Kikosi cha Yanga kilichoibana Al Ahly kwa kuilaza 1-0 jijini Dar jumamosi iliyiopita |
IMETHIBITIKA kuwa, wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika timu
ya Young Africans itacheza mchezo wa marudiano siku ya jumapili jijini
Cairo dhidi ya timu ya Al Ahly ukiwa ni mchezo utakaotoa picha halisi ni
timu gani itasonga mbele katika hatua ya 16 bora.
Ikiwa ni takribani siku tano kabla
ya kufanyika mchezo wenyewe wenyeji Al Ahly wameshindwa kuweka wazi ni
uwanja gani utakaotumika kwa ajili ya mchezo huo huku Meneja wa klabu
hiyo Abdoulazi akisema huenda mchezo ukachezwa jijini Cairo au
Alexandria na kusema majibu kabili yatapatikana siku ya jumatano mchana.
Wenyeji
wameiandalia timu ya Young Africans kufikia katika Hoteli ya Baron
iliyopo maneneo ya Uwanja wa michezo wa kimataifa Cairo huku pia
wakiipangia timu kufanya mazoezi katika uwanja wao uliopo eneno la Nasri
City.
Katika mchezo wa
awali uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye dimba la Uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam Young Africans ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa
bao 1-0 dhidi ya Al Ahly ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo
shukrani kwa bao la Nahodha wa timu Nadir Haroub "Cannavaro"
aliyetikisha nyavu dakika ya 82 ya mchezo.
Mara baada ya
mchezo huo kikosi cha mholanzi Hans Van der Pluijm kiliingia kambini
jana jioni katika hotel ya Ledger Bahari Beach tayari kwa maandalizi ya
mchezo marudiano ambapo timu imeendelea kufanya mazoezi katika uwanja wa
Boko Beach Veterani.
Kuelekea mchezo huo wa jumamosi tayari
uongozi wa Young Africans ulishaanza kufanya maandalizi ya safari ambayo
inatarajiwa kuwepo kabla ya mwisho mwa wiki hii huku msafara
ukitarajiwa na kuwa idadi ya watu 35, wakimwemo viongozi, benchi la
ufundi pamoja na wachezaji 19.
Hali ya wachezaji ni nzuri, kiafya,
fikra na morali ya kuelekea mchezo wenyewe bado ni kubwa kwani bench la
ufundi na wachezaji wanaamini maandalizi wanayoyafanya yatasaidia
kupelekea kupata ushindi katika mchezo huo na kuweza kusonga mbele
katika hatua ya 16 bora.
Baadhi ya wachezaji wanaotarajiwa kuondoka usiku wa leo kuifuata Al Ahly ni makipa Deogratius Munishi 'Dida' na Juma Kaseja, Nadir Haroub 'Cannavaro, David Luhende, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Simon Msuva, Mrisho Ngasa, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbagu, Juma Abdul, Frank Domayo, Mbuyu Twite, Rajab Zahir na Said Bahanuzi.
Okwi na Kiiza, wataungana na kikosi hicho Alhamisi wakitokea Lusaka, walipo na timu yao ya Taifa ya Uganda ( The Cranes) ambayo jana ilikuwa inacheza na Zambia (Chipolopolo) mechi ya kimataifa ya kirafiki.
Yanga inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili iweze kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
Maandalizi ya sehemu ya kambi ambapo timu itafikia jijini Cairo tayari yanaendelea vizuri kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania ambapo kwa upande wa klabu ya Young Africans Afisa Habari Baraka Kizuguto tayari yupo nchini Misri kwa siku ya pili akiendelea kuweka mambo sawa.
Okwi na Kiiza, wataungana na kikosi hicho Alhamisi wakitokea Lusaka, walipo na timu yao ya Taifa ya Uganda ( The Cranes) ambayo jana ilikuwa inacheza na Zambia (Chipolopolo) mechi ya kimataifa ya kirafiki.
Yanga inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili iweze kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
Maandalizi ya sehemu ya kambi ambapo timu itafikia jijini Cairo tayari yanaendelea vizuri kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania ambapo kwa upande wa klabu ya Young Africans Afisa Habari Baraka Kizuguto tayari yupo nchini Misri kwa siku ya pili akiendelea kuweka mambo sawa.
Mchezo wa jumapili unatarajiwa
kufanyika katika uwanja wa Arab Contractors uliopo jijini Cairo huku
mechi hiyo ikichezwa bila ya mashabiki kufuatia Serikali ya Misri kuzuia
mashabiki wa soka kutokana na mashabiki hao kufanya vurugu katika
mchezo wa Fainal ya Super Cup dhidi ya CS Sfaxien na kupelekea askari
kadhaa kujeruhiwa.
No comments:
Post a Comment