Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
MTU
mmoja aitwaye Hamis Mohamed (47) Mkazi wa Kondoa mkoa wa Dodoma,
amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha baada ya kukutwa na madawa
ya kulevya aina ya mirungi aliyekuwa anaisafirisha kwa mtindo wa aina
yake.
Akiongea
na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas alisema
kwamba tukio hilo lilitokea tarehe 05.11.2014 muda wa saa 11:00 jioni
eneo la Mianzini ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa anasafirisha madawa hayo
kwenye gari aina ya Fusso basi lenye namba za usajili T. 577 BFM ambapo
aliihifadhi kwenye magunia mawili huku juu na pembeni ya magunia hayo
akiweka viatu.
‘’Katika
magunia yale alikuwa ameweka viatu na katikati aliweka viroba 36 vya
madawa hayo aina ya mirungi ambayo alikuwa anasafirisha toka nchini
Kenya kupeleka Kondoa mkoani Dodoma hivyo ukiangalia unaweza kusema ni
viatu pekee’’. Alifafanua Kamanda Sabas.
Alisema
tukio hilo lilifanikiwa kutokana na mahusiano mema yaliyopo kati ya
Jeshi hilo na raia wema ambao walitoa taarifa iliyofanyiwa kazi haraka
na asakari wa Jeshi hilo.
Baada
ya askari hao kupata taarifa hiyo walianza kulifuatilia gari hilo na
lilipofika maeneo ya Mianzini jijini hapa kwenye maegesho ya basi hilo
ndipo walipoanza kufanya upekuzi na kufanikiwa kukamata magunia hayo
yaliyokuwa na viatu vilivyochanganywa na madawa hayo.
Kamanda
Sabas alisema kwamba mtuhumiwa huyo bado anaendelea kuhojiwa na
atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
No comments:
Post a Comment