Full Squad ya Manchester United msimu huu |
MASHABIKI wa soka wa vinara wa Ligi Kuu ya England, Manchester United wanasubiri masaa tu kuweza kushsrehekea ubingwa wao wa 20 wa ligi hiyo iwapo timu yao itaicharaza Aston Villa wanaokutana naoi usiku wa leo.
Pambano hilo litakalochezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Mashetani Wekundu wa Old Trafford, ndiyo utakaoamua kama Manchester United kama ndiyo mabingwa wa msimu huu au kusubiri mpaka mwishoni mwa wiki kuweza kufanya hivyo baada ya wapinzani wao Manchester City jana kupoteza mwelekeo.
Manachester City ambao ndiyo mabingwa watetezi wa ligi hiyo, jana walikumbana na kipigo cha aibu baada ya kunyukwa ugenini mabao 3-1 licha ya kuongoza kwa muda mrefu kwa bao 1-0 na kujikuta wakishindwa kupunguza pengo la pointi na mahasimu wao hao ambao wamekaa kileleni kwa muda mrefu.
Iwapo Manchester United itaishinda ASston Villa katika pambano hilo litakalochezwa majira ya saa 4 usiku kwa saa Afrika Mashariki itamaanisha kwamba itafikisha pointi 84 ambazo haziwezi kufikiwa na klabu yoyote wakiwemo watetezi hao waliosalia na pointi 68 na kusaliwa na mechi tano zinazoweza kuwafikishia pointi 53 tu iwapo watashinda mechi zao zilizosalia.
Pia ushindi huo utamaanisha kwamba Mashetani Wekundu hao watavunja rekodi ya kuwa klabu iliyotwaa mataji mengi ya ligi hiyo wakivunja rekodi ya Liverpool ya mataji 19 iliyokuwa ikiishikilia.
Vinara hao wataikaribisha Aston Villa wakitoka kwenye pambano lililoisha kwa sare ya mabao 2-2 dhidio ya West Ham United, wakiwa na tahadhari kuwa dhidi ya timu inayopigana kuepuka kushuka daraja kwani uzembe wowote utawacheleweshewa mbio zao za ubingwa huo.
United itakosa huduma za nyuota wa zamani wa Aston Villa, Ashley Young, lakini ikiwa na matumaini kwa kinara wake wa mabao, Robin van Persie atakuwa akipigana kumfukuzia Luis Suarez aliyemzidi kwa mabao mawili mpaka sasa katikamorodha ya wafungaji atakayeshirikiana na Wayne Rooney kuhakikisha wanaitia adabu Villa itakayomtegemea Christian Benteke na Gabriel Agbonlahor kuinusuru timu yao na kipigo.
Je washabiki wa Machester United watasherehekea ubingwa au watasubiri hadi mwishoni mwa wiki? Ni suala la kusubiri kuona, japo asilimia kubwa ya Mashetani Wekundu wanaamini leo ni RAHA TUPU kwao.
No comments:
Post a Comment