipaji ambayo vimeweza kupevuka na kuwa na manufaa ndani ya muda mfupi unatoa faraja na kuonesha dira ya mafanikio.


AZAM FC

Kocha wa Azam atua Bongo, wa Simba kesho (?)

Kocha Omog alipowasili nchini asubuhi ya leo hapa akielekea kwenye gari (Azam FC)

HATIMAYE kocha mkuu mptya wa Azam, Joseph Omog ametua nchini na anatarajia kutambulishwa kwa wanahabari mara baada ya kumalizana na uongozi wa klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kocha huyo kutoka Cameroon na aliyekuwa akiifundisha timu ya AC Leopards ya Jamhuri ya Congo ametua asubuhi ya leo tayari kusaini mkataba wa kuanza kuinoa timu hiyo iliyoachana na Muingereza Stewart John Hall.
Wakati Azam wakimpokea kocha wao, Simba wenyewe inadaiwa kuwa itampokea kocha wake mpya,  Zdravko Logarusickutoka Croatia kesho tauyari kuanza kibarua chake kuchukua mikoba ya King Abdallah Kibadeni anayedaiwa kuelekea Ashanti United.
Kocha huyo alitangazwa na Kaimu Makamu Mwenyekiti , Joseph Itang'are na kupingwa na Mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage, aliyesisitiza kuwa Kibadeni ataendelea kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kwani hawaoni sababu ya kumuengua kikosini kwa sasa.
Huyu ndiye kocha mpya wa Simba anayeelezwa atatua kesho nchini

Kombe la Dunia hatimaye latua Tanzania


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akilifunua Kombe la Dunia la FIFA katika Uwanja wa michezo wa CCM Kirumba mjini Mwanza jana jioni baada ya kulipokea Kombe hilo lililotua nchini kwa mara ya pili, ambapo leo wananchi watapata fursa ya kupiga nalo picha.
 

Rais Kikwete, akilinyanyua Kombe hilo kwa furaha baada ya kuzindua rasmi shambra shambra za ujio wake nchini katika uwanja wa Kirumba jijini Mwanza jana jioni.
 
Rais Kikwete, akifurahia huku akiwa ameliinua Kombe hilo juu kuwaonyesha wananchi waliojitokeza kwenye Uwanja wa Kirumba kulipokea. Wananchi wa Jiji la Dar es Salaam, leo watapata fursa ya kupiga picha na kombe hilo katika Uwanja wa Taifa.

Wakongwe kibao kumsindikiza Mzee Gurumo akiagwa TCC

Mzee Gurumo anayetarajiwa kuagwa rasmi baada ya kustaafu muziki
MKONGWE wa muziki wa dansi Kassim Mapili amethibisha kushiriki Tamasha la Gurumo 53 litakalofanyika Jumamosi ya tarehe 14 mwezi Disemba mwaka huu.

Mapili amesema si yeye tu, bali pia ataratibu mpango mzima wa kuhakikisha wakongwe wote wa muziki wa dansi wanashiriki tamasha hilo bure bila malipo yoyote.

Tamasha hilo ambalo ni mahsusi kwaajili ya kumuaga mwimbaji mkongwe Muhidini Mwalimu Gurumo 'Kamanda' litafanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe.

Mratibu wa tamasha hilo, Juma Mbizo amesema Mapili ameamua kubeba jukumu la kuandaa wakongwe ambao ambao watatengeneza wimbo maalum wa kumuaga Gurumo utakaosikika kwa mara ya kwanza TCC Club Disemba 14.

Baadhi ya wakongwe  wengine waliothibitsha kushiriki Tamasha la Gurumo 53 ni pamoja Komandoo Hamza Kalala, Tshimanga Kalala Assossa na Waziri Ali.

Gurumo anaagwa kufuatia  kutangaza kwake kuachana rasmi na muziki wa jukwaani baada ya kudumu kwenye kazi hiyo kwa miaka 53.

Bendi za Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na wanamuziki kibao waliowahi kung’ara na Sikinde ni sehemu ya wasanii watakaosindikiza tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu.

Hadi kustaafu kwake Gurumo aliyezitumikia pia bendi za Kilimanjaro Chacha,Rufiji Jazz, Kilwa Jazz, Sikinde na OSS – Ndekule, alikuwa ni kiongozi na mmoja wa wamiliki wa Msondo Ngoma.

Wasanii waliowahi kuitumikia Sikinde ambao watakuwepo kumsindikiza Gurumo ni pamoja na Cosmas Chidumule, Abdallah Gama, Hussein Jumbe, Mashaka Shaaban, Kalamazoo, Henry Mkanyia na Karama Legesu. Wengine ni Ali Yahaya na Boniface Kachale, Benno Villa Anton, na Ibrahim Mwinchande.

Hata hivyo, licha ya wasanii hao waliowahi kuitumikia Sikinde kuwemo kwenye tamasha hilo, bendi ya Mlimani Park “Sikinde Ngoma ya Ukae” haitashirki katika Gurumo 53 kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wao.

Mbizo amesema Mlimani Park ina mkataba unaowabana kufanya onyesho lolote litakalowakutanisha na Msondo hadi baada ya sikukuu ya Krismasi (Disemba 25, 2013).

Juma Mbizo amesema licha ya Sikinde kutoshiriki tamasha hilo lakini nyimbo zote zilizotamba ndani ya bendi hiyo ambazo zilitungwa na Gurumo, zitarindima TCC Club kwa ubora ule ule.

“Wanamuziki wengi waliofanya kazi na Gurumo katika Sikinde enzi hizo, hawako tena katika bendi hiyo, hivyo watakuwa huru kuungana na mwimbaji huyo mkongwe na kushusha burudani nzito.

Samatta, Ulimwengu kuweka rekodi leo Afrika na Tp Mazembe?

http://millardayo.com/wp-content/uploads/2013/09/B12CXSM0063.jpg
TP Mazembe watavuna nini leo kwa Watunisia Kombe la Shirikisho?
Na Nurat Mahmoud, Lubumbashi 
WASHAMBULIAJI Mbwana Ally Samatta na Thomas Emanuel Ulimwengu leo watakuwa wanawania kuwa Watanzania wa kwanza kuvaa Medali za Dhahabu za michuano ya Afrika wakati klabu yao, Tout Puissant Mazembe itakapokuwa inamenyana na CS Sfaxien ya Tunisia, katika fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi.
Mazembe inatakiwa kushinda mabao 3-0 leo nyumbani ili kutwaa taji hilo, baada ya awali kufungwa mabao 2-0 na Watunisia hao Uwanja Olympique de Rades mjini Tunis katika Fainali ya kwanza.
Mbwana Samatta kushoto akiwa ameinua Kombe la Super la DRC miezi miwili iliyopita,je leo atainua Kombe la Shirikisho?

Siku hiyo, mabao yaliyoizamisha Mazembe yalifungwa na washambuliaji wa kimataifa wa Gabon, Ibrahim Didier Ndong aliyefunga bao la kwanza dakika ya 16 na mshambuliaji Taha Yassine Khenissi aliyefunga la pili dakika ya 90 na ushei wakimtungua kipa mahiri, Robert Muteba Kidiaba.
Washambuliaji wote wa Tanzania, Samatta na Ulimwengu walianza katika kikosi cha Mazembe pamoja na Tressor Mputu Mabi, lakini hawakuweza kuwanusuru mabingwa mara nne Afrika na kipigo hicho.
Sfaxien, timu pekee iliyoshinda Kombe la Shirikisho mara mbili tangu kutambulishwa kwa mfumo mpya mwaka 2004, yenye maskani yake katika mji uliozungukwa na bahari ya Mediterranean, Sfax itahitaji sare katika mchezo wa marudiano au kufungwa kwa tofauti isiyozidi bao 1-0, mjini Lubumbashi ili kujinyakulia taji.
Bingwa wa Kombe hilo atazawadiwa kitita cha dola za Kimarekani, 625 000, wakati mshindi wa pili atapata dola 432 000.
Mshindi pia atamenyana na mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, Al Ahly ya Misri kuwania taji la Super Cup mechi itakayopigwa nchini Misri Februari 2014.
Wachezaji waliokuwa wakiunda kikosi cha Simba SC mwaka 1993 walivalishwa Medali za Fedha na Rais mstafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi baada ya kufungwa mabao 2-0 na Stellah Abidjan ya Ivory Coast mwaka 1993 katika fainali ya pili ya Kombe la CAF Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Awali, Simba ilitoa sare ugenini na kuwapa matumaini Watanzania kwamba taji la kwanza kubwa Afrika lingetua nchini mwaka 1993.
Washambuliaji hao, Samatta na Ulimwengu baada ya fainali hiyo ya mwisho leo, kesho watapanda ndege kuelekea Nairobi, Kenya kuungana na kikosi cha Bara, Kilimanjaro Stars kinachoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge.

Jicho Jipya la Odama kutoka Desemba 24

Hii ndiyo filamu mpya ya Jennifer Kyaka 'Odama' itakayoachiwa siku moja kabla ya Sikukuu ya Xmass unajua vimbwanga na Salim Ahmed? Ebu isaker itakapotoka umuone huyu jamaa asivyo na mpinzani kwa sasa miongoni mwa waigizaji walioibuka hivi karibuni...Anatisha!

Huyu jamaa kiboko anashikilia rekodi ya aina yake, ebu msome!


 [HenryEarlMontage.jpg]
HENRY Earl, the man who has been arrested more than 1,250 times, spent another Thanksgiving in jail.
Earl, crowned the "World's Most Arrested Man" by The Smoking Gun, was most recently arrested on Oct. 4 for public intoxication in Lexington, Ky.
According to Fayette County Detention Center records, where Earl is currently incarcerated, he has been arrested 1,267 times. His next court date is Dec. 5.
"He is somewhat of a superstar in his own little world," County Detention Center Officer John Casey told ABCNews.com.
According to records obtained by The Smoking Gun, Earl's rap sheet spans back four decades. He was first busted in Fayette County in July 1970, when he was 20 years old, for carrying a concealed weapon. He was arrested 33 more times in that decade alone.
Earl, whose arrests usually involve alcohol, The Smoking Gun reported, spent Thanksgiving behind bars for the third time in the past five years. He celebrated his 64th birthday in jail on Oct. 24.

ABCNews

Kaseba kuzipiga na Jibaba Desemba 21

Mabondia Japhet Kaseba wa jijini Dar es Salaam, na Alibaba Ramadhan wa jijini Arusha, wanategemea kupanda ulingoni siku ya jumamosi ya tarehe 21 Decemba, mwaka huu katika ukumbi wa friends corner hotel,kuzichapa katika pambano la ubingwa wa pst
Pambano hilo liloandaliwa na Promota Ibrahim Kamwe chini ya  BigRight Promotion kwa usimamizi wa PST, pia litakuwa na mapambano  mengine tisa ya utangulizi ambayo yatawakutanisha mabondia kama Karage Suba na Fadhil Awadh, watakaozichapa kuwania ubingwa wa Mkoa katika uzito wa wealter Kg66 pambano la raundi kumi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Mratibu wa pambano hilo Ibrahim Kamwe, alisema kuwa  zaidi ya hayo mapambano ya ubingwapia mahasimu wawili wa uzito wa juu Lusekelo Daudi atazipiga na  Mbaruku Kheri (ndota) ikiwa ni marudio ya mchezo wao wa kusisimua uliokosa mshindi. 

Mabondia wengine watakaopanda ulingoni ni pamoja na Bondia Adam Yahaya (Baby Edo) atazipiga na Harman Richard, mkongwe Enerst Bujiku (Tyson) atacheza na Shah Kassim,  kukumbushia Enzi za akina Stanley Mabesi , Jocky Hamis mkongwe wa zamani atazipiga na bondia sawa na mwanae  mbena Rajabu.

Wengine ni Issa Omar  atazipiga na Haji Juma wa Tanga, Moro Best atapigana na Shafii Ramadhan, huku Shaban Bodykitongoji akizipiga na Mwinyi Mzengera. 

Mabondia wote wameshasaini mikataba ya makubaliano ya mchezo huo na wameshaingia kambini kujiandaa na mechi zao hizo ambazo zina upinzani wa hali ya juu.

kinachoendelea kwa sasa ni kumalizia mchakato wa ulinzi kutoka Kampuni ya Kiwango Security na jeshi la polisi amblo limeahidi kutoa mchango mkubwa ili kufanikisha pambano hilo.

CHADEMA YAAMUA KUFUNGA MDOMO SAKATA LA ZITTO

 http://www.dar24.com/wp-content/uploads/2012/06/Willibrod-Slaa1.jpg
HATIMAYE Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa mjadala kuhusu viongozi wake waliovuliwa nyadhifa zao kwa madai ya kukisaliti chama umefungwa.

Viongozi waliovuliwa nyadhifa zao ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, aliyevuliwa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitila Mkumbo, aliyevuliwa ujumbe wa Kamati Kuu (CC) na Samson Mwigamba, aliyevuliwa uenyekiti wa Mkoa wa Arusha.

Kauli ya kufunga mjadala huo ulioshika kasi kwa takribani wiki moja sasa, ilitangazwa jana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Dk. Slaa alisema mjadala huo umefungwa, na tayari barua za mashitaka 11 kwenda kwa watuhumiwa zimeshatumwa.

“Nataka niwaambie wana CHADEMA wote wanaotumia mitandao na njia nyingine za mawasiliano kwamba mjadala huo sasa umefungwa, hatutaki kusikia, kuona mwanachama yeyote anauendeleza, lakini tutajibu tu pale itakapoonekana kuna upotoshaji,” alisema Dk. Slaa.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, kazi iliyobaki ni kwa watuhumiwa kujibu mashitaka yao ndani ya siku 14 na hatma yao itajulikana kwenye kikao cha Kamati Kuu (CC).

Dk. Slaa ambaye amepata kuwa mgombea urais wa CHADEMA mwaka 2010 na kutoa upinzani mkali kwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano, alisema kuna mambo mengi mazito ya kujadili kuliko hilo la mzozo wa Zitto na wenzake.

“Tumekumbwa na tatizo la umeme hapa ambao hatujui chanzo, kuna wenzetu wanaendelea kupigwa na kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji, hatuwezi kuendelea na malumbano ambayo hayana tija, CHADEMA ni chama makini na bado kiko imara,” alisema Dk. Slaa.

Kauli ya Dk. Slaa itahitimisha mjadala huo ambao tangu watuhumiwa hao walipotangazwa kuvuliwa madaraka, kumekuwa na majibishano kati ya viongozi wa CHADEMA na watuhumiwa hao.

Mara baada ya mkutano na waandishi wa habari wa kutangaza uamuzi wa kuwavua madaraka viongozi hao, Zitto na Dk. Kitila kwa mara ya kwanza walijibu mapigo katika mkutano wao na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, Zitto na Kitila walitaja sababu walizodai ndizo zimewafanya kuvuliwa nyadhifa zao, ikiwemo suala la ukaguzi wa hesabu za fedha za ruzuku inayotolewa kwa vyama vyenye wabunge, kikiwemo CHADEMA.

Zitto alidai kwa muda mrefu amekuwa akizushiwa kupokea rushwa na kukisaliti chama, na kwamba hatoki ndani ya chama hicho kwani nusu ya maisha yake tangu alipojiunga akiwa na miaka 16, hadi sasa ana miaka 37, maisha yake yapo CHADEMA.

Kutokana na maelezo hayo ya Zitto na Kitila, CHADEMA juzi walilazimika kuitisha mkutano na kudai kuwa viongozi hao waliovuliwa madaraka, walishindwa kusema ukweli mbele ya waandishi wa habari wiki iliyopita wa kile kilichowafanya wavuliwe nafasi zao.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu, alisema Zitto na Dk. Kitila hawakusimamishwa nyadhifa zao kwa masuala ya PAC, uchaguzi wa mwaka 2010, wala kutoshiriki kwenye operesheni za chama au sababu nyingine, na kwamba walitaja sababu hizo ili kupotosha tuhuma zinazowakabili kwa jamii.

“Walichokifanya kina Zitto na Kitila ni “Diversion” (kubadili mwelekeo) wa mashitaka yao yanayotokana na waraka wa kihaini wa mabadiliko, ambao ni kinyume na katiba, kanuni na maadili na itifaki ya chama,” alisema Lissu.

Aliongeza kuwa CHADEMA ina mwongozo wa uchaguzi uliopitishwa na Kamati Kuu, na Zitto na Kitila wanaufahamu ingawa haijulikani ni kwanini wao walienda kinyume na mambo yanayojadiliwa katika Kamati Kuu.

Aidha, Lissu alieleza kuwa Dk. Kitila anapotosha umma kwa kauli yake kuwa Kamati Kuu haina mamlaka ya kumvua nafasi yake ya ujumbe wa Kamati Kuu maana amechaguliwa na Baraza Kuu.

Zanzibar Heroes kuvuna nini leo kwa Ethiopia, Kili Stars kesho!


Zanzibar Heroes wanaotarajiwa kuvaana na Ethiopia leo katika Chalenji
WAKATI mabingwa watetezi Uganda jana wakianza vyema mbio zake za kuwania taji la 14 la Kombe la Chakenji kwa kuilaza Rwanda bao 1-0, huku Sudan ikiisasambua Eritrea kw amabao 3-0, wawakilishi wa Tanzania upande wa visiwani, Zanzibar Heroes leo inatarajiwa kushuka uwanjani kuumana na Ethiopia.
Hilo ni pambano la pili na washindi wa tatu wa michuano iliyopita baada ya awali kuanza mechi za michuano hiyo kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sudan Kusini.
Zanzibar Heroes ambayo inanolewa na kocha Seif Bausi na inayoundwa na wachezaji wengine chipukizi italazimika kupata ushindi wa leo mbele ya Ethiopia iliyoanza na sare ya 1-1 dhidi ya wenyeji Kenya ili kuweka hai nafasi ya kutinga robo fainali.
Ethiopia waliokuwa katika kinyang'anyiro cha kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia 2014 na kutolewa na Nigeria, siyo timu ya kubeza, hivyo vijana wa Zanzibar Heroes wanapaswa kuwa makini katika mechi hiyo ya leo iwapo inataka kudhihirisha kuwa haikuiotea Sudan Kusini walipoilaza mechi iliyopita.
Mechi nyingine inayochezwa leo kwenye mfululizo wa michuano hiyo itakayofikia tamati Desemba 12 ni kati ya Harambee Stars dhidi ya Sudan Kusini.
Kikoi cha Kilimanjaro kitakachoshuka dimbani kesho dhidi ya Somalia
Wawakilishi wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars iliyoanza kwa sare ya 1-1 na mabingwa wa zamani wa Afrika, Zambia yenyewe itashuka kesho kupepetana na Somalia kabla ya wiki ijayo kumalizia mechi zake za kundi B dhidi ya Burundi, ambapo wenyewe kesho wataumana na Zambia 'Chipolopolo'.

Hatuhamishi Kombe la Dunia Brazil-FIFA


SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) imesema halina mpango wa kuhamisha michuano ya Fainali ya Kombe la Dunia 2014 kutoka nchini Brazil ingawa nchi hiyo imepata changamoto katika maandalizi ya michuano hiyo.

Wafanyakazi wawili walipoteza maisha baada ya kuangukiwa na nguzo ambazo ziliharibu uwanja wa Corithians ulio mjini Sao Paulo.

Timu ya taifa ya Brazil inatarajiwa kucheza mechi ya ufunguzi ya Kombe la dunia katika uwanja huo wenye uwezo wa kuwa na watazamaji 65,000.

Vyanzo vya habari vya juu ndani ya Shirikisho hilo vimeendelea kusisitiza kuwa hakuna mbadala kutokana na kutokea kwa ajali hiyo.

Brazil ilikiri kuwa inafanya jitihada za kumaliza ujenzi wa viwanja 12 kwa ajili ya michuano hiyo, sita kati ya hivyo ipo tayari kwa ajili ya michuano ya kombe la shirikisho.

Ajali iliyotokea siku ya Jumatano ni ya tatu kusababisha kifo katika viwanja vitakavyopigiwa kipute cha kombe la dunia. Wafanyakazi wengine wawili walipoteza maisha kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Uchunguzi umeanza hii jana kubaini chanzo cha ajali mjini Sao Paulo.

Askari abambwa akifanya ngono na mahabusu chooni

Kim akiburuzwa na wezake kwa kosa la kufumaniwa mahabusu chooni
ASKARI Polisi mmoja mwenye cheo cha kati nchini China, Yun Kim anashikiliwa katika kituo kimoja kidogo akituhumiwa kufanya mapenzi na mahabusu mwanamke ambaye ni mke wa askari mwenzake.

Inadaiwa askari huyo alikumbwa na mkasa huo katika kituo kidogo cha polisi katika kitongoji cha Chau, mjini Beijing, ambapo inadaiwa siku hiyo Kim alikuwa zamu ya usiku pamoja na maaskari wengine, ambapo pia mahabusu huyo alikuwa kituoni hapo kwa kosa la utapeli.

Mwanamke huyo ambaye ni mke wa askari ambaye jina lake limehifadhiwa, anadaiwa kuletwa kituoni hapo kwa kosa la kujipatia dola 200 kutoka kwa mama mmoja waliokuwa wakifanya biashara pamoja.

Kutokana na kushindwa kumlipa mama aliyekuwa akifanya naye biashara, mke huyo wa askari alijikuta akifikishwa kituoni akisubiri kufunguliwa mashtata siku iliyofuata.

Imeelezwa kuwa, mama huyo hakutaka mume wake ambaye ni askari polisi kwenye kituo kingine afahamu kama ana kesi ya utapeli, hivyo aliamua kuongea na askari huyo.

Mke huyo wa askari anadai kukiri kumtapeli mama huyo, hivyo alikuwa tayari kwenda kumchukulia pesa hizo nyumbani kwake.

Afande huyo anadaiwa kumshawishi kimapenzi mama huyo ili amruhusu kwenda nyumbani kuchukua pesa anazodaiwa, lakini sharti pia waongozane wote.

Kwa lengo la kuepuka aibu ya kujulikana na mume wake kama amefikishwa polisi kwa kesi ya utapeli, mama huyo mahabusu alikubali kufanya mapenzi kituoni hapo na askari huyo.

Akisimulia zaidi tukio hilo,  askari mwenzake aliyekuwa zamu, alisema aliwafuma wawili hao kwenye choo cha kike wakifanya mapenzi.

Ilikoanzia ni kwamba, walipanga mchezo mahabusu huyo aombe ruhusa kwenda chooni na ndipo kamanda naye akajisogeza chooni kwa siri na kuanza kufanya mapenzi.

Hata hivyo, askari aliyewashtukia baada ya kubaini muda mrefu ukipita bila askari mwenzake aliyemsindikiza chooni kurudi, aliamua kufuatilia na kuwakuta wakiburudika.
Askari huyo pamoja na mwanamke huyo, wanakabiliwa na kesi ya kufanya ngono eneo la kazi, huku mwanamke huyo akiendelea kukabiliwa na kesi yake ya utapeli.

IDFA yajitosa gogoro la Simba




Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage
Katibu Mkuu w IDFA, Daud Kanuti (aliyesimama kushoto)
UONGOZI wa Chama cha Soka Wilaya ya Ilala (IDFA) umezitaka pande mbili zinazolumbana ndani ya klabu ya Simba kukaa meza moja na kumaliza tofauti zao kwa manufaa ya klabu yao badala ya kuendeleza mgogoro usiokuwa na faida.
Aidha uongozi huo umesema mtindo wa kupinduana umepitwa na wakati na wanachama na viongozi wa Simba wanapaswa kulitambua hilo na kushikamana ili kuijenga timu yao katika usajili wa dirisha dogo ili wafanye vyema kwenye duru la pili la Ligi Kuu na kusubiri Uchaguzi Mkuu wao utakaofanyika Mei mwakani.
Akizungumza na MICHARAZO jana, Katibu Mkuu wa IDFA, Daud Kanuti, alisema chama chao kama walezi wa klabu za soka wilaya ya Ilala kinasikitishwa na hali inayoendelea Simba na kuwataka wadau wa klabu kumaliza kistaarabu mzozo wao kwa mustakabali wa klabu yao.
Kanuti alisema bila kujali nani mwenye haki katika mzozo unaoendelea, alisema ni vyema pande zinazosigana kukaa pamoja na kumaliza tofauti kwa ajili ya kujenga umoja na mshikamani Simba na kufanya usajili makini kwa ajili ya duru la pili la ligi kuu badala ya kutumia muda mwingi kulumbana.
"Haya malumbanmio yanayoendelea hayaijengi Simba, IDFA tunawaaasa wakae na kumaliza tofauti zao kwa manufaa ya klabu yao, mambo ya kupinduana na kutunushiana misuli ili kuendeleza migogoro yamepitwa na wakati, wadau waangalie mgogoro unaeondelea una manufaa gani kwa timu yao," alisema.
Alisema kuendelea kwa mzozo baina ya wale wanaounga mkono kupinduliwa kwa Mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage na wale wanaoumuunga mkono kunaweza kuwa mtihani kwa klabu yao katika ushiriki wake wa duru la pili la ligi kuu na pengine kufanya  vibaya na kuzidisha mgogoro.
"Bahati nzuri uchaguzi mkuu wa Simba upo karibuni, ni Mei mwakani, nadhani wanasimba wavumiliane na kusubiri kuchaguana badala ya kupinduana, pia kwa hivi sasa katiba zinataka viongozi wakae madarakani mpaka vipindi vyao viishe kabla tu kwa dharura maalum zinazokubalika," alisema Kanuti.

Fainali za EBSS kipwanipwani leo Escape 2

http://api.ning.com/files/Vkr5AOZtf8IZ*LagrRC25iuMgDMtqJBcY*2rC84HA-D2knVsJ1IRqqnYPVSh4FaKmVYZCkbH2bxVmkvhjegztCTP06*wPYSO/EBSSFINALEPROMOPOSTER1.jpg

FAINALI ya shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Epiq Bongo Star Search ambalo linafanyika leo katika ukumbi wa Escape 2 jijini Dar es Salaam litapambwa pamoja na burudani nyingine, wakali wa miondoko ya pwani wanaotamba sasa nchini Snura na Shaa.
Snura amejizolea umaarufu nchi nzima kutokana na singo yake ya 'Majanga' katika kipindi ambacho Shaa anakuja juu kutokana na wimbo wake mpya wa 'Sugua Gaga' ambazo zote zinachezeka kwa kuzungusha kiuno zaidi.
Akizungumza na MICHARAZO jana, jaji mkuu wa shindano hilo Ritta Poulsen alisema mbali ya Snura na Shaa, wasanii wengine watakaotoa burdani ni Barnaba, Komandoo, Msechu na 'live' bendi.
Alisema safari hii onyesho hilo litakuwa la aina yake kutokana na kujiandaa vya kutosha ili kuhakikisha wanawapa burudani nzuri mashabiki wa shindano hilo ambalo hufanyika kila mwaka.
Mshindi atazawadiwa sh. milioni 50 pamoja na kuingia mkataba wa mwaka mmoja na wadhamini wakuu wa shindano hilo, kampuni ya simu za mkononi Zantel, alisema Rita.
Mshindi huyo pia atasaini mkataba wa jinsi gani atazitumia fedha za zawadi ambazo atapewa na waandaaji wa shindano hilo, alisema Rita ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Bench Mark.
"Tumeamua kufanya hivyo ili kuhakikisha mshindi anazitumia vizuri fedha ambazo atazipata mara baada ya kuibuka mshindi katika shindano hilo," alisema.
Naye Barnaba alisema amejiandaa kutoa burudani safi kwa mashabiki watakahudhuria onyesho hilo, ikiwemo kutambulisha nyimbo yake mpya ya 'Jasho la Mnyonge'.