Daren Wilson Afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuua kijana
mweusi nchini Marekani amejiuzulu. Wakili wa Darren Wilson ambaye ni
afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuua kijana mweusi Michael Brown
kwenye eneo la st Louis nchini Marekani mwezi Agosti anasema kuwa polisi
huyo amejiuzulu.
Mapema wiki hii bwana Wilson aliondolewa mashtaka hatua iliyozua
ghadhabu miongoni mwa waamerika weusi.Afisa huyo amekuwa likizoni tangu
mauji hayo yafanyike, mauaji ambayo yalisababisha majuma kadha ya
maandamano.
Michael Brown,kijana mweusi nchini Marekani alipigwa risasi na
kuuawa. Gazeti la St Louis limesema kuwa afisa huyo mwenye miaka 28
aliamua kujiuzulu baada ya kitengo chake cha polisi kupokea vitisho
kwamba ghasia zitafutia iwapo ataendelea kuhudumu kama mfanyikazi.
Gazeti hilo lilichapisha kile lilichodai kuwa barua yake ya kujiuzulu
ambayo ilisoma:''nimearifiwa kwamba iwapo nitaendelea kuwa mfanyikazi
wa idara ya Polisi basi hatua hiyo itawachochea maafisa wa polisi na
raia wa eneo la Furguson kuishi kwa hofu,hali ambayo siwezi kuikubali
hata kidogo.''
No comments:
Post a Comment