Wazee wa Uturuki watakaovaana na Ashanti Utd kesho Taifa |
Ashanti Unitrd weatakubali 5 nyingine kwa Yanga? |
MZUNGUKO wa pili wa
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza kesho
(Januari 25 mwaka huu) kwa mechi nne zitakazochezwa katika miji ya
Bukoba, Dar es Salaam na Tanga.
Mabingwa watetezi
Yanga watakuwa wageni wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
wakati kwenye jiji hilo hilo Uwanja wa Azam Complex kutakuwa na mechi
kati ya wenyeji Azam FC na Mtibwa Sugar kutoka Morogoro.
Coastal Union na
Oljoro JKT zitaumana kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Kagera
Sugar ikiikaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Raundi ya 14 ya ligi
hiyo itaendelea Jumapili (Januari 26 mwaka huu) kwa mechi mbili. Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa shuhuda wa mechi kati
ya Simba na Rhino
Rangers kutoka Tabora wakati maafande wa JKT Ruvu na Mgambo Shooting
watapambana Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Viingilio kwenye
mechi ya Ashanti United na Yanga vitakuwa sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Viingilio mechi ya Mkwakwani vitakuwa sh. 10,000 kwa sh. 3,000, Uwanja wa
Azam Complex sh. 10,000 kwa sh. 3,000, Uwanja wa Kaitaba ni sh. 5,000
kwa sh. 3,000.
No comments:
Post a Comment