Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom nchini Tanzania Bara, Yanga
wameshawasili salama jijini Dar es salaam wakitokea jijini Antalya
nchini Uturuki walipokuwa wameweka kambi ya wiki mbili kwa ajili ya
maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya Ligi ya
Mabingwa Afrika.
Young Africans imetua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl JK Nyeree
majira ya saa 9:30 alfajiri kwa shirika la ndege la Turkish Airline na
moja kwa moja kikosi cha wachezaji 27 na benchi la Ufundi kimeingia
kambini kujiandaa na mchezo huo wa kesho.
Kocha mkuu wa Young
Africans Hans Van Der Plyum amesema anashukuru kikosi chake kimefika
salama jijini Dar es salaam na amesema vijana wake watafanya mazoezi
mepesi leo jioni kabla ya kesho kushuka dimba la Uwanja wa Taifa.
Akiongelea
kambi ya Antalya Hans amesema kambi ilikuwa nzuri na mafanikio makubwa
kwani vijana wameonyesha uwezo wa hali ya juu katika nidhamu, kujituma,
upendo na kushirikiana kitu ambacho ndio nguzo ya timu kufanya vizuri.
Aidha
Hans amewaomba wanachama wa Young Africans, wapenzi na washabiki kesho
kujitokeza kwa wingi kuja kuishuhudia timu yao iliyokuwa kambini Uturuki
itakapocheza na wauza mitumba wa Ilala Ashanti United na kuitambulisha
staili yao ya uchezaji kutoka Antalya.
No comments:
Post a Comment