WENYEJI
wa Fainali za Afrika za 2023, Guinea imeweka bayana kwamba hatakubali kuhamisha michuano hiyo toka mwanzoni mwa mwaka na kufanyika katikati ya mwaka kama FUIFA inavyotaka.
Wenyeji hao wamesema kuwahawakubaliani na fainali za Mataifa ya Afrika za
mwaka 2023 kuchezwa mwezi Juni ili kuziwezesha fainali za Kombe la Dunia
kufanyika Qatar, alisema waziri wao wa michezo.
Domani Dore alipingana
na taarifa ya Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) Jerome
Valcke, ambaye wiki iliyopita alisema kuwa, fainali za Mataifa ya Afrika 2023
zinatakuwa kusogezwa mbele kwa miezi sita hadi Juni kutoka katika muda wake wa
kawaida wa mwezi Januari.
Fainali za Kombe
la Dunia za mwaka 2022 zimepangwa kufanyika Novemba na Desemba, kufuatia
mapendekezo ya kamati ya maandalizi.
Valcke alisema
kuandaa fainali za Kombe la Dunia mwezi mmoja baadae ni jambo lisilowezekana,
na aliongeza kuwa anakubaliana na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kuhamisha
fainali hizo zinazoshirikisha jumla ya timu 16 baadae mwaka huo.
Hatahivyo, Guinea,
imesema kuwa itapinga tarehe hizo mpya.
"hatuwezi
kuandaa fainali za Mataifa ya Afrika mwezi Juni, ni kipindi cha mvua, “’alisema
Dore alipozungunza na televisheni ya Guinea.
"Caf walitakiwa
kusikiliza ushauri wa Guinea kuwa kama sisi ni taifa tunatakiwa kuamua tarehe
gani zifanyike. Tunaelewa matatizo yanayolizunguka Kombe la dunia na kugongana
na fainali za Mataifa ya Afrika.
"Lakini Caf walitakiwa
kusikilisha maoni yetu. Mwezi juni , haiwezekani, " aliongeza Dore.
Shirikisho hilo la
Soka la Afrika limesisitiza kuhusu fainali Mataifa ya Afrika 2023 nchini Guinea,
likisema kuwa "Uamuzi kuhusu Afcon 2023 utatolewa na Kamati ya Utendaji ya
CAF, na sio mtu mwingine, wakati utakapofika."
No comments:
Post a Comment