STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 9, 2013

Ramadhani Shauri kuwania taji la Dunia

Ramadhani Shauri

BINGWA wa Afrika anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Ngumi za Kulipwa la IBF, Ramadhani Shauri ameteuliwa kuwania ubingwa wa vijana wa dunia wa IBF.
Kwa mujibu wa taarifa ya IBF/USBA, inasema kuwa bingwa huyo wa uzito wa Feather atawania taji hilo la dunia katika uzito wa light kwa vijana chini ya umri wa miaka 25.
Shauri alitwaa taji hilo la Afrika kwa kumchapa Mganda, Sunday Kizito katika pambano laio lililofanyika mwishoni mwa mwaka jana jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo ya IBF/USBA iliyotolewa na rais wa shirikisho hilo, Onesmo Ngowi ni kwamba hiyo ni fursa nzuri kwa Mtanzania huyo kuweza kujitangaza kimataifa iwapo atafanikiwa kutwaa taji hilo la dunia la vijana.
Inaelezwa IBF iliamua kumpatia Shauri nafasi ya kugombea ubingwa huo wa vijana baada ya kuangalia mkanda wa video wa pambano lake la ubingwa wa Afrika na kuridhika kuwa anaweza kushindania ubingwa huo wa vijana,
Mabondia wengi wa Marekani waliokuja kuwa mabingwa wa dunia na kuweza kupata pesa nyingi walianza kuwa mabingwa wa dunia kwa vijana hivyo kuweza kupanda chati kwenye viwango vya IBF.
Mifano wa mabondia hao ni akina Bernard Hopkins, Floyd Maywealther na Oscar De la Hoya.
Iwapo Shauri atashinda na kuwa bingwa wa dunia upande wa vijana atakuwa kwenye macho ya mapromota wakubwa duniani kama kina Don King, Bob Arum na wengine wengi.
Pia itakuwa ni mara ya kwanza kwa historia ya ngumi nchini kwa Mtanzania kutwaa taji kubwa kati ya manne duniani ya IBF, WBA, WBO na WBC.
Kadhalika inaeleza kushinda kwa Mtanzania huyo kutatoa fursa kwa nchi ya anzania kujitangaza kibiashara na utalii duniani.

Kikosi cha Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Simba

SIMBA, OLJORO HAPATOSHI LEO ARUSHA, AZAM ZAMU YAO KESHO

LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya 16 leo kwa mechi kadhaa ambapo jijini Arusha, mabingwa watetezi Simba itavaana na wenyeji wao JKT Oljoro.
Mechi hiyo namba 129 itafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, huku Simba ikiingia na kumbukumbu ya sare katika mechi yake iliyopita dhidi ya JKT Ruvu wakati wenyeji wao wakiwa wameshinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.
Simba italazimika kupata ushindi ili kufufua mbio zao za kuwania taji hilo kwa mara ya pili mfululizo ambalo linawindwa na timu za Yanga iliyopo kileleni na Azam wanaoshika nafasi ya pili ambao kesho watakuwa wageni wa Mtibwa Sugar mjini Manungu, Morogoro.

Mechi nyingine zinazochezwa leo Jumamosi ni pamoja na kivumbi kitakachowaka uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, wakati wenyeji  Kagera Sugar na Mgambo Shooting zitaonyeshana kazi katika pambano litakaloamuliwa na mwamuzi Amon Paul kutoka Musoma, Mara.
Toto Africans baada ya kufanya vibaya katika mechi tatu zilizopita ugenini imerejea nyumbaji jijini Mwanza itakapoumana na Coastal Union ya Tanga katika mchezo utaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Mchezaji wa kimataifa wa Coastal Union kutoka Brazil, Gabriel  Barbosa

Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union, Nassor BinSlum, aliweka wazi kwamba huenda mchezaji wao wa kimataifa kutoka Brazil, Gabriel Barbosa, ambaye ITC yake imeshapatikana atashuka dimbani katika pambano hilo.
Mchezaji huyo alikwama karibu duru zima la msimu huu kuichezea Coastal kwa kukosa hati hiyo, lakini Binslum kaithibitishia MICHARAZO kwamba kila kitu sasa kipo shwari na wapo tayari kumtumia mchezaji wao huyo.
Mwamuzi Simon Mberwa kutoka mkoani Pwani ndiye atakayechezesha mechi kati ya wenyeji Tanzania Prisons na African Lyon ambayo imepata huduma za kocha mpya Salum Bausi kutoka Zanzibar. Hiyo itakuwa mechi ya kwanza kwa Bausi kuiongoza timu katika VPL.
Maofisa wengine wa mechi hiyo ni mwamuzi msaidizi namba moja Abdallah Rashid, mwamuzi msaidizi namba mbili Abdallah Mkomwa wote kutoka Pwani wakati mwamuzi wa mezani ni John Kanyenye wa Mbeya. Kamishna wa mechi hiyo ni Rashid Rwena kutoka Ruvuma.
Mechi kati ya Mtibwa Sugar na Azam iliyokuwa ichezwe kesho imesogezwa mbele kwa siku moja ambapo sasa itafanyika Jumapili katika Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro.

Kikosi cha Azam

Polisi Tabora wajipa moyo

Mwinyimadi Tambaza (aliyesimama)

LICHA ya kuanza vibaya mechi za Ligi Daraja la Kwanza kwa kupokea kipigo cha bao 1-0 toka kwa Rhino Rangers, Kocha Mkuu wa timu ya Polisi Tabora, Mwinyimadi Tambaza ametamba hajakatishwa tamaa katika mikakati yake ya kuinusuru timu hiyo.
Kocha huyo alinyakuliwa na Polisi Tabora hivi karibuni kwa ajili ya duru la pili la ligi hiyo iliyoanza wiki iliyopita na kuisaidia kuiongoza kufanya vema katika mechi zao za kirafiki ikiwemo kuibana Kagera Sugar na kuzinyuka timu za Tabora Combain na Reli.
Hata hivyo katika mechi yake ya kwanza walilazwa na Rhino na juzi alitarajiwa kuiongoza tena katika pambano lao la pili dhidi ya Polisi Dodoma mechi linalotarajiwa kupigwa uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.
Tambaza alisema licha ya kwamba kipigo hicho kimetibua mipango yao ya kuvuna pointi za kutosha katika duru hilo, lakini bado wanaamini Polisi Tabora itasalia ligi hiyo kwa kushinda mechi zinazofuatia mbele yao.
"Hatujakatishwa tamaa na kipigo cha Rhino, ilitokea kama bahati mbaya kutokana na vijana wangu kujisahau lakini tumejipanga kufanya vema kwa mechi zetu zijazo, naomba mashabiki wa Polisi Tabora wasikate tamaa kwani kazi ndiyo kwanza imeanza," alisema.
Kocha huyo alisema wamerekebisha makosa yaliyowaponza mbele yua Rhino na kwamba wamepania kuanzia mechi yao ya leo kutopoteza pointi yoyote ili wamalize duru hilo katika nafasi nzuri hata kama hawatapanda Ligi Kuu msimu ujao.

Sikinde yapeleka Jinamizi lake Sauti za Busara

Waimbaji wa Mlimani Park, Hassan Kunyata, Abdallah Hemba na Hassan Bichuka wakiwajibika

BENDI kongwe ya muziki wa dansi, Mlimani Park 'Sikinde' inatarajiwa kuondoka jijini Dar keshokutwa kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kushiriki tamasha la kimataifa la muziki la Sauti za Busara litakalofanyika visiwani humo kuanzia Alhamisi.
Katibu wa Sikinde, Hamis Milambo aliiambia MICHARAZO kuwa, bendi yao ni miongoni mwa makundi ya muziki na wasanii walioalikwa kushiriki tamasha hilo linalofanyika kila mwaka visiwani Zanzibar.
Alisema bendi yao imejiandaa kwenda kutoa burudani kabambe sambamba na kujitangaza kupoitia tamasha hilo ambalo hushirikisha wasanii na makundi ya muziki kutoka nchi mbalimbali za Kiafrika.
"Bendi yetu imeteuliwa kushiriki tamasha la kimataifa la muziki la Sauti za Busara na tunatarajiwa kuondoka Jumanne kuelekea Zanzibar tukiwa tumekamilika na kutaka kuwaonyesha makundi mengine kwamba sisi ndiyo Mabingwa wa dansi," alisema.
Sikinde itaungana na wasanii wengine wa Tanzania katika tamasha hilo litakalofanyikia eneo la Ngome Kongwe, akiwamo Peter Msechu, Msafiri Zawose & Sauti Band, Super Maya Baikoko, Lumumba Theatre Group na Culture Musical Club.
Makundi mengine yatakayoshiriki tamasha hilo litakalomalizika Februari 17 ni Cheikh Lo (Senegal), Khaira Arby (Mali), Comrade Fatso na Chabvondoka (Zimbabwe), Atongo Zimba (Ghana), N'Faly Kouyaté (Guinea), Nathalie Natiembe (Reunion), Nawal & Les Femmes de la Lune na (Comoros/Mayotte).
Pia wamo Wazimbo (Msumbiji), The Moreira Project (Msumbiji/Afrika Kusini), Owiny Sigoma Band (Kenya/UK), Mokoomba (Zimbabwe), Mani Martin (Rwanda), Burkina Electric (Burkina Faso/USA) na Sousou & Maher Cissoko (Senegal/Sweden).
Kwa mujibu wa waandaaji wa tamasha hilo pia litajumuisha filamu za muziki wa Kiafrika, kumbukumbu, video za muziki na maonesho ya moja kwa moja, yote yakilenga kukuza utajiri na utofauti wa muziki wa Kiafrika.

Sadikina kuuza sura mara mbili

Msanii Sadikina Mussa 'Vicky'

MUIGIZAJI wa filamu anayekuja juu nchini, Sadikina Mussa 'Vicky' anatarajiwa kuuza sura katika filamu mbili tofauti za 'Hiari Yangu' na 'My Heart'.
Akizungumza na MICHARAZO, Sadikina alisema filamu hizo zilizowashirikisha wasanii mbalimbali wakiwemo nyota zimeshakamilika na zitaingizwa sokoni hivi karibuni.
Mwanadada huyo, alisema filamu zote zinahusisha masuala ya mapenzi lakini katika mitazamo tofauti na kwamba amezitendea haki kutokana na kiu aliyonayo ya kujitangaza zaidi.
Alisema katika filamu ya Hiari Yangu amecheza kama nyumba ndogo ya Kobra ambaye ndiye mhusika mkuu bila kujua kama ni mume wa shoga yake kipenzi na kuibua ugomvi uliosababisha uhasama baina yake na shogaye huyo.
"Ni moja ya kazi murua, inasisimua na ipo katika kiwango cha hali juu kama ilivyo 'My Heart'," alisema Sadikina shabiki mkubwa wa Yanga na Manchester United.

Sadikina Mussa 'Vicky'

Baby Madaha afyatua mpya akijiandaa kwenda kuwania tuzo Nigeria

Baby Madaha katika pozi

WAKATI filamu yake ya 'Ray of Hope' ikiteuliwa kwenda kuwania tuzo ya kimaataifa za African Magic nchini Nigeria, msanii nyota nchini wa filamu na muziki, Baby Madaha anajiandaa kupakua filamu mpya   iitwayo 'Tatakoa'.
Akizungumza na MICHARAZO, Madaha alisema filamu hiyo imekamilika na ipo katika hatua za kuingizwa sokoni ikiwa imeshirikiana na wasanii kadhaa nyota nchini akiwamo Jumanne Kihangale 'Mr Tues'.
Madaha aliwataja wasanii wengine walioshiriki filamu hiyo inayozungumzia masuala ya mapenzi, uchawi na mauaji ni Salma Jabu 'Nisha', Frola Mvungi, Mariam Mndeme na wengineo.
"'Tatakoa' ni filamu ya aina yake imesheheni uchawi, mapenzi na mauaji ndani yake, yaani nimekuja kama Angelina Jolie," Baby Madaha alitamba.
Alisema wakati filamu hiyo ikiwa njiani, kazi yake iliyonyakua tuzo za ZIFF-2012 ya 'Ray of Hope' imeteuliwa kuwania tuzo za filamu za kimataifa za African Magic ambazo zitafanyika mwezi ujao nchini Nigeria.
Madaha alisema amefurahi kuona filamu hiyo ikiziangusha nyingine za wasanii wakongwe nchini na Afrika Mashariki katika mchujo wa kupenya kuwania tuzo hizo maarufu Afrika na duniani kwa ujumla.
Msanii alisema kwa sasa anajiandaa kwa ajili ya safari hiyo ya kwenda Nigeria, akiwaomba Watanzania wamuombee aweze kuibuka kidedea katika tuzo hizo.

Baby Madaha katika pozi jingine matata

Warembo wa Utalii 'kutalii' mikoa sita

Baadhi ya warembo wa Miss Utalii Tanzania wakiwa katika pozi

Warembo wa Miss Utalii Tanzania katika pozi

WAREMBO wanaojiandaa na kinyang'anyiro cha Miss Utalii Tanzania, wanatarajiwa kuanza ziara ndefu ya kutalii katika Hifadhi na vivutio vingine vya utalii katika miji mitano tofauti.
Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo 'Chipps' alisema warembo hao wanaanza ziara hiyo wiki ijayo kwa kuitembelea mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Lindi, Pwani na Mtwara.
Chipungahelo alisema warembo hao watatalii na kujifunza mambo mbalimbali kabla ya kinyang'anyiro chao katika hifadhi za taifa za Mikumi, Udzungwa, Saadan na Selous, pia wakitembele vivutio vya kitalii kama maeneo ya kihistoria ya Bagamoyo, Amboni, Kijiji cha Makumbusho, Makumbusho ya Taifa na Pugu Sekondari.
"Pia watatembelea maeneo ya fukwe ya Kigamboni, Soko la Kimataifa la Magogoni, Uwanja wa Taifa,  Uwanja wa Ndege wa J.K.Nyerere, Soko la Kariakoo, mashule kadhaa za Sekondari na Msingi na kutembelea Manispaa zote za mkoa wa Dar es Salaam kukutana na viongozi wakuu wa wilaya, mikoa na wabunge wake," alisema.
Warembo hao wanatarajiwa kuchuana katika shindano la kusaka kisura wa mwaka 2012-2013 litakalofanyika jijini Dar es Salam mwishoni mwa mwezi huu.