MABINGWA watetezi wa Serie A ya nchini Italia, Juventus, imezidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya usiku huu kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Torino.
Katika pambano hilo lililochezwa kwenye mjini wa Turin, wenyeji walijikuta wakimaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya beki waoStephan Lichtsteiner kulimwa kadi nyekundu kutokana na kupewa kadi ya pili ya njano.
Wenyeji hao walitangulia kuandika bao mapema kupitia kwa Arturo Vidal kwa mkwaju wa penati iliyotolewa na mwamuzi dakika ya 15 kabla ya wageni wao kurejesha bao hilo dakika saba baadae kupitia kwa Bruno Peres.
Wakati wengi wakidhani matokeo yangeisha kwa sare ya 1-1, kiungo mkongwe Andrea Pirlo aliifungia Juventus bao muhimu la ushindi dakika za lala salama na kuifanya 'Kibibi' cha Turin, kufikisha jumla ya pointi 34 kutokana na michezo 13.
MUda mchache ujao wanaoshikilia nafasi ya pili AS Roma wenye pointi 28 watakuwa nyumbani kuwakaribisha Inter Milan katika pambano linalotarajiwa kuwa kali.
No comments:
Post a Comment