Baadhi ya warembo wa Miss Utalii Tanzania wakiwa katika pozi |
Warembo wa Miss Utalii Tanzania katika pozi |
WAREMBO wanaojiandaa na kinyang'anyiro cha Miss Utalii Tanzania, wanatarajiwa kuanza ziara ndefu ya kutalii katika Hifadhi na vivutio vingine vya utalii katika miji mitano tofauti.
Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo 'Chipps' alisema warembo hao wanaanza ziara hiyo wiki ijayo kwa kuitembelea mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Lindi, Pwani na Mtwara.
Chipungahelo alisema warembo hao watatalii na kujifunza mambo mbalimbali kabla ya kinyang'anyiro chao katika hifadhi za taifa za Mikumi, Udzungwa, Saadan na Selous, pia wakitembele vivutio vya kitalii kama maeneo ya kihistoria ya Bagamoyo, Amboni, Kijiji cha Makumbusho, Makumbusho ya Taifa na Pugu Sekondari.
"Pia watatembelea maeneo ya fukwe ya Kigamboni, Soko la Kimataifa la Magogoni, Uwanja wa Taifa, Uwanja wa Ndege wa J.K.Nyerere, Soko la Kariakoo, mashule kadhaa za Sekondari na Msingi na kutembelea Manispaa zote za mkoa wa Dar es Salaam kukutana na viongozi wakuu wa wilaya, mikoa na wabunge wake," alisema.
Warembo hao wanatarajiwa kuchuana katika shindano la kusaka kisura wa mwaka 2012-2013 litakalofanyika jijini Dar es Salam mwishoni mwa mwezi huu.
No comments:
Post a Comment