WAKALA wa Barabara Tanzania (TANROADS), umesema kuanzia Machi 17 mwaka
huu mzani wa kupimia magari Kibaha hautaendelea kutoa huduma kwa magari
na huduma hiyo itahamia katika mzani mpya wa Vigwazwa.
Hayo
yalisemwa na Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale wakati
akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
Alisema
mzani wa Kibaha ulikuwa unatumia dakika moja na nusu kupima gari moja
hali ambayo ilikuwa inasababisha msongamono ila mzani wa Vigwaza utakuwa
unatumia sekunde 30 kwa gari moja.
Mhandisi Mfugale alisema
kituo hicho cha Vigwazwa ni cha kisasa kina Mtambo wa Kuchambua magari
(Weight-in- Motion) kwa kupima magari yakitembea.
Pia Mfugale
alisema hicho kina Mzani Mkubwa (Multi-deck) unaweza kupima gari lolote
kwa mkupuo hali ambayo itasaidia kupunguza msongamano.
"Mzani wa
Vigwaza umekamilika na juzi ulianza kazi kwa majaribio ila tunatarajia
kusitisha huduma ya upimaji uzito eneo la Kibaha kesho, hivyo ni vyema
madereva wakajiandaa kwa hilo," alisema.
Alisema barabara ya za
kuingia katika mzani huo ambazo zina kilometa 1.8 zimekamilika ambazo
zina upana wa milikita 200 na kudumu kwa miaka zaidi ya 50.
Mtendaji
Mkuu huyo alisema mzani huo utakuwa unaelekeza magari ambayo
yamezidisha mzigo wapi yakapaki na yale ambayo hayana tatizo yaendelee
kwa safari.
Alisema magari yanayotakiwa kupima uzito ni kuanzia
yale yenye uzito kuanzia tani 3.5 ambapo aliwataka madereva kufuata
taratibu na sheria za barabara kwa kuacha nafasi ya mita 30 kati ya gari
na gari.
Mhandisi Mfugale alitoa rai kwa wamiliki wa magari
kuhakikisha kuwa wanatengeneza magari yao ili kuepusha kuharibika katika
eneo hilo kwani watapigwa faini.
Mfugale alisema mzani huo
umegharimu bilioni 11 ambapo jitihada zao ni kuendelea na ujenzi katika
mzani nyingine ili ziweze kuwa na ubora kama wa Vigwaza.
No comments:
Post a Comment