KOCHA Mkuu Mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ameanza mambo yake baada ya kutangaza kikosi cha wachezaji 26 akimjumuisha kipa wa Yanga Ally Mustafa 'Barthez'.
Mkwasa alitangaza kikosi hicho kilichowajumuisha pia mshambuliaji wa JKT Ruvu Samuel Kamuntu, huku pia akitangaza jopo lake la Benchi la Ufundi atakalosimamia akisaidiana na Hemed Morocco.
Wachezaji walioitwa kwa ajili ya pambano la marudiano la kuwania kucheza fainali za Chan 2016 dhidi ya Uganda The Cranes ni; Makipa: Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ally (Azam), Ally Mustafa “Barthez” (Yanga).
Walinzi:
Shomari Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohamed Hussein
“Tshabalala” (Simba), Haji Mwinyi (KMKM), Nadir Haroub “Cannavaro”
(Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Hassan Isihaka (Simba), Aggrey Morris
(Azam).
Viungo: Jonas Mkude (Simba), Abdi Banda (Simba), Salum Telela (Yanga), Frank Domayo (Azam).
Mawinga: Saimon Msuva (Yanga), Said Ndemla (Simba), Deus Kaseke (Mbeya City), Ramadhan Singano “Messi” (Simba).
Washambuliaji: John Bocco (Azam), Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Ame Ally (Mtibwa Sugar).
Wachezaji
Juma Abdul (Yanga), Mudathir Yahya (Azam) na Samwel Kamuntu (JKT Ruvu)
wameitwa kama wachezaji wa akiba katika kikosi cha timu ya Taifa
kinachoingia kambini kesho.
Katika hatua nyingine Mkwasa
ametangaza benchi la ufundi la Taifa Stars, kocha msaidizi Hemed
Morocco, kocha wa magolikipa Peter Manyika, Mshauri wa timu Abdallah
Kibadeni, mtunza vifaa Hussein Swedi Gaga huku mratibu wa timu akiwa ni
Alhaj Ahmed Mgoyi.
Kamati ya tiba ya TFF itapendekeza majina ya daktari wa timu na mchua misuli watakaoungana na kambi ya Taifa Stars
STRIKA
USILIKOSE
Wednesday, June 24, 2015
Jackson Mayanja atua Coastal, Kabange amfuata Tanga
Kocha Jackson Mayanja akiweka dole gumba katika mkataba wa kuifundisha Coastal msimu ujao anayemuangalia ni Katibu Mkuu, Kassim El Siagi |
MABINGWA
wa Ligi kuu soka Tanzania bara mwaka 1988,Coastal Union,Wagosi wa Kaya imeingia
mkataba wa miaka miwili na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Kagera
Sugar, Jackson
Mayanja ambaye
ni raia wa Uganda
kuifundisha timu ya Coastal Union katika msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania
Bara itakayoanza Mwezi Agosti mwaka huu .
Utiliaji wa saini wa Kocha huyo ulifanyika (leo)jana
mjini hapa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa timu ya Coastal Union
akiwemo Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Albert Peter na Katibu Mkuu wa timu
hiyo,Kassim El Siagi.
Akizungumza
baada ya kumalizika zoezi hilo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema
kuwa kutokana na umahiri aliokuwa nao kocha huyo wanaimani kubwa ataipa
mafanikio timu hiyo hasa katika harakati za kuhakikisha inafanya vizuri ligi
kuu msimu ujao.
Amesema kuwa
uwezo wa Kocha huyo utaleta matumaini makubwa ya mafanikio hasa ukizingatia ni
kocha mwenye uwezo mzuri wa kufundisha na kuzipa mafanikio timu hivyo tunaamini
kuja wake kwetu itakuwa chachu katika maendeleo.
Mayanja
ambaye aliwahi kuzifundisha timu za soka Kiyuvu FC ya Rwanda,Timu ya Mamlaka ya
Mapato nchini Uganda (URA),Vipers FC ya
Bunamwaya na KCC ya Uganda amesema kutua
kwenye timu hiyo kumpa faraja kubwa hivyo atahakikisha anatoa mchango wake
kwenye kuipa mafanikio.
Amesema kuwa
mipango yake mikubwa ni kuhakikisha timu hiyo inang’ara katika michuano ya Ligi
kuu msimu ujao ikiwemo kubadili aina ya mchezo wa timu hiyo ili iweze kupata
mafanikio kwa kuweka umoja baina ya wachezaji mashabiki, wanachama na wapenzi.
Amesistiza
pia umuhimu wa mshikamano baina ya wapenzi,wanachama na viongozi ili kuiwezesha
timu hiyo kuchukua Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao kwani dhamira yake ni kutaka
kuona timu hiyo inang’ara kwenye medani za kitaifa na kimataifa.
Katika hatua nyingine aliyekuwa msaidizi wa Mayanja ndani ya Kagera Sugar, Mrage Kabange ameamua kumfuata bosi wake mjini Tanga kwa kusaini African Sports.
Kabange amechukuliwa na Wana Kimanumanu waliopanda Ligi Kuu msimu ujao baada ya kutemeshwa kazi kwa Wakata Miwa mara baada ya msimu wa 2014-2015 kumalizika Mei 9 mwaka huu.
Subscribe to:
Posts (Atom)