Emmanuel Okwi akiwa na mpira wake baada ya kupiga hat trick dhidi ya Ruvu Shooting |
Ibrahim Ajibu katika mazoezi ya Yanga |
Donald Ngoma |
Mtibwa Sugar |
STRAIKA wa Simba, Emmanuel Okwi anayeichezea Simba amewazidi ujanja mastraika wa Yanga, Donald Ngoma na Ibrahim Ajibu, baada ya kusalia kileleni mwa orodha ya wafungaji akiwa na mabao manne, licha ya nyota hao wa Jangwani kushuka dimbani kwa dakika nyingi zaidi ya Mganda huyo.
Okwi ametumia dakika 90 tu kufunga mabao yake akicheza mchezo mmoja tu na kuukosa mchezao mmoja, lakini Ngoma na Ajibu kila mmoja amecheza mechi mbili na kufunga bao moja kila mmojam, jambo lililowapa kiburi mashabiki wa Msimbazi kuwatambia wenzao wa Jangwani.
Mganda huyo aliyewahi kuichezea Yanga misimu mitatu iliyopita, aliukosa mchezo wa timu yake dhidi ya Azam Jumamosi iliyopita ulioisha kwa suluhu, lakini hilo halikumfanya ashindwe kukalia kiti cha uongozi wa wafungaji.
Okwi ambaye jana asubuhi alishindwa kuhudhuria mazoezi ya timu yake yaliyofanyika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam ili kujiandaa na mchezo wao ujao dhidi ya Mwadui Jumapili hii, alishindwa kuwahi mechi ya Azam kutokana na kuwa na timu yake ya taifa ya Uganda The Cranes iliyoenda kuvaana na Misri katika mechi ya makundi ya kuwania Fainali za Kombe la Dunia 2018.
Ngoma aliyeifungia Yanga bao la kusawazisha katika mchezo wa kwanza dhidi ya Lipuli na kutolewa katika kipindi cha pili kwenye mchezo dhidi ya Njombe Mji, bado hajarudi kwenye ubora wake tangu atoke kwenye majeraha ya muda mrefu yaliyomfanya ashindwe kuitumikia timu hiyo kwenye mechi za nusu wa msimu uliopita aliomaliza na mabao nane.
Ajibu aliyecheza dakika 180 za mechi mbili za Yanga za msimu huu, naye alifunga bao moja lililokuwa la pekee katika mchezo wao na Njombe Mji na kuzidi kuwapa kiburi Simba kuamini kuwa, licha ya Yanga kuwa na safu kali ya washambuliaji lakini jeshi la mtu mmoja, yaani Okwi ni funika bovu.
Okwi alifunga mabao manne katika mechi ya ufunguzi wa ligi dhidi yas Ruvu Shooting ambapo Simba walishinda mabao 7-0 na timu yake kushindwa kupata matokeo kwenye Uwanja wa Azam Complex dhidi ya Azam.
Mpaka sasa wachezaji 27 wamefanikiwa kufunga jumla ya mabao 32, huku Mohammed Rashid wa Prisons na Marcel Bonventure wa Majimaji wenye mabao mawili kila mmoja wakionekana kumkimbiza Okwi.
Mpaka sasa Ligi ikiwa imeshacheza mechi 16, Ruvu Shooting ndio klabu yenye ukuta mlaini baada ya kuruhusu mabao tisa na yenyewe kufunga bao moja tu, huku Chama la Wana Stand United ikiwa ndiyo timu pekee ambayo haijafanikiwa kufunga bao hata moja, licha ya yenyewe kuruhusu mabao mawili nyavuni mwao.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo nane, Ijumaa Azam itaikaribisha Kagera Sugar kabla ya Simba na Yanga kucheza katika miji ya Dar es Salaam na Ruvuma dhidi ya Mwadui na Majimaji, wakati vinara wa ligi hiyo, Mtibwa Sugar wenyewe wataendelea kuwa nyumbani kuwakaribisha Mbao FC iliyotoka kujeruhiwa mjini Dodoma na Singida United Jumapili iliyopita.
Msimamo Ligi Kuu Tanzania Bara 2017-2018 ulivyo kwa sasa
P W D L F A PTS
1.Mtibwa 2 2 0 0 2 0 6
2.Simba 2 1 1 0 7 0 4
3.Prisons 2 1 1 0 4 3 4
4.Lipuli 2 1 1 0 2 1 4
5.Yanga 2 1 1 0 2 1 4
6.Azam 2 1 1 0 1 0 4
7.Singida 2 1 0 1 3 3 3
8.Mwadui 2 1 0 1 2 2 3
9.Mbao 2 1 0 1 2 2 3
10.Mbeya 2 1 0 1 1 1 3
11.Ndanda2 1 0 1 1 1 3
12.Majimaji2 0 1 1 2 3 1
13.Kagera2 0 1 1 1 2 1
14.Ruvu 2 0 1 1 1 8 1
15.Njombe2 0 0 2 1 3 0
16.Stand 2 0 0 2 0 2 0
WAFUNGAJI:
4 Emmanuel Okwi (Simba)
2 Marcel Boniventure (Majimaji)
Mohammed Rashid (Prisons)
1 Ibrahim Ajibu (Yanga)
Erasto Nyoni (Simba)
Juma Liuzio (Simba)
Shiza Kichuya (Simba)
Donald Ngoma (Yanga)
Paul Nonga (Mwadui)
Yahaya Mohammed (Azam)
Salim Khamis (Mwadui)
Kenny Ally (Singida United)
Boniface Maganga (Mbao FC)
Hussein Javu (Mtibwa Sugar)
Eliud Ambukile (Mbeya City)
Kassim Khamis (Prisons)
Nurdin Chona (Prisons)
Hassan Kapalata (Njombe Mji)
Seif Karihe (Lipuli)
Jerome Lambele (Lipuli)
Mudathir Yahya (Singida)
Michelle Katsvairo (Singida)
Seleman Kihimbwa (Mtibwa)
Habib Kayombo (Mbao)
Majid Bakar (Ndanda)
Raphael Kyara (Ruvu Shooting)
RATIBA WIKIENDI HII:
Ijumaa Sept 15, 2017
Azam v Kagera Sugar
Jumamosi Sept 16, 2017
Mtibwa Sugar v Mbao FC
Majimaji v Yanga
Prisons v Ndanda
Stand United v Singida United
Lipuli v Ruvu Shooting
Jumapili Sept 17, 2017
Simba v Mwadui
Mbeya City v Njombe Mji
No comments:
Post a Comment