Hazard akipiga penati iliyookolewa wakati Chelsea wakitoka sare ya 1-1 |
Man City wakiadhibiwa na Doumbia |
Yaya Toure akishangilia bao lake jana |
Kisha akaja akalimwa kadi nyekundu ya kwamba maisha yake Etihad |
Wachezaji wa Bayern Munich wakishangilia mabao yao yaliyowapeleka kwenye 16 Bora ya Ulaya |
Fracky Ribery akishangilia bao la kwanza la Bavarians |
Cheslea katika mechi ya Kungi G ilishtukizwa kwa bao lililofungwa dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza baada ya Agim Ibraimi kuifungia Maribor, kabla ya Nemanja Matic kusawazisha katika dakika ya 73.
Wakiwa na nafasi ya kuendeleza rekodi ya kipigo cha Maribor, Chelsea walipoteza penati baada ya mshambuliaji Eden Hazard kushindwa kukwamisha mpira wavuni.
Hata hivyo matokoe hayo bado yameiacha Chelsea kileleni mwa msimamo wa kundi hilo wakiwa na pointi nane wakifuatiwa na Schalke 04 iliyolala ugenini kwa mabao 4-2 mbele ya Sporting yenye pointi tano.
Katika mechi nyingine za michuano hiyo, Manchester City walijikuta wakijiweka pabaya kwa kukubali kipigo cha mabao 2-1 nyumbani dhidi ya CSKA Moscow, huku ikiwapoteza nyota wake wawili, akiwamo Yaya Toure aliyefunga bao pekee la timu hiyo.
Yaya alilimwa kadi ya pili ya njano na kusindikizwa na nyekundu na kuwa kadi yake ya kwanza tangu aanze kuichezea timu hiyo na tayari amewaomba radhi mashabiki wa klabu hioyo ya Etihad.
CSKA Moscow waliwashtukiza wenyeji kwa bao la mapema la dakika ya pili kupitia Seydou Doumbia akimalizia kati ya Natcho kabla ya Yaya Toure kusawazisha dakika sita baadaye ma Doumbia akamaliza udhia dakika ya 34 kwa kufunga bao la pili na katika kipindi cha pili wenyeji kuwapoteza Yaya na Fernandinho.
Kipigo hicho kimeiacha City wakiwa wanaburuza mkia wakiwa na pointi mbili wakitakiwa kupata ushindi mfululizo dhidi ya Bayern Munich waliofuzu baada ya kuilaza Roma kwa mabao 2-0 na ile dhidi ya Roma wenyewe ambao wanashika nafasi ya pili wakilingana pointi na CSKA.
Katika mechi nyingine Porto ya Ureno ikiwa ugenini nchini Hispania ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Athletico Bilbao, huku Shakhtar Donetsk ya Uturuki wakiichakaza BATE kwa mabao 5-0 katika mechi za kundi H.
No comments:
Post a Comment