BINGWA wa uzito wa juu wa WBC raia wa Ukraine,
Vitali Klitschko anataka kufuata nyayo za bondia mwenzake, Manny Pacquiao wa
Ufilipino kwa kujiingiza kwenye siasa, ila yeye anautaka Urais wa nchi hiyo
kwenye uchaguzi wa 2015.
Manny Pacquiao pamoja na kuwa mbunge lakini pia
anajishughulisha siasa ni mbunge wa Bunge la Ufilipino, hali ambayo
imemvutia Klitschko ambaye mwezi Agosti alisema lengo kubwa ni kuifanya Ukraine
kuwa nchi ya kisasa yenye maisha ya kiulaya.
Anasema ataamua na watu wenye mtazamo mmoja, ndoto zinazofanana na kuingia kwenye siasa na kutokea ndani kufanya mabadiliko.
Bondia huyo mwenye elimu ya udaktari kwa kusomea ambapo ana masta yake ambayo alichukua baada ya kupata elimu ya juu ua utabibu wa binadamu.
No comments:
Post a Comment