Marehemu Mabina enzi za uhai wake |
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Eng. Evarist Ndikilo kufuatia vifo vya
watu wawili vilivyotokea tarehe 15 Desemba,2013 katika Kitongoji cha Kanyama
Kata ya Kisesa Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza.
Rais
ametuma salamu hizo kwa Mkuu wa Mkoa kufuatia vifo vya BW. Clement Mabina na
Tenery Malimi vilivyotokea baada vurugu zilizosababishwa na mabishano ya ardhi.
Rais
amemuomba Mkuu wa Mkoa kuwatahadharisha wananchi kutokuchukua sheria mikononi
mwao na pia kuwa waangalifu na matumizi ya silaha za moto.
“Nimesikitishwa
na kufadhaishwa sana na taarifa za vifo vya wananchi hao wawili (2)
vilivyosababishwa na mgogoro wa Ardhi ambao ungeweza kupata suluhu kwa njia za
amani. Ni vema wananchi kuwa na subira na kuwa waangalifu katika kutatua
migogoro yao”. Rais amesema na kuongeza kuwa “ ni
vema subira na busara zikawa ndio muongozo wa kutatua migogoro yetu katika
jamii badala ya hasira”.
Aidha,
Rais Kikwete amemuomba Mkuu wa Mkoa amfikishie salamu zake za dhati kwa familia
na ndugu wa Marehemu Mabina pamoja na Wazazi na ndugu wa Marehemu Tenery Malimi,
ambao walifariki kutokana na vurugu hizo.
“Amewaomba
familia zote mbili ziwe na subira wakati huu mgumu kwa kuondokewa na wapendwa
wao na kuviacha vyombo vya dola kuchukua hatua kwa kufuata taratibu zilizopo”. Kwa ndugu Mabina, Chama cha Mapinduzi
kimepoteza mmoja wa viongozi wake mahiri na wa kutumainiwa. Aidha, kwa marehemu Tenery taifa limepoteza
mmoja wa vijana wake wanaochipukia ambae angejaaliwa kuishi angeweza kutoa
mchango muhimu kwa maendeleo ya jamii na nchi yetu.
Mabina amewahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo
Diwani na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Magu mwaka 2000 – 2005, Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza, mwaka 2007 – 2012.
Rais
ameziombea nyoyo za marehemu wote Mungu azilaze
mahali pema peponi Amen.
Imetolewa
na;
Premi
Kibanga,
Mwandishi
wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
17
Desemba,2013
No comments:
Post a Comment