STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 22, 2014

Sadiki Momba kuwania ubingwa wa WBO Ghana

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEix3VuE4iWjFp3iKQhLtRkqdBKWUAD5xOHaI9e5j0VmRfJR4QLZz2vJcq1WwjEnBnWJjH8ls-TAJM76Z-VNT4Q2YoyzJgBAHmH5kedVdyjnEmVEsa2cVFSIPZHS-a2LASixt3y1g5BFH7bw/s1600/IMG_6645.JPG
Momba (Kushoto) akiwa katika moja na mapambano yake ya ngumi nchini
BONDIA Sadiki Momba ameondoka nchini kwenda Ghana kwa ajili ya kupanda ulingoni siku ya Krismasi kuwania ubingwa wa WBO-Mabara dhidi ya mwenyeji wake, Emmanuel Tagoe.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania, PST, Anthony Rutta, Momba aliondoka nchini juzi Jumamosi kwa Ndege ya Shirika la Kenya Airways na atapanda ulingoni kwenye uwanja wa michezo wa Accra, mjini Accra siku za Desemba 26.
Rutta alisema pambano hilo la uzani wa Light (lightweight) litakuwa la raundi 12 na litakuwa nafasi nyingine kwa Mtanzania huyo kulipa kisasi kilichomkuta bondia mwenzake mapema mwezi huu Allan Kamote alioyepigwa kwa KO katika kuwania ubingwa wa dunia wa WBO.
"Baada ya Allan Kamote kupigwa kwa KO na George Ashie Desemba 5, safari hii PST imempeleka Sadiki MOmba kupigana na Mghana Emmanuel Tagoe kuwania ubingwa wa Mabara wa WBO pambano litakalochezwa mjini Accra, Ghana DEsemba 26," alisema Rutta.
Kwa muda mrefu mabondia wa Tanzania wamekuwa hawafanyi vizuri kila wanapoenda kupambana nje ya nchi hali ambayo imekuwa ikizua maswali mengi, japo mamlaka zinazosimamia ngumi hizo zimekuwa zikijitetea kuwa inatokana na maandalizi duni.

No comments:

Post a Comment