MCHEZO WA NGUMI ULIPOHAMASISHWA CHALINZE, PWANI
Bondia Amos Thomas kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Edrew Joseph wakati wa mpambano wa kuamasisha mchezo wa masumbwi Chalinze Mkoa wa pwani Juzi mchezo huo ulitoka droo picha na www.superdboximgcoach.blogspot.com |
Baazi ya mashabiki wakiwa na Diwani wao |
Bondia Said Minyusi wa Chalinze kushoto akirusha konde ambalo alina madhala kwa Zumbe Kukwe wa Dar wakati wa mpambano wa kuamasisha masumbwi Chalinze mkoa wa Pwani juzi Kukwe alishinda kwa TKO ya raundi ya kwanza picha na www.superdboximgcoach.blogspot.com |
Baazi ya mashabiki waliojitokeza kuhamasisha mchezo wa masumbwi wakiangalia burudani hiyo |
Mabondia walio itimisha mpambano huo wakati wa kuhamasisha masumbwi Chalinze |
Diwani wa Kata ya Bwilingi Chalinze Ahmed Kalama Nassar akizungumza kabla ya mpambano wa mwisho kwa ajili ya kuhamasisha ngumi katika kata hiyo |
Mwaite Juma wa Chalinze kushoto akimwangalia bondia Mussa Ali baada ya kupiga konde zito na kwenda chini |
Na Mwandishi Wetu
ZAIDI ya mashabiki 300 wamejitokeza
kuangalia mpambano wa Masumbwi kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa ngumi
Chalinze Mkoa wa Pwani pamoja na vitongoji vyake mashindano hayo ya
masumbwi yaliyoandaliwa maalumu kuhamasisha mchezo uho katika vitongoji
maarufu.
Uliwakutanisha mabondia wa Dar es
salaam na Chalinze na mabondia wanaotamba katika kitongoji hicho
mpambano huo wa masumbwi ulioanza saa tatu ya usiku na kumalizika saa
nne na nusu uliwakutanisha bondia Amos Thomas aliye toka sare na Edrew
Joseph uku mpambano mwingine ukiwakutanisha Zumbe Kukwe wa Dar es salaam
aliye mgalagaza bila huruma Said Minyusi wa chalinze
Mpambano mwingine ni Alex Kado wa chalinze alishindwa kuhimili mikiki mikiki ya Nassoro Khatibu na kupigwa kwa ponti
Pambano lililokuwa likisubiliwa na
watu wengi zaidi ni mpambano uliowakutanisha Mwaite Juma wa Chalinze na
Mussa Ali ambapo mwaite aliweza kumsambalatisha ali kwa TKO ya raundi ya
kwanza na kupeleka shwangwe kwa wapenzi waliojitokeza katika mpambano
huo
Baada ya kumalizika kwa mpambano huo
Diwani wa Kata ya Bwilingi Chalinze Ahmed Kalama Nassar ambaye alikuwa
mgeni rasmi wa mpambano huo alisema yupo tayali kuwanunulia vifaa vya
mchezo huo ili kuendeleza masumbwi katika kata hiyo
Ambapo ame haidi kuongeza ushirikiano
wa wataalamu wa masumbwi kwa kushilikiana na viongozi ili chalinzi kiwe
kitovu cha masumbwi nchini
No comments:
Post a Comment