LONDON, England
TIMU za Manchester
United na Arsenal leo zinakutana katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA.
Tayari kocha wa Arsenal,
Arsene Wenger amekiri kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na uzoefu wa timu
hizo katika mashindano hayo. Timu hizo ndizo zilizotwaa taji hilo mara nyingi.
Wenger alisema
anaamini timu itakayoibuka na ushindi leo ndio itakuwa bingwa wa kombe hilo.
Mchezo huo utapigwa
kuanzia saa 4:45 usiku kwa majira ya Afrika Mashariki.
“Ninauona
huu ni mchezo mgumu na utakaotoa sura halisi ya ubigwa hasa ikizingatiwa kuwa
atakayeibuka mshindi ndiye anayeweza kutwaa taji hili mwishoni, “alisema
kocha huyo.
Aidha, nahodha wa
Manchester United, Wayne Rooney atacheza mchezo huo huku akiwa na kumbukumbu ya
mataji tisa, lakini katika vikombe hivyo, halipo la FA.
Rooney akiwa na
timu hiyo mwaka 2005 wakati timu yake hiyo ilipocheza na Arsenal pamoja na
mwaka 2007 ilipocheza na
Chelsea, haikuweza
kushinda kombe hilo.
“Kwa miaka mingi
hatujafikia hatua ya kucheza fainali kwa mchezo huu tunaweza kuondoa gundu na
kufikia fainali kirahisi na kulitwaa taji hilo, ”alisema alisema
Rooney.
Katika mechi nyingine ya michuano hiyo iliyochezwa usiku wa kuamkia leo, Liverpool ilibanwa nyumbani na Blackburn na sasa watarudiana kupata mshindi wa kuungana na timu ya Aston Villa iliyotangulia kwa kuilaza West Bromwich Albion.
No comments:
Post a Comment