STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, September 21, 2012

Kocha Yanga akiri kuzidiwa ujanja na Mtibwa alaumu wachezaji wake

Kocha Tom Saintfiet akiwa haamini kama jahazi la timu yake limezana uwanja wa Jamhuri, walipokandikwa mabao 3-0 na Mtibwa Sugar

KOCHA wa klabu ya Yanga, Tom Saintfiet, amekiri timu yake ilizidiwa maarifa na Mtibwa Sugar na kulazwa mabao 3-0, akidai hakuna cha kusingizia kwa kipigo hicho.
Akihojiwa na kituo kimoja cha redio, Mbelgiji huyo alisema tofauti na utetezi wake katika mechi iliyopita waliotoka sare ya 0-0 na Prisons Mbeya, kipigo cha Mtibwa kilikuwa halali kwa sababu kila kitu kwao kilikuwa vema.
Saintfiet, alisema hawezi kusema uwanja wa Jamhuri ulikuwa mbaya, ama chakula au hoteli waliyolala kama ilivyokuwa mjini Mbeya, zaidi ya kuwashutumu wachezaji wake kwamba hawakuwa makini uwanjani kutumia nafasi walizopata.
"Mtibwa walipata nafasi nne na kuzitumia vema tatu kwa kufunga mabao matatu, wakati sisi tulipata karibu nafasi nane na hata moja hatukutumia," alisema.
Aliongeza amegundua kinachowaathiri wachezaji wake ni kulewa sifa za magazetini na hivyo kuishia kushindana kubadilisha mitindo ya nywele na viatu badala ya kushindana uwanjani kuisaidia timu.
"Wamelewa sifa, walisifiwa kwenye michuano ya Kagame na wamejisahau wao kila siku wamekuwa wakishindana kubadilisha mitindo ya nywele na viatu, watambue wakati mwingine wanapaswa kufanya nini uwanjani," alisema.
Alidai lau kama yeye (Saintfiet) na msaidizi wake, Fred Felix Minziro wangeingia uwanjani wangeweza kufunga mabao kwa nafasi walizokuwa wamezitengeza.
Yanga ilikumbana na kipigo hicho cha 3-0 toka kwa Mtibwa katika mechi ambayo Hamis Kiiza alikosa penati dakika lala salama, na kuicha ikisaliwa na pointi moja tu.
Timu hiyo kesho inatarajiwa kushuka dimbani kuumana na JKT Ruvu katika mechi nyingine ngumu, ingawa Saintfeit amedai amezungumza na wachezaji na kuahidi kurekebisha makosa kwa kuipa timu ushindi hili mambo yasiendelee kuwa mabaya.

No comments:

Post a Comment