Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage |
Katibu Mkuu w IDFA, Daud Kanuti (aliyesimama kushoto) |
Aidha uongozi huo umesema mtindo wa kupinduana umepitwa na wakati na wanachama na viongozi wa Simba wanapaswa kulitambua hilo na kushikamana ili kuijenga timu yao katika usajili wa dirisha dogo ili wafanye vyema kwenye duru la pili la Ligi Kuu na kusubiri Uchaguzi Mkuu wao utakaofanyika Mei mwakani.
Akizungumza na MICHARAZO jana, Katibu Mkuu wa IDFA, Daud Kanuti, alisema chama chao kama walezi wa klabu za soka wilaya ya Ilala kinasikitishwa na hali inayoendelea Simba na kuwataka wadau wa klabu kumaliza kistaarabu mzozo wao kwa mustakabali wa klabu yao.
Kanuti alisema bila kujali nani mwenye haki katika mzozo unaoendelea, alisema ni vyema pande zinazosigana kukaa pamoja na kumaliza tofauti kwa ajili ya kujenga umoja na mshikamani Simba na kufanya usajili makini kwa ajili ya duru la pili la ligi kuu badala ya kutumia muda mwingi kulumbana.
"Haya malumbanmio yanayoendelea hayaijengi Simba, IDFA tunawaaasa wakae na kumaliza tofauti zao kwa manufaa ya klabu yao, mambo ya kupinduana na kutunushiana misuli ili kuendeleza migogoro yamepitwa na wakati, wadau waangalie mgogoro unaeondelea una manufaa gani kwa timu yao," alisema.
Alisema kuendelea kwa mzozo baina ya wale wanaounga mkono kupinduliwa kwa Mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage na wale wanaoumuunga mkono kunaweza kuwa mtihani kwa klabu yao katika ushiriki wake wa duru la pili la ligi kuu na pengine kufanya vibaya na kuzidisha mgogoro.
"Bahati nzuri uchaguzi mkuu wa Simba upo karibuni, ni Mei mwakani, nadhani wanasimba wavumiliane na kusubiri kuchaguana badala ya kupinduana, pia kwa hivi sasa katiba zinataka viongozi wakae madarakani mpaka vipindi vyao viishe kabla tu kwa dharura maalum zinazokubalika," alisema Kanuti.
No comments:
Post a Comment