Yanga |
Azam watakaoanza na El Merreikh ya Sudan |
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), imetangaza ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo Azam wamepangwa kuanza na El Merreikh ya Sudan, wakati Yanga wakitupiwa maafande wa Jeshi kutoka Botswana.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Azam ambao watashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza mwakani itaanzia nyumbani kabla ya kuwafuata Wasudan hao kwao katika mechi ya marudiano.
Wenyewe Yanga ambao mwaka huu ilishiriki Ligi ya Mabingwa na kung'olewa raundi ya pili na waliokuwa mabingwa watetezi, Al Ahly, imepangwa kuanzia pia nyumbani katika Kombe la Shirikisho dhidi ya BDF IX ya Botswana inayomilikiwa na Jeshi la nchi hiyo.
Wawakilishi wengine wa Zanzibar, mabingwa KMKM wataanzia ugenini kwa kuumana na Al Hilal ya Sudan katika Ligi ya Mabingwa Afrika na wawakilishi wa Kombe la Shirikisho, Polisi wataanza ugenini dhidi ya CF Mounana ya Gabon.
Mechi za awali za michuano hiyo zitaanza kuchezwa kati ya Februari 13-15 na zile za marudiano zitakuwa Machi 28-Machi 1.
Ratiba kamili ya michuano hiyo Ligi ya Mabingwa ipo hivi;
No comments:
Post a Comment