Manji (kati)n akitetea na Cannavaro na Chuji misimu kadhaa ya nyuma ya Ligi Kuu Bara |
Kamati ya Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilitangaza leo Ijumaa ndio siku ya kufunguliwa kwa zoezi hilo, lakini mpaka jioni hii hakuna aliyejitokeza, huku kukiwa na taarifa kwamba Yanga wameugomea uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Alloyce Komba amedokeza kuwa, hakuna aliyejitokeza kuchukua fomu, lakini akiamini muda bado kwani wana siku 5 za zoezi hilo kufikia tamati.
Hata hivyo MICHARAZO imenasa taarifa kuwa, uchaguzi huo umesuswa na wana Yanga baada ya kutaka usifanyike kipindi hiki ambacho klabu yao itakuwa kwenye pilikapilika za kuelekea kwenye mechi zao za kimataifa ya Kombe la Shirikisho.
Yanga imepangwa Kundi A na timu za MO Bejaia ya Algeria, TP Mazembe ya DR Congo na Medeama ya Ghana na itaanza mechi zao siku mbili kabla ya kuvaana na Bejaia mjini Algiers, Algeria.
Uchaguzi wa Yanga umepangwa kufanyika Juni 15, lakini uongozi wa klabu hiyo ukitaka ufanyike tarehe moja na uchaguzi wao mdogo uliofanyika Julai 15, 2012 na kumuingiza Mwenyekiti na tajiri wao, Yusuf Manji.
No comments:
Post a Comment