Kocha Jackson Mayanja akiweka dole gumba katika mkataba wa kuifundisha Coastal msimu ujao anayemuangalia ni Katibu Mkuu, Kassim El Siagi |
MABINGWA
wa Ligi kuu soka Tanzania bara mwaka 1988,Coastal Union,Wagosi wa Kaya imeingia
mkataba wa miaka miwili na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Kagera
Sugar, Jackson
Mayanja ambaye
ni raia wa Uganda
kuifundisha timu ya Coastal Union katika msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania
Bara itakayoanza Mwezi Agosti mwaka huu .
Utiliaji wa saini wa Kocha huyo ulifanyika (leo)jana
mjini hapa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa timu ya Coastal Union
akiwemo Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Albert Peter na Katibu Mkuu wa timu
hiyo,Kassim El Siagi.
Akizungumza
baada ya kumalizika zoezi hilo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema
kuwa kutokana na umahiri aliokuwa nao kocha huyo wanaimani kubwa ataipa
mafanikio timu hiyo hasa katika harakati za kuhakikisha inafanya vizuri ligi
kuu msimu ujao.
Amesema kuwa
uwezo wa Kocha huyo utaleta matumaini makubwa ya mafanikio hasa ukizingatia ni
kocha mwenye uwezo mzuri wa kufundisha na kuzipa mafanikio timu hivyo tunaamini
kuja wake kwetu itakuwa chachu katika maendeleo.
Mayanja
ambaye aliwahi kuzifundisha timu za soka Kiyuvu FC ya Rwanda,Timu ya Mamlaka ya
Mapato nchini Uganda (URA),Vipers FC ya
Bunamwaya na KCC ya Uganda amesema kutua
kwenye timu hiyo kumpa faraja kubwa hivyo atahakikisha anatoa mchango wake
kwenye kuipa mafanikio.
Amesema kuwa
mipango yake mikubwa ni kuhakikisha timu hiyo inang’ara katika michuano ya Ligi
kuu msimu ujao ikiwemo kubadili aina ya mchezo wa timu hiyo ili iweze kupata
mafanikio kwa kuweka umoja baina ya wachezaji mashabiki, wanachama na wapenzi.
Amesistiza
pia umuhimu wa mshikamano baina ya wapenzi,wanachama na viongozi ili kuiwezesha
timu hiyo kuchukua Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao kwani dhamira yake ni kutaka
kuona timu hiyo inang’ara kwenye medani za kitaifa na kimataifa.
Katika hatua nyingine aliyekuwa msaidizi wa Mayanja ndani ya Kagera Sugar, Mrage Kabange ameamua kumfuata bosi wake mjini Tanga kwa kusaini African Sports.
Kabange amechukuliwa na Wana Kimanumanu waliopanda Ligi Kuu msimu ujao baada ya kutemeshwa kazi kwa Wakata Miwa mara baada ya msimu wa 2014-2015 kumalizika Mei 9 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment