STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, January 24, 2014

Juma Jabu kuwakosa Yanga kesho Taifa

Juma Jabu enzi akiwa Simba
BEKI wa zamani wa Simba na Coastal Union aliyetua Ashanti United, Juma Jabu 'Jay Jay', amesikitika kuwakosa mabingwa watetezi Yanga wanaorejea leo kutoka Uturuki katika mechi yao ya la Ligi Kuu Tanzania Bara itakayochezwa kesho.
Beki huyo wa pembeni hatacheza mechi hiyo itakayochezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutokana na kutingwa na majukumu yake ya masomo kwani kwa sasa mchezaji huyo anasoma katika Chuo cha DSI.
Akizungumza na MICHARAZO, Jabu alisema alikuwa na hamu kubwa ya kuivaa Yanga katika mechi hiyo, lakini amelazimika kuomba ruksa kwa 'mabosi' wake ili kujiandaa na mitihani.
Jabu alisema kwa sasa anasomea masomo ya 'Clearing and Forwading' katika chuo hicho na hivyo kipindi hiki yupo katika mitihani, japo mechi ijayo ambayo Ashanti itaikaribisha Mgambo JKT uwanja wa Chamazi, atakuwepo.
"Nasikitika sitaweza kucheza mechi ya Jumamosi dhidi ya Yanga kwa sasa nipo kwenye mitihani, lakini mechi ijayo dhidi ya Mgambo naamini nitaanza kuitumikia rasmi klabu yangu ya Ashanti niliyorejea tena," alisema.
Jabu, alisema anaamini wachezaji wenzake chini ya kocha mpya Abdallah Kibadeni, wataiduwaza Yanga waliokuwa wakijifua Uturuki kwa karibu wiki mbili kwa kuipa kipigo ili kulipa kisasi cha mabao 5-1 walichopewa katika mechi ya kwanza ya msimu huu.
Beki huyo aliyeichezea Ashanti United iliposhiriki Ligi Kuu kwa mara ya kwanza mwaka 2004-2007, ni miongoni mwa wachezaji 15 walioongezwa kwenye kikosi cha Ashanti kwenye usajili wa dirisha dogo.

No comments:

Post a Comment