STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, April 22, 2013

Mashindao ya Riadha U20 kufanyika Zenji

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4MRYWGaiLwnTGgJtc49qDsVjytrioJmvE95B2Ndd9okhk30ZTiIrdlFtXuVPYbyPaAJvb67dr-elIWgHn5MlMAJdkDSqh2K30GlGAGBlWMhdAxh-kZgVQtM8pIvegFVxip0vb6SncB78/s1600/nyambui.JPG
Katibu Mkuu wa RT,Suleiman Nyambui (Kulia)

NCHI 10 zinatarajia kushiriki mashindano ya riadha kwa vijana chini ya miaka 20 kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, yatakayofanyika Visiwani Zanzibar kuanzia Juni 8 hadi 9, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui, wameamua kuyapeleka mashindano hayo Zanzibar kutokana na uwanja huo kutokutumika kwa muda mrefu tangu ulipofanyiwa ukarabati.

“Tumeamua mashindano haya yafanyike visiwani humo kutokana na uwanja huo kutokutumika kwa muda toka ufanyiwe marekebisho, na kujua kama una uwezo wa kuhimili mikikimikiki ya mashindano makubwa kama haya ya kimataifa,” alisema Nyambui.

Alizitaja nchi zinazotarajia kushiriki mashindano hayo kuwa ni Misri, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Somaria, Uganda, Sudan, Sudan Kusini ambayo itashiriki kama mgeni mwalikwa, Kenya, Tanzania na wenyeji Zanzibar.

Nyambui alisema amependekeza katika Kamati ya Utendaji, wachezaji kumi watakaofikia viwango vya kushiriki mashindano ya Afrika, sita wa kiume na wanne wa kike kuchaguliwa kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo baadaye mwaka huu.

No comments:

Post a Comment