Kanga (kushoto) aliyefungiwa Russia kwa kutoa ishara za matusi baada ya kubaguliwa na mashabiki wa Spartak Moscow |
Kanga alionyesha ishara hiyo baada ya kuonyesha ishara ya matusi kwa mashabiki wa Spartak Moscow ambao walimfanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi.
Kiungo huyo wa klabu ya FC Rostov mwenye umri wa miaka 24 alikuwa akipigiwa kelele za nyani na mashabiki wa Spartak wakati wa mchezo wa Ligi Kuu nchini humo uliofanyika jijini Moscow.
Katika kujibu mapigo ya kejeli hizo nyota huyo alitoa ishara hizo hatua ambayo RFU ilibidi kuchukua hatua kwa kumtoza pia na faini ya paundi 600.
Spartak nao walitozwa faini ya paundi 830 kutokana na mashabiki wao kuonyesha vitendo vya kibaguzi.
Septemba mwaka huu beki wa Dynamo Moscow Christopher Samba alifungiwa mechi mbili kwa kufanya tukio kama hilo wakati mashabiki wa timu ya Torpedo Moscow walivyomfanyia vitendo vya kibaguzi.
KIUNGO wa kimataifa wa
Gabon, Guelor Kanga amefungiwa mechi tatu na Shirikisho la Soka la
Urusi-RFU kwa kuonyesha ishara ya matusi kwa mashabiki wa Spartak Moscow
ambao walimfanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi. Kiungo huyo wa klabu ya
FC Rostov mwenye umri wa miaka 24 alikuwa akipigiwa kelele za nyani na
mashabiki wa Spartak wakati wa mchezo wa Ligi Kuu nchini humo
uliofanyika jijini Moscow jana. Nyota huyo naye alijibu mapigo hatua
ambayo RFU ilibidi kuchukua hatua kwa kumtoza pia na faini ya paundi
600. Spartak nao walitozwa faini ya paundi 830 kutokana na mashabiki wao
kuonyesha vitendo vya kibaguzi. Septemba mwaka huu beki wa Dynamo
Moscow Christopher Samba alifungiwa mechi mbili kwa kufanya tukio kama
hilo wakati mashabiki wa timu ya Torpedo Moscow walivyomfanyia vitendo
vya kibaguzi.
Make Money
Make Money
No comments:
Post a Comment