STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, May 6, 2013

Shaaban Dihile akiri Ligi Kuu msimu huu kiboko

Kipa Shaaban Dihile akiwa mazoezini na Taifa Stars
KIPA namba moja wa zamani wa Tanzania, Shaaban Dihile anayeidakia JKT Ruvu, amekiri Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2012-2013 ulikuwa mgumu kupita kiasi na kushukuru kutoshukwa kwao daraja.
Dihile, alisema kwa hali waliyokuwa nayo msimu huu na ugumu wa ligi ulivyokuwa, anaona ni kama miujiza kwa kikosi chao kusalia kwenye ligi hiyo kwa msimu ujao.
Akizungumza na MICHARAZO, Dihile aliyewahi kutamba na timu za Micco Villa, Everet ya Temeke, Dar Newala na Pan Afrika kabla ya kutua JKT mwaka 2005 alisema maandalizi yaliyofanywa na klabu zilizoshiriki ligi ya msimu huu ndiko kulikofanya ligi iwe ngumu na isiyotabirika kirahisi.
"Msimu huu ligi imekuwa ngumu na timu kutotabirika kwa klabu zilizofanya uzembe kwenye maandalizi yake zimejikuta kwenye wakati mgumu, ndiyo maana mpaka sasa siamini kama tumepoina kushuka daraja kutokana na hali tuliyokuwa nayo tangu tunaanza duru la kwanza mwaka jana," alisema Dihile.
Kipa huyo machachari ambaye msimu huu amekuwa akisumbuliwa na majeraha, alisema anaamini JKT watajipanga upya kwa msimu ujao ili warejee kwenye ligi ijayo wakiwa wapya na kuendeleza cheche zao.
Kuhusu kushindwa kufurukuta kwa wazawa msimu huu na kufunikwa na wageni, Dihile alisema ni kitu kinachotokea katika soka, japo alikiri kuyumba kwa wachezaji wa Kibongo kunachangia kufanya Stars nayo iyumbe kwa kukosa wachezaji wa kuaminika kikosi licha ya kuimwagia sifa kocha Kim Poulsen.
"Kung'ara kwa 'mapro' ni msiba wa kikosi cha Stars, kwani wachezaji wengine wanaotegemewa kwenye timu hiyo ni wale wanaotamba kwenye ligi, hata hivyo jambo la kuvutia ni kwamba Tanzania tumebahatika kuwa na kocha mzuri na mwenye kutambua kazi yake," alisema Dihile.
Katika orodha ya wafungaji mabao ya ligi hiyo inayomalizika Mei 18, kinara ni Kipre Tchetche, akifuatiwa kwa mbali na wachezaji kama akina Mcha Khamis Vialli, Paul Nonga, Hussein Javu, ambao wanabanana na akina Didier Kavumbagu, Haruna Niyonzima na Hamis Kiiza.

No comments:

Post a Comment