Yanga |
Yanga ililazimishwa suluhu na Ndanda jana katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa jkwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuwafanya washindwe kukalia kiti cha uongozi wa ligi hiyo unaoshikiliwa na Azam waliopo DR Congo, japo imerejea katika nafasi ya pili walioshushwa Jumamosi na Mtibwa Sugar.
Sare hiyo ya jana imeifanya Yanga kufikisha pointi 19 baada ya mechi 11, mbili nyuma ya Azam waliolingana nao kimichezo ambao kesho wanatarajiwa kumalizia mechi zao nchini Congo baada ya juzi kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya wenyeji wao TP Mazembe.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema wanatarajia kwenda Tanga kwa mechi tyao ya Jumatano wakiwa na nia mopja ya kuhakikisha wanapata ushindi kama ilivyofanya wiki iliyopita mjini Morogoro walipowafunga maafande wa Polisi kwa bao 1-0.
Muro alisema wanatambua pambano hilo litakuwa gumu kutokana na ukweli Coastal Union watakuwa nyumbani na hawajafanya vema katika mechi zao za karibuni, lakini wao hawatajali hilo zaidi ya kupata ushindi ili kujiweka katika nafasio nzuri ya kunyakua taji hilo.
"Matokeo dhidi ya Ndanda ni ya kawaioda katika mchezo na sasa tunajipanga kwa mechi ijayo dhidi ya Coastal Union tutakaowafuata Mkwakwani kwa dhamira moja ya kuvuna pointi," alisema Muro.
Tangu ligi iendelee tena baada ya mapumziko ya Novemba 9, Yanga imevuna pointi sita tu katika mechi nne ilizocheza mpaka sasa baada ya kutoka sare ya 2-2 na Azam kisha kulazimishwa suluhu na Ruvui Shooting kabla ya kuwazabua Polisi Moro na kubanwa na Ndanda.
No comments:
Post a Comment