STRIKA
USILIKOSE
Wednesday, November 27, 2013
Arsenal, Milan zaua, Chelsea, Barca zafa Ulaya
Jack Wilshere alifunga bao la pili la timu yake ya Arsenal |
Neymar akijaribu kuipigania timu yake isife mbele ya Ajax |
Muuaji wa Chelsea, Mohammed Salah akishangilia bao lake pekee usiku wa jana |
Arsenal iliishinda Olympique Marseille kwa mabao 2-0 ikiwa nyumbani uwanja wa Emirates mabao yote yakifungwa na Jack Wilshere.
Wilshere alifunga bao la kwanza katika sekunde 29 tu ya mchezo huo kabla ya kuongeza jingine katika kipindi cha dakika ya 65 na kuwafanya vinara hao wa England kubaki kileleni na pointi 12 ikiwaacha Borussia Dotmund iliyopinyuka Napoli 3-1 na wapinzani wao wakiwa na pointi 9 kila mmoja.
Barcelona ikiwa ugenini ilijikuta ikiangukia kua kwa kulazwa mabao 2-1 na wenyeji wao Ajax, huku Chelsea nayo ikilala ugenini kwa bao 1-0 katika mchezo mwingine uliokuwa mkali.
Barca walijikuta wakitanguliwa kufungwa mabao yote mawili na wenyeji wao kupitia kwa Hoesen aliyefunga katika dakika ya 18 na 41 na kwenda mapumziko wakiwa nyuma.
Kipindi cha pili Barcelona walifanikiwa kujitutumua na kupata baop la kufutia machozi kupitia mkwaju wa penati iliyofungwa na Xavi dakika ya 49 baada ya Veltman kufanya madhambi yakiyomtoa nje na kuipa pengo timu yake ya Ajax.
Chelsea nayo ilitunguliwa bao 1-0 na Basel, huku AC Milan ikizinduka na kuilaza Celtic kwa mabao 3-0, Mario Balotelli akifunga bao la tatu, nazo timu za Zenit na Atletico Madrid zikishindwa kutambiana na kutoka sare ya bao 1-1 sawa na ilivyokuwa kwa Porto dhidi ya Vienna.
Nazo timu za Schalke 04 iliyokuwa ugenini na Bucharest ya Romania zilishindwa kufungana katika mecho mwingine mkali.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena usiku wa leo kwa michezo ya makundi manne mengine kukamilisha raundi ya tano ya makundi hayo kabla ya kusalia mechi mmoja za kukamilisha mechi za makundi.
Subscribe to:
Posts (Atom)