PAMBANO la Ligi Kuu ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa jana
(Machi 2 mwaka huu) imeingiza sh. 20,610,000 ambapo kila klabu ilipata mgawo wa
sh. 4,402,492 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
3,143,898.31.
Katika mchezo huo Simba iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 na kuendelea kusalia kwenye nafasi ya nne ya msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Azam yenye pointi 40 na kufuatiwa na Yanga yenye 38 kisha Mbeya City inayokamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 36.
Katika hatua nyingine mechi ya
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati ya Mlale JKT na Lipuli iliyokuwa ichezwe Machi
9 mwaka huu Uwanja wa Majimaji mjini Songea sasa itachezwa Machi 5 mwaka huu.
Bodi ya
Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko hayo ili kuipunguzia gharama timu
ya Lipuli ya Iringa ambayo jana (Machi 2 mwaka huu) ilicheza mechi mjini Songea
dhidi ya Majimaji.
No comments:
Post a Comment